Skip to main content

Posts

Showing posts with the label JAMII

KISHINDO CHA SERIKALI YA AWAMU YA SITA MKOA WA DODOMA CHINI YA MKUU WA MKOA MH.ROSEMARY SENYAMULE.

                                     MKUU WA MKOA  MH.ROSEMARY SENYAMULE. Na Shadaiya S Hassan   ELIMU YA MSINGI   Katika mkoa wa DODOMA bajeti ya fedha za mpango wa elimu bila malipo kwa shule za msingi imeongezeka kutoka sh.4,466,566,533.72 mwaka 2022/2021 hadi sh.6,903,484,140.63 mwaka 2022/2023 sawa na ongezeko la asilimia 54.56  Shule za msingi za serikali zimeongezeka Kutoka shule 736 mwaka  2022/2021 hadi shule 784 mwaka 2022/2023  sawa na ongezeko la asilimia 6.52  Zimeanzishwa shule mbili za msingi zinazofundisha kwa kutumia lugha ya kingereza yaani ENGLISH MEDIUM katika halmashauri ya Bahi na Dodoma jiji. Vyumba vya madarasa kwa shule za msingi kutoka 5812 mwaka 2020/2021 hadi 6205 mwaka 2022/2023 hili ni ongezeko la vyumba 393, madarasa haya yamejengwa kupitia mradi wa waTCRP ,mradi wa LANES ,kupitia serikali kuu na mapato ...

WANANCHI WATAKIWA KUKAA MBALI NA SIMU /KOMPUTA KUEPUKA KUUMWA MACHO

             Wananchi wanaotumia simu na Komputer kwa muda mrefu wameshauriwa kukaa umbali wa sentimita 25 kutoka macho yalipo mpaka katika vifaa hivyo ili kuepuka magonjwa ya Macho. Ushauri huo umetolewa na Daktari bingwa wa macho kutoka Hospitali ya Charity Vision Tanzania iliyopo Jijini Dodoma Dokta EDMUND MUSHUMBUSI  wakati akizungumza na Dodoma FM. Dr Mushumbusi   amesema ili kuepuka matatizo yatokanayo na matumizi ya muda mrefu ya vifaa hivyo kama maumivu ya kichwa ni vyema mtu akaweka umbali wa sentimita 25 pamoja na kupumzika kila baada ya muda ili kuyapumzisha macho. Akizungumzia shida anayoweza kuipata mtu anayetumia vifaa hivyo kwa muda mrefu ni maumivu ya kichwa,kuchoka au kuuma kwa macho, kutokuona vizuri pamoja na maumivu ya shingo na mgongo. Amesema kama ilivyo kawaida ya kupumzisha viungo vingine vya mwili macho pia yana takiwa kupumzika kutokana na kuwa na umuhimu mkubwa kwa binadamu. Na Ph...

WASHAURIWA KUTUMIA MBOLEA KULIMA KILIMO BORA

      Wakulima katika kijiji cha chikopole wilaya ya Bahi mkoani Dodoma wameshauriwa kutumia njia mbadala ya kufikisha mbolea mashambani mwao ili   kulima kilimo bora. Ushauri huo unakuja baada ya kuwepo na changamoto za kutokuwa na nyenzo za kuwasaidia wakulima hao kufikisha mbolea kwa wingi na kwa muda husika mashambani mwao jambo linalopelekea kutofikia dhamira katika kilimo chao. Akizungumza na Dodoma FM ofisini kwake afisa kilimo na mifugo wa kijiji cha Chikopelo Bwana DANIEL CHUNGA amesema ni kweli changamoto hiyo ipo lakini kila mara wamekuwa wakiwashauri wakulima hao kuanza mapema kusogeza mbolea karibu na mashamba yao kufuatia kuishi karibu na wanapofanyia shughuli zao za kilimo. Bwana CHUNGA amesema pamoja na changamoto hizo wakulima hao wanakabiliwa na mwingiliano kati yao na wafugaji kwani katika kijiji hicho hakuna mpangilio maalumu wa sehemu gani wafugaji wanapaswa kuchungia mifugo yao na badala yake mashamba ya wakulima hutumi...

WANANCHI WASHAURIWA KUFUATA KANUNI ZA UNUNUZI WA ARDHI

        Jamii imetakiwa kufuata taratibu za kisheria katika ununuzi wa ardhi ili kuepuka migogoro ya ardhi inayojitokeza mara nyingi miongoni mwa familia. Rai hiyo imetolewa na Mwanasheria wa Kujitegemea Bwana Goodluck Ludala ambapo amesema migororo mingi ya ardhi inatokana na watu kutokufuata taratibu za kisheria za manunuzi ambapo inaweza kupelekea mtu kupoteza haki yake . Amesema iwapo mtu atapata migogoro ya ardhi anatakiwa kupeleka shauri lake baraza la kata na baada ya uamuzi kutoka mlalamikaji anapaswa kukaza hukumu katika baraza la ardhi la wilaya jambo ambalo watu wengi huwa hawafanyi na kupoteza haki zao. Aidha amesema kumekuwa na baadhi ya watu wanaopuuza hukumu ya mahakama pasipo kukata rufaa ambapo ameeleza kuwa kufanya hivyo ni kosa kisheria na hapo mlalamikaji anapaswa kutoa taarifa katika mahakama iliyotoa hukumu ili hatua zaidi zichukuliwe. Haya Yamejiri ikiwa ni siku chache baada ya Dodoma FM   kupokea kisa cha m...

SERIKALI KUSHIRIKIANA NA WAGANGA WA TIBA ASILI KUBAINI WANAOUA ALBINO

                                           Serikali imeahidi kutoa ushirikiano kwa waganga wa tiba asili katika jitihada za kuwabaini watu wanaojihusisha na mauaji ya vikongwe na watu wenye Ualbino. Hatua hiyo imekuja kufatia hivi karibuni waganga wa tiba asili kuomba kupewa ushirikiano na serikali wakati wa zoezi la kusajili waganga hao ili kubaini waganga wabaya na wazuri jambo ambalo litasaidia kuwabaini waganga matapeli wanaojihusisha na vitendo hivyo. Akiongea na umoja wa waganga wa tiba asili na wakunga ( UWAWATA) pamoja na watu wenye ualbino Mwenyekiti wa bunge la Jamhuri ya muungano wa Tanzania  Mussa Zungu amesema kuwa waganga wabaya wataendelea kuwepo iwapo wateja wabaya watakuwepo hivyo waganga wote watoe ushirikiano kwa vyombo vya dola ili hatua zichukuliwe dhidi ya wale watakaobainika. Naye kamanda wa polisi mkoa wa Dodoma  G...

SERIKALI :SIYO JUKUMU LETU KUGHARAMIA MAZISHI YA WAZAZI WA WATUMISHI

                                                                          Serikali imesema haina jukumu la kugharamia huduma za mazishi wazazi   wa mtumishi wa umma wanapofariki kutokana na baadhi ya wazazi kuwa na watoto zaidi ya mmoja. Naibu waziri ofisi ya Rais tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEM) Mh. Joseph Kakunda ameyasema hayo leo Bungeni Jijini Dodoma kwa niaba ya Waziri ofisi ya Rais utumishi na utawala bora wakati akijibu swali la Mbunge Kosato Chumi aliehoji ni lini Serikali itawajumuisha wazazi wa mtumishi kama wanufaika wa huduma mbalimbali anazopata mtumishi wa umma. Amesema kwa mujibu wa kanuni za kudumu katika utumishi wa umma inaelekeza huduma za mazishi kutolewa kwa mtumishi mwenyewe pamoja na wategemezi wa nne na uwepo wa kanuni hiyo imesaidia Serikali kue...

SERIKALI YAAHIDI KUPANDISHA MISHAHARA HALI YA UCHUMI ITAKAPOIMARIKA

Waziri wa Nchi ofisi ya Rais utumishi na utawala bora Kapten George Mkuchika amesema Serikali ya awamu ya tano inaendelea kuboresha masilahi ya watumishi wa umma na itapandisha mishahara kwa watumishi hao baada ya hali ya uchumi wa Nchi kuimarika. Waziri Mkuchika ameyasema hayo leo Bungeni Jijini Dodoma wakati akijibu swali la Mbunge wa viti maalumu Mh. Catherin Magige aliehoji Serikali ya awamu ya tano ina mikakati gani ya kuwajali watumishi wa umma katika masilahi yao. Kapten Mkuchika amesema Serikali imekuwa ikifanya juhudi mbalimbali katika kuboresha masilahi ya watumishi wa umma kwa kuwapatia mikopo, kuwapeleka mafunzo katika taaluma mbalimbali na zoezi la kupandisha mishahara litafanyika wakati wowote hali ya uchumi wa Nchi utakapo ruhusu. Katika hatua nyingine Kapten Mkuchika amekanusha taarifa za zuio kwa wakurugenzi wa Halimashauri, Manispaa pamoja na Majiji juu ya kuto kuwatangaza wapinzani iwapo wameshinda katika chaguzi mbalimbali kutokana na wak...

WATAMANI KUENDELEZA VITENDO VYA UKEKETAJI WAOGOPA SHERIA

            Pamoja na elimu inayoendelea kutolewa juu ya madhara ya ukeketaji bado kuna baadhi ya maeneo yanaonesha kuendeleza vitendo hivyo vya kikatili kwa wanawake. Dodoma fm imezungumza na baadhi ya wazee wa kimila katika kijiji cha Chikopelo wilayani Bahi ambao wameonesha kutamani kuendeleza vitendo hivyo isipokuwa wanaogopa vyombo vya sheria. Kutokana na imani ya wazee hao kituo hiki kimezungumza na kaimu mganga mkuu mkoa Dodoma Mzee Nasoro ambae amesema mwanamke aliyekeketwa anapata madhara makubwa wakati wa kujifungua ikiwamo kupoteza damu nyingi na hata kupelekea kifo kwa mtoto. Nae mgaguzi msaidizi wa polisi kutoka dawati la jinsia na watoto Lovie Mhena amesema Vitendo vya ukeketaji vimetajwa kuwa ni kosa la jinai kwa mujibu wa sheria ambapo adhabu yake ni kifungo cha miaka 30 jela. Kutoka mtandao wa wanawake Tanzania bi Sara Mwaga anasema pamoja na tafiti kuonesha dodoma inashika nafasi ya pili katika ukeketaji lakin...

JIJI LA DODOMA LAINGIZWA KATIKA MASHINDANO YA KITAIFA USAFI WA MAZINGIRA

                                                 Uongozi wa jiji la Dodoma umewaomba wananchi  kuendelea kudumisha hali ya usafi ili jiji la Dodoma liweze kuibuka kidedea katika mashindano  ya kitaifa ya usafi wa mazingira. Ushindanishwaji huo utayahusisha majiji yote nchini, jiji la Dodoma likiingia kwa mara ya kwanza katika kinyang’anyiro hicho, na uongozi wa Jiji hilo kuahidi ushindi. Akielezea namna jiji la Dodoma lilivyojipaga   kufanya vizuri katika utunzaji wa mazingra na kupata ushindi, mkuu wa idara ya mazingira na udhibiti wa taka ngumu jiji Dodoma bwna Dickson Kimaro amesema mkoa haupo tayari kumuangusha rais kwa maamuzi yake yenye busara ya kuufanya Mkoa wa Dodoma kuwa jiji, na kuwataka wananchi wote kushiriki kuyatunza mazingira. Aidha bwna Kimaro amewataka watu kuacha kutupa taka kiholela, badala yake watupe katika maeneo y...

KAMANDA MUROTO AWATOA WASI WASI WAKAZI WA DODOMA KUELEKEA SIKUKUU YA IDDI

Katika kuelekea sikukuu ya Eid alfitiri Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma limeendelea kuimarisha ulinzi ili kuhakikisha sikukuu inasheherekewa kwa utulivu  pamoja na kuwakamata wahalifu wa makosa mbalimbali. Akizungumza na waandishi wa habari Ofisini kwake   Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma GILLES MUROTO amesema jeshi la polisi limekuwa likifanya msako wa nyumba kwa nyumba ili kuhakisha wanadhibiti uhalifu na wahalifu na wote watakaokamatwa watafikishwa mahakamani. Kamanda MUROTO amesema jeshi la polisi limekamata zaidi ya watu 25 kwa makosa tofauti tofauti ikiwemo ya uvunjaji, utapeli, bangi na uuzaji wa bidhaa za vipodozi vyenye viambata vya sumu. Sambamba na hayo ametoa wito kwa wananchi kuendelea kutoa taarifa za wahalifu na uhalifu ili jiji la Dodoma liweze kuwa shwari wakati wote. Kwa upande wao wananchi wamesema ni vyema vijana wa kafanya kazi kwa bidii na kuliomba jeshi la Polisi liendelee kuchukua hatua kwa wahalifu wanaowakamata. Na P...

SERIKALI YAOMBWA KUZINGATIA VIGEZO VYA USAJILI WAGANGA TIBA ASILI

Serikali imeombwa kuzingatia vigezo muhimu vinavyotakiwa wakati wa zoezi la kusajili Waganga wa tiba asili ili kuondoa sintofahamu iliyopo kati ya serikali na waganga wa tiba asili ambao wamekuwa wakituhumiwa kujihusisha na imani za kishirikina zinazopelekea uwepo wa mauaji ya watu wenye ualbino nchini. Kauli hiyo imetoewa na mke wa waziri mkuu mstaafu mama Tunu Pinda wakati akifungua semina ya siku moja mjini Dodoma iliyoandaliwa na shirika la Hope Derivery Foundation iliyowakutanisha watu wenye ualbino na waganga wa tiba asili kwa lengo la kuondoa sintofahamu iliyopo baina ya makundi hayo mawili. Amesema kuwa serikali ni vyema ikazingatia mambo muhimu wakati wa kuwasajili waganga hao kwa kuwashirikisha viongozi mbalimbali wa maeneo husika   ili kwatambua waganga halali na matapeli na sio kutumia vigezo vya mganga kuwa na matunguli pekee hali itakayosaidia kukomesha mauaji hayo kwanni wengi wao wanaojuhusisha na vitendo hivyo ni wale matapeli. Kwa u...