Ametoa wito juu ya Maafisa Elimu wa mikoa na Maafisa Elimu wilaya kuwakumbusha walimu kote nchini kuzingatia muongozo wa utoaji wa adhabu shuleni chini ya kifungu namba 61 cha sheria ya elimu sura ya 353 ya sheria pamoja na kanuni zake.
Na Martha Mgaya
Serikali imetoa wito huu kufuatia kusambaa kwa video fupi katika mitandao ya kijamii iliyomuonesha mwalimu wa shule ya msingi Kakanja iliyopo Wilaya ya Kyerwa, Mkoa wa Kagera akimpiga vikali mwanafunzi wa shule hiyo.
Akizungumzia juu ya tukio hilo, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alieleza kuwa vitendo kama hivyo, vimesababisha madhara mengi ikiwemo kuleta taharuki kwa jamii ,athari ya kimwili ,kiakili na msongo wa
“Serikali haitofumbia macho na wala kukubaliana na aina hiyo ya adhabu kali. Tayari serikali imechukua hatua za kinidhamu kwa wahusika.’’ anaeleza Waziri Mkuu Kassim Majaliwa.
Anasema serikali imekuwa ikitekeleza afua mbalimbali kuhakikisha ulinzi na usalama wa mtoto awapo kwenye mazingira yote.Licha ya kuwepo kwa mifumo hiyo kuna ukiukwaji wa sheria na taribu kwa makusudi , hivyo kusababisha madhara makubwa kwa jamii .
Pia, Waziri Majaliwa amezitaka Mamlaka za elimu nchini kuhakikisha kuwa utoaji wa adhabu shuleni unazingatia waraka namba 24 wa mwaka 2002 wa Wizara ya Elimu na Utamaduni ambao umeainisha utaratibu wa utoaji wa adhabu.
“Mwanafunzi wa kike atapewa adhabu ya viboko mkononi na mwalimu wa kike isipokuwa kama shule hiyo haina mwalimu wa kike”
“Adhabu ya viboko itakapotolewa iorodheshwe katika kitabu kilicho tengwa kwa kusudi hili ikiwa ni pamoja jina la mwanafunzi aliyepewa adhabu ,kosa alilotenda,idadi ya viboko na jina la mwalimu aliyetoa adhabu hiyo.’’ anafanua Majaliwa wakati akielezea taratibu zinazo paswa kuzingatiwa wakati wa utoaji adhabu.
Hatua zingine zilizotajwa katika muongozo ni pamoja na Mwalimu mkuu kusaini katika kitabu kila mara adhabu hiyo inapotolewa na endapo mwanafunzi akikataa adhabu ya viboko atasimamishwa shule.
Sambamba na hilo Waziri Majaliwa ameeleza kuwa walimu wamekuwa wakifanya kazi kubwa kuliko mapungufu machache yanayoonekana kupitia mitandao ya kijamii. Hivyo kuitaka jamii kutoyarusha matukio yanayo fanywa na baadhi ya walimu kwenye mitandao.
“Bahati mbaya kwa jamii zetu jambo baya linasambaa zaidi kuliko jema.’’ anasema Majaliwa, “hata hivyo , licha ya mapungufu kutoka kwa baadhi ya walimu, walimu wanafanya mambo mengi makubwa malezi kwa watoto wetu ambayo pengine hayakusambaa na kuonekana. Jamii haipaswi kubeza juhudi zinazo fanywa na walimu badala yake muwatie moyo.’’
Majaliwa amesisitiza lengo siyo kuficha taarifa bali kuzuia taharuki,chuki na uhasama ndani ya jamii, katika nyanja zote kama afya ,vyombo vya ulinzi na usalama na maeneo mengine yanayofanana na hayo.
Comments
Post a Comment