MKUU WA MKOA MH.ROSEMARY SENYAMULE.
Na Shadaiya S Hassan
ELIMU YA MSINGI
Katika mkoa wa DODOMA bajeti ya fedha za mpango wa elimu bila malipo kwa shule za msingi imeongezeka kutoka sh.4,466,566,533.72 mwaka 2022/2021 hadi sh.6,903,484,140.63 mwaka 2022/2023 sawa na ongezeko la asilimia 54.56
Shule za msingi za serikali zimeongezeka Kutoka shule 736 mwaka 2022/2021 hadi shule 784 mwaka 2022/2023 sawa na ongezeko la asilimia 6.52
Zimeanzishwa shule mbili za msingi zinazofundisha kwa kutumia lugha ya kingereza yaani ENGLISH MEDIUM katika halmashauri ya Bahi na Dodoma jiji.
Vyumba vya madarasa kwa shule za msingi kutoka 5812 mwaka 2020/2021 hadi 6205 mwaka 2022/2023 hili ni ongezeko la vyumba 393, madarasa haya yamejengwa kupitia mradi wa waTCRP ,mradi wa LANES ,kupitia serikali kuu na mapato ya ndani ya halmashauri 💪💪.
ELIMU YA SEKONDARI
Fedha za mpango wa elimu ya sekondari bila malipo imeongezeka kutoka sh.4,585,462,268.12 mwaka 2020/2021 hadi sh.7,549,386,970.44 mwaka 2022/2023 sawa na ongezeko la asilimia 64.63 .
Shule zimeongezeka kutoka shule 193 mwaka 2020/2021 hadi 218 mwaka 2022/2023 hili ni ongezeko la shule mpya 25 ndani ya mkoa💪
Vyumba vya madarasa kutoka 2226 mwaka 2020/2021 hadi 3256 mwaka 2022/2023 hili ni ongezeko la madarasa 2030 ndani ya mkoa ambayo yametokana na mradi wa TCRP, fedha za SEQUIP , fedha za tozo,fedha kutoka serikali kuu,na kupitia mapato ya ndani ya halmashauri💪.
SAMBAMBA NA HAYA SERIKALI YA MKOA WA DODOMA IMEENDELEA KUHAKIKISHA HUDUMA ZINATOLEWA KWA VIWANGO ILI WANANCHI WAENDELEE KUONA UMUHIMU WA MADARASA HAYA NA MCHANGO MZIMA WA SERIKALI KWENYE ELIMU.
∆ WAKIULIZA WAJIBUNI KWA HOJA MIAKA MIWILI YA HESHIMA KUBWA ,MIAKA 63 YA DHAHABU ,MIAKA 46 YA KIJANI.
Comments
Post a Comment