MKUU WA MKOA MH.ROSEMARY SENYAMULE. Na Shadaiya S Hassan ELIMU YA MSINGI Katika mkoa wa DODOMA bajeti ya fedha za mpango wa elimu bila malipo kwa shule za msingi imeongezeka kutoka sh.4,466,566,533.72 mwaka 2022/2021 hadi sh.6,903,484,140.63 mwaka 2022/2023 sawa na ongezeko la asilimia 54.56 Shule za msingi za serikali zimeongezeka Kutoka shule 736 mwaka 2022/2021 hadi shule 784 mwaka 2022/2023 sawa na ongezeko la asilimia 6.52 Zimeanzishwa shule mbili za msingi zinazofundisha kwa kutumia lugha ya kingereza yaani ENGLISH MEDIUM katika halmashauri ya Bahi na Dodoma jiji. Vyumba vya madarasa kwa shule za msingi kutoka 5812 mwaka 2020/2021 hadi 6205 mwaka 2022/2023 hili ni ongezeko la vyumba 393, madarasa haya yamejengwa kupitia mradi wa waTCRP ,mradi wa LANES ,kupitia serikali kuu na mapato ya ndani ya halmashauri 💪💪. ELIMU YA SEKONDARI Fedha za mpango wa elimu ya sekondari bila malipo imeongezeka kutoka sh.4,585,462,268.12 mwaka 2020/202
MH.DKT SAMIA SULUHU. "Nimesikitishwa na vifo vya watu 17 vilivyotokea jana saa 4:30 usiku eneo la Magila Gereza, wilaya ya Korogwe , Mkoa wa Tanga .Nawapa pole wafiwa na wote walioguswa na vifo hivi.Nawaombea ndugu zetu hawawapunzike mahala pema na majeruhi wapone haraka."Ameyasema hayo MH.DKT Samia Suluhu. Katika taarifa iliyotolewa na Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Omary Mgumba leo imeeleza kuwa ajali hiyo imehusisha magari mawili na kusababisha vifo vya watu 17 na Majeruhi 12. Ambao majina yao wote hayajafahamika, miili ya marehemu imehifadhiwa katika Hospitali yetu ya Wilaya ya Korogwe na majeruhi 10 wamehamishiwa Hospitali ya Mkoa wa Tanga, Bombo na majeruhi wawili wamebaki Hospitali ya Korogwe kwa matibabu. “Ajali hii imehusisha gari aina ya Mitsubishi Fuso na Coaster iliyokuwa imebeba mwili wa marehemu na abiria 26 ikitokea Dar kwenda Moshi kwenye mazishi” imeeleza taarifa hiyo. Na Martha Mgaya.