MKUU WA MKOA MH.ROSEMARY SENYAMULE. Na Shadaiya S Hassan ELIMU YA MSINGI Katika mkoa wa DODOMA bajeti ya fedha za mpango wa elimu bila malipo kwa shule za msingi imeongezeka kutoka sh.4,466,566,533.72 mwaka 2022/2021 hadi sh.6,903,484,140.63 mwaka 2022/2023 sawa na ongezeko la asilimia 54.56 Shule za msingi za serikali zimeongezeka Kutoka shule 736 mwaka 2022/2021 hadi shule 784 mwaka 2022/2023 sawa na ongezeko la asilimia 6.52 Zimeanzishwa shule mbili za msingi zinazofundisha kwa kutumia lugha ya kingereza yaani ENGLISH MEDIUM katika halmashauri ya Bahi na Dodoma jiji. Vyumba vya madarasa kwa shule za msingi kutoka 5812 mwaka 2020/2021 hadi 6205 mwaka 2022/2023 hili ni ongezeko la vyumba 393, madarasa haya yamejengwa kupitia mradi wa waTCRP ,mradi wa LANES ,kupitia serikali kuu na mapato ...