Wananchi wanaotumia
simu na Komputer kwa muda mrefu wameshauriwa kukaa umbali wa sentimita 25
kutoka macho yalipo mpaka katika vifaa hivyo ili kuepuka magonjwa ya Macho.
Ushauri huo
umetolewa na Daktari bingwa wa macho kutoka Hospitali ya Charity Vision
Tanzania iliyopo Jijini Dodoma Dokta EDMUND MUSHUMBUSI wakati akizungumza na Dodoma FM.
Dr Mushumbusi amesema ili kuepuka matatizo yatokanayo na
matumizi ya muda mrefu ya vifaa hivyo kama maumivu ya kichwa ni vyema mtu
akaweka umbali wa sentimita 25 pamoja na kupumzika kila baada ya muda ili
kuyapumzisha macho.
Akizungumzia shida
anayoweza kuipata mtu anayetumia vifaa hivyo kwa muda mrefu ni maumivu ya
kichwa,kuchoka au kuuma kwa macho, kutokuona vizuri pamoja na maumivu ya shingo
na mgongo.
Amesema kama ilivyo
kawaida ya kupumzisha viungo vingine vya mwili macho pia yana takiwa kupumzika
kutokana na kuwa na umuhimu mkubwa kwa binadamu.
Na
Phinna Nimrod DODOMA FM
This is exactly what I was looking for. Thanks for sharing this great article! That is very interesting Smile I love reading and I am always searching for informative. you can cheak this W3fmradio
ReplyDeleteLatest platform for web marketing and search engine marketing (SEM) and (SEO) tool. This tool provides a complete SEO skill. The mostly person uses search engine marketing for online marketing. this totally depends on latest trends in search engine marketing.
ReplyDelete