Wakulima katika
kijiji cha chikopole wilaya ya Bahi mkoani Dodoma wameshauriwa kutumia njia
mbadala ya kufikisha mbolea mashambani mwao ili kulima kilimo bora.
Ushauri huo unakuja
baada ya kuwepo na changamoto za kutokuwa na nyenzo za kuwasaidia wakulima hao
kufikisha mbolea kwa wingi na kwa muda husika mashambani mwao jambo
linalopelekea kutofikia dhamira katika kilimo chao.
Akizungumza na
Dodoma FM ofisini kwake afisa kilimo na mifugo wa kijiji cha Chikopelo Bwana
DANIEL CHUNGA amesema ni kweli changamoto hiyo ipo lakini kila mara wamekuwa
wakiwashauri wakulima hao kuanza mapema kusogeza mbolea karibu na mashamba yao
kufuatia kuishi karibu na wanapofanyia shughuli zao za kilimo.
Bwana CHUNGA
amesema pamoja na changamoto hizo wakulima hao wanakabiliwa na mwingiliano kati
yao na wafugaji kwani katika kijiji hicho hakuna mpangilio maalumu wa sehemu
gani wafugaji wanapaswa kuchungia mifugo yao na badala yake mashamba ya
wakulima hutumika kwa ajili ya malisho pale wanapokuwa wamevuna .
Ikumbukwe wananchi
katika kijiji cha Chikopelo wengi wao ni wakulima na hutumia kilimo kujikwamua na
njaa pamoja na kiuchumi lakini changamototo walizo nazo zinachangia kutofikia
malengo yao.
Na
RWEIKIZA KATEBALIRWE DODOMA FM
Comments
Post a Comment