Mila potofu katika
jamii ya kimasai imetajwa kuwa changamoto kwa maafisa ustawi wa jamii wa
halimashauri ya wilaya ya Ngorongoro kutokana na kukosa ushirikiano wa
kutatua Tatizo la ukeketaji kwa jamii hiyo.
Akizungumza na waandishi ya habari Afisa Ustawi Wa jamii Bwana ALOYCE LOLIKISWALI katika semina iliyoandaliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu
Sanyansi na Utamaduni UNESCO kwa lengo la kupinga ukeketaji wa wanawake amesema
kukosekana kwa ushirikiano kwa jamii imekuwa ni changamoto ambayo imepelekea
kushindwa kudhibiti ukeketaji pamoja na ukatili wa kijinsia.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Malaigwanan Bwana JOSEPH TIRIPAI
amebainisha kuwa mila na desturi zao zitabadilika kulingana na wakati lakini watahakikisha
wanalinda watoto wanaozaliwa kutokeketwa na kusisitiza elimu kuendelea kutolewa
hususani shuleni.
Katika hatua nyingine mratibu wa afya ya mama na mtoto
ameeleza kuwa wanawake wajawazito waliokeketwa wanalazimika kujifugua kwa upasuaji na kupelekea wengi wao
kushindwa kufika katika zahanati na kujifungulia nyumbani huku wengi wao wakipoteza
maisha
Kwa upande wa sheria ya Tanzania ukeketaji ni kosa la
jinai na endapo mhusika akikamatwa atahukumiwa kifungo cha miaka 5 hadi 15 huku
wahusika wakibainishwa kuwa ni wazazi ndio wanachaingia ukeketeji kwa wtoto wa
kike.
Takwimu zinaonyesha kuwa Katika suala la ukeketaji wa wanawake mkoa wa Manyara unaongoza
ukiwa na asilimia 58 ukifuatiwa na Mkoa wa Dodoma asilimia 47,Arusha asilimia 41 Mara asilimia
32 na Siginda ikiwa na Asilimia 3.
Na,Mindi
Joseph Dodoma FM
Nikwann mnapenda sana kusemea mkoa Mara na kuupa kipaumbele na wakati Kuna mikoa inaongoza kwa aslimia kubwa no mom samson chachs
ReplyDelete