Uongezewaji wa
dripu za uchungu kwa kinamama wajawazito imetajwa kuwa ni chanzo cha kupelekea kinamama kujifungua kwa
njia ya upasuaji.
Akizungumza na
Dodoma FM mtaalamu wa upasuaji kutoka katika hospitali ya Rufaa jijini hapa
Doctor CHETO HAULO ameitaja sababu hiyo kama njia pekee inayosababisha mjamzito
kupasuliwa kutokana na mama huyo kuongezewa uchungu kabla mtoto hajajiandaa
kutoka.
Amesema kuongezeka
au kushuka kwa mapigo ya moyo ya mtoto hii pia ni miongoni mwa sababu
inayopelekea mama kutojifungua kwa njia ya kawaida hivyo kumpelekea mama huyo
kupasuliwa ili kuokoa maisha ya mtoto.
Aidha amewashauri
kinamama ambao wanaomba kujifungua kwa njia ya
upasuaji kutokana na kuogopa
uchungu wa kujifungua kwa kawaida kuachana na hiyo tabia na badala yake
wajifungue kwa njia salama kutokana na athari zitokanazo na upasuaji.
Dokta Cheto
amebainisha madhara yatokanayo na upasuaji kuwa miongoni mwa madhara hayo ni
baadhi yao kutopona vizuri sehemu iliyopasuliwa pamoja na kupata magonjwa kupitia kidonda hicho .
Kutokana na madhara
hayo mgonjwa anashauriwa kutokubeba ujauzito kwa kipindi cha miaka mitatu ili
kuupa nafasi mwili kurudi katika hali yake ya kawaida.
Na
ANIFA RAMADHAN DODOMA FM
Comments
Post a Comment