![Image result for KUPIMA MAKAZI JIJIJINI DODOMA](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgFiuDjle3HOYmeagb32Qr-ZgI7OfjWxjTm0HamCQPXHIQ2WBNisEz39qgz31qJVX62nGhKDZmWg4flyLvGsncUc-8UnkcOHWUf1WcZT4cPjsMNJUrtB4rnD9f508r8ZHrHIksk_W1VGXQ/s640/Dodoma-One.jpg)
Mamlaka zinazohusika na
zoezi la upimaji wa makazi katika jiji la Dodoma zimeombwa kuendelea
kupima viwanja vya wananchi katika maeneo mbalimbali ya jiji ikiwemo kata ya
Mkonze ili kuepusha ujenzi holela.
Wito huo umetolewa leo na
mwenyekiti wa mipango miji na mazingira kutoka jiji la Dodoma ambaye pia ni
diwani wa kata ya Mkonze BW, David
Bochela wakati akizungumza na DODOMA FM na kusema kuwa suala la kupima linapaswa
kuzingatiwa ili kuendana na hadhi ya jiji.
Amesema kuwa nia ya wananchi
ni kujenga ili waishi katika makazi bora hivyo viongozi mbalimbali ikwemo wa
serikali za mitaa wana wajibu wa kusimamia jambo hilo kwani jamii bado
inahitaji kupewa elimu ili kutokomeza suala la ujenzi holela ambalo limekuwa
likikwamisha shughuli za maendeleo.
Hata hivyo amewataka
wananchi kuunga mkono jitihada za viongozi pamoja na kuyapokea makampuni
yanayohusika na suala la upimaji wa makazi pindi yanapofika katika maeneo yao
ili kufanikiwa jambo hilo kwa wakati.
Kwa upande wao baadhi ya
wananchi jijini Dodoma wamesema kuwa ujenzi holela umekuwa ukichangiwa na
gharama za upimaji kuwa juu ukilinganisha na vipato vyao hivyo ni vyema
serikali ikatazama jambo hilo ili kufanikisha zoezi hilo.
NA ALFRED BULAHYA DODOMA FM
Comments
Post a Comment