Skip to main content

Posts

Showing posts with the label MICHEZO

HABARI MOTOMOTO KUTOKA KATIKA MAGAZETI YA LEO FEBRUARY 4,2023

 

HIZI HAPA AJENDA ZA MKUTANO MKUU WA DHARURA WA SIMBA

                              Uongozi wa klabu ya Simba umetangaza ajenda nne zitazako jadiliwa katika mkutano mkuu wa dharura wa mabadiliko ya katiba utakaofanyika Mei 20. Mkutano huo unatarajia kuanza saa 3 asubuhi katika ukumbi wa Kimataifa wa mikutano wa Mwalimu Nyerere Convention Center. Ajenda hizo ni 1. Kufungua Mkutano. 2. Kusoma mapendekezo ya marekebisho ya maboresho ya katiba ya Simba Sports Club. 3. Kupokea na kupitisha/ kutopitisha marekebisho/maboresho ya Karina. 4. Kufunga Mkutano.

NINJE TUNAENDA KUPINDUA MATOKEO MALI

Kocha mkuu wa timu ya Taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 20 'Ngorongoro Heroes' Ammy Ninje amesema wataweza kupindua matokeo katika mchezo wa marudiano dhidi ya Mali utakaopigwa wiki ijayo mjini Bamako. Ngorongoro ilikubali kipigo cha mabao 2-1 kutoka Mali jana katika uwanja wa Taifa, Dar es Salaam hivyo kujiweka kwenye mazingira mazuri ya kufuzu hatua inayofuata.                      Kocha Ninje amesema wachezaji wake walicheza vizuri lakini kuna makosa kidogo ambayo atayafanyia kazi kabla ya mchezo wa marudiano wiki ijayo. "Tuna nafasi ya kugeuza matokeo nchini Mali, tulicheza vizuri lakini tulishindwa kutumia nafasi tulizo tengeneza ila tumeona mapungufu yaliyojitokeza tutayafanyia kazi. "Mali hawakuwa bora sana kwetu ila walitumia vizuri nafasi walizopata na kufanikiwa kutufunga mabao mawili hata sisi tunaweza kufanya hivyo kwao," alisema Ninje. Ngorongoro itat...

MWIGULU:YANGA WAJITUME PESA WATAPATA

Wachezaji wa timu ya Yanga wameshauriwa kujituma ili kupata matokeo katika michuano ya kombe la Shirikisho Afrika ili kupata pesa nyingi ambazo zitaweza kutatua matatizo yanayo wakabili. Ushauri huo umetolewa na Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba na kusema kwa sasa wachezaji wa Yanga wanapaswa kutuliza akili na kuongeza jitihada katika michuano hiyo. Mwigulu amesema  kuwa anafahamu wachezaji wanadai pesa nyingi kwa klabu lakini kama watafanya vizuri watapata hela nyingi kuliko wanazodai. "Wachezaji wa Yanga wanapaswa kujitambua na kuelekeza akili katika michuano ya Shirikisho ambako wanaweza kupata kiasi kikubwa cha pesa kuliko wanachoidai klabu," alisema Mwigulu. "Wachezaji wa Yanga wanapaswa kujitoa sana katika mechi za makundi Afrika kwakua watapata pesa nyingi kwa mustakabali wa maisha yao," alisema Mwigulu.

HUDDERSFIELD TOWN YASALIA LIGI KUU

Alama moja katika uwanja wa Stamford Bridge umeihakikishia klabu ya Huddersfield kuwepo katika ligi kuu nchini Uingereza katika msimu ujao, matokeo ya leo yanawafanya kufikisha alama 37 katika msimamo wa ligi alama ambazo zinawahakikishia uwepo katika ligi kuu. Habari nyingine kubwa katika mchezo wa leo ni namna ambavyo kocha wa Chelsea Antonio Conte alikipanga kikosi chake akimuacha Eden Hazard nje pamoja na Olivier Giroud na alama moja waliyoipata hii leo inawaweka katika hatihati kushiriki Champions League msimu ujao. Suluhu ya leo ya Huddersfield inamaanisha kwamba timu zote zilizopanda daraja msimu huu zinabaki ligi kuu na hii ikiwa ni mara ya tatu katika historia ya Epl kwa jambo kama hili kutokea ambapo ilishatokea msimu wa 2001/2002(Blackburn, Fulham na Bolton) na ikatokea pia 2011/2012(Swansea, Norwich na Qpr). Kwingineko mabao mawili ya Riyad Mahrez na moja la Jamie Vardy yalitosha kuiua Arsenal bao 3 kwa 1, ambapo matokeo haya yanawafanya Arsenal kuwa ...

KOCHA WA PRISONS AIVUA UBINGWA YANGA

Kuelekea mchezo wa VPL kati ya Tanzania Prisons dhidi ya Yanga, Kocha mkuu wa Prisons Abdallah Mohamed ‘Bares’ ameivua ubingwa Yanga na kuipa Simba nafasi ya kushinda taji la ligi kuu msimu huu.   Bares amesema Simba inahitaji pointi moja kuwa bingwa wa ligi huku ikiwa na mechi tatu jambo ambalo linaiondoa Yanga katika mbio za ubingwa wa VPL 2017/18.                          “Tunaona tayari Yanga ameshaondoka kwenye mbio za ubingwa kwa sababu Simba anahitaji pointi moja kuwa mabingwa, mchezo dhidi ya Yanga ni muhimu sana kwetu kupata pointi tatu.”   “Nadhani Yanga wanakuja wakiwa wanajiandaa zaidi kwa mechi yao ya kimataifa, huu utakuwa mchezo wa kuandaa mazoezi ambayo yatawasaidia na mapungufu ambayo wameona kwenye mchezo waliofungwa 4-0 USM Alger. Nadhani kikubwa mwalimu atatazama hicho zaidi.”   “Kikosi changu kipo vizuri isipokuwa tutamkosa mchezaji mmoja Salum Kime...

KOCHA SINGIDA AAPA KULIPIZA KISASI DHIDI YA SIMBA

Kocha wa timu ya Singida United, Mholanzi, Hans van Der Pluijm kuelekea kwenye mechi yao dhidi ya Simba itakayopigwa kwenye Uwanja wa Namfua, amesema kuwa lazima walipe kisasi kwa wapinzani wao hao. Katika mchezo wa mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu Bara, Singida United ilipoteza kwa kufungwa mabao 4-0 dhidi ya Simba kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar.                         Pluijm alisema kuwa hiyo ni nafasi nzuri kwao kulipa kisasi kwa wapinzani wao hao waliowafunga mabao 4-0.                         

YANGA KUIVAA PRISONS LEO IKIWA NA WACHEZAJI PUNGUFU

Kikosi cha Yanga kinateremka dimbani Sokoine jioni ya leo kuvaana na Tanzania Prisons katika mchezo wa Ligi Kuu Bara.                          Uongozi wa Yanga umesema unataka kutengeneza heshima hata kama wataukosa ubingwa wa ligi kwa kushinda mechi zote zilizosalia. Yanga inashuka dimbani ikiwa pungufu kufuatia nyota wake kadhaa kusalia jijini Dar es Salaam ikilelezwa kuwa ni madai ya mshahara. Msafara wa Yanga haujaweka wazi orodha ya kikosi kilichosafiri kwa ajili ya mchezo dhidi yao na Prisons utakaoanza saa 10 leo. Timu zote mbili zimejivuna kupigania alama tatu kuelekea mechi hiyo inayosubiriwa kwa hamu kubwa na mashabiki wa soka jijini Mbeya.

SIMBA WAANZA SAFARI KUELEKEA SINGIDA, KIKOSI KITAPITA BUNGENI KUPOKEA BARAKA ZA MCHEZO

Kikosi cha Simba kimeanza safari ya kuelekea Singida kwa ajili ya mtanange wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Singida United. Simba itapitia katika Makao Makuu ya nchi, Dodoma, kuweka kambi fupi kabla ya kuendelea na safari ya kuelekea mjini Singida. Taarifa kwa mujibu wa Meneja wa kikosi hicho cha wekundu wa Msimbazi, Richard Robert, amesema kuwa kikosi kitapita jijini hapo ili kuweka kambi fupi kabla ya kuendelea na safari. Inaelezwa kuwa Simba wamepanga kupitia Bungeni kwa ajili ya kupata baraka za kuelekea mechi yao na Singida itakayopigwa Mei 12 kwenye Uwanja wa Namfua. Tayari kikosi hicho kipo njiani hivi sasa kuelekea jijini humo na kesho kitaanza tena safari ya Singida.

YANGA KUSHINDA MECHI ZOTE ZILIZOBAKI ILI KUZIMA KELELE ZA UBINGWA SIMBA

Baada ya kusalimu amri kwa kuipa nafasi Simba ya kuutwaa ubingwa wa ligi msimu huu, Yanga wamesema watapambana kushinda mechi zote zilizosalia.   Kupitia kwa Afisa wa Habari wa Yanga, Dismas Ten, ameeleza kuwa Yanga inahitaji heshima ya kushinda mechi zote zilizosalia ili kulinda heshima yao. Ten anaamini ushindi wa mechi zilizosalia utathibitisha kuwa wao ndiyo mabingwa wa taji la ligi mara tatu mfululizo pamoja na kuweka heshima ya kuonesha kuwa wao si wasindikizaji. Kikosi cha timu hiyo kipo Mbeya muda huu tayari kwa mchezo dhidi ya Tanzania Prisons utakaoanza majira ya saa 10 kamili jioni. Yanga imeenda Mbeya ikiwa na wachezaji pungufu huku ikiwa na dhamira ya kuwapunguza Simba shamrashamra za ubingwa kwa kuhakikisha kuwa inapata alama tatu muhimu.