Mganga
Mkuu wa Wilaya ya Bahi Jijini Dodoma Dk.Philipina Philipo amewatoa hofu
wakazi wa Wilaya hiyo juu ya taarifa za
kuwepo kwa madhara katika miti ya kivuli maarufu kama PANGA UZAZI ambayo imezua
hofu kwa wananchi hao.
Hoja
hiyo imeibuliwa katika kikao cha Baraza la Madiwani wa halmashauri hiyo ambapo
baadhi ya madiwani wameomba kupatiwa ufafanuzi kuhusu kuwepo kwa fununu kuwa
mti huo una madhara na kuongeza kuwa baadhi ya wananchi wameanza kuikata
wakihofia kupatwa na madhara hayo.
Akitoa ufafanuzi kuhusu miti hiyo Mganga Mkuu wa Wilaya Dk.Philipina Philipo amesema hadi hivi sasa hakuna utafiti wowote uliofanyika na kubainisha kuwa mti huo hauna madhara hivyo wananchi hawana haja ya kuhofia chochote.

Kutokana
na Majibu hayo ya DK PHILIPINA yamepelekea kuibua kwa hoja nyingine kwa
madiwani ambapo baadhi yao wametoa maoni tofauti tofauti juu ya ufafanuzi huo.
Kufuatia
hayo katibu tawala msaidizi mkoa anayeshughulikia masuala ya
Serikali za Mitaa Emmanuel Kuboja ambaye pia ni muwakilishi wa Mkuu wa Mkoa
naye akalazimika kutoa ufafanuzi wa kitaalamu juu ya miti hiyo
Pamoja na majibu hayo yalioonyesha kuwaridhisha madiwani hao Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Daniford Chisomi amewaomba wananchi kuendelea kuipanda miti hiyo kwa wingi kwani ina faida lukuki na haina madhara yoyote kama ilivyosemekana hapo awali.

Na,Mindi
Joseph Dodoma FM
Comments
Post a Comment