Mama wajawazito
wameshuriwa kutumia dawa aina ya FOLIC ACID katika kipindi cha miezi mitatu ya
mwanzo ya ujauzito ili kuepuka kupata mtoto mwenye mapungufu.
Rai hiyo imetolewa
na Daktari kutoka Hospitali ya Matovyolwa mjini Dodoma Dk.MUBARACK ISSA ALI wakati akizungumza na Dodoma
FM juu ya athari zitokanazo na mama kutotumia dawa hizo.
Dr Mubarack amesema
katika kipindi cha ujauzito mama huwa anapitia changamoto nyingi hivyo ni
vyema akatumia dawa aina ya FOLIC ACID ili kuepuka kupata mtoto mwenye tatizo
la mgongo wazi, kichwa kikubwa pamoja na upungufu wa damu.
Aidha Dk. Mubarack
amesema ili kuepuka kupata mtoto
njiti kipofu na kusababisha kifo kwa
mtoto ni vyema mama akaepuka matumizi ya
pombe, dawa za kulevya pamoja na
sigara kutokana na vitu hivyo kuwa ni
chanzo cha matatizo hayo kwa mtoto.
Sambamba na hayo
amewataka kina baba kuwa karibu na wake zao ikiwa ni pamoja na kuwajali na
kuwaonesha upendo katika kipindi chote cha ujauzito.
Lakini pia akina
mama wajawazito wametakiwa kuepuka kuvaa mavazi ya kuwabana katika kipindi
hicho pamoja na kuzingatia usafi.
Na
Phina Nimrod Chanzo:Dodoma FM
Comments
Post a Comment