![Image result for hospitali ya Benjamin Mkapa](https://farm1.staticflickr.com/808/27200162148_93867e9a1e_b.jpg)
Serikali imesema
inatambua changamoto ya upungufu wa madaktari bingwa katika hospitali ya
Benjamin Mkapa iliyopo Mkoani Dodoma huku mikakati mbalibali ikifanyika ili
kutatua changamoto hiyo.
Naibu Waziri wa
afya maendeleo ya jamii jinsia wazee na watoto Dokta Faustine Ndugulile
ameyasema hayo leo Bungeni Mjini Dodoma wakati akijibu swali la Mbunge Rukia
Ahamed aliehoji Serikali ina mpango gani katika kutatua changamoto ya upungufu
wa madaktari bingwa katika Hospitali ya Benjamin Mkapa.
Dokta Ndugulile amesema
Serikali imeweka mikakati ya kuondoa changamoto hiyo katika hospitali ya Benjamin
Mkapa pamoja na hospital nyingine za rufaa za Mikoa zilizo na upungufu wa
madaktari pamoja na kufadhili masomo ya madaktari bingwa wapatao 125.
Kwa upande wake Naibu Waziri wa TAMISEM Mh.
Josephat Kandege amesema nia ya Serikali ni kuhakikisha kuwa vituo vya afya na
zahanati zinatoa huduma stahiki kwa wananchi na kusisitiza kuwa popote
itakapobainika kituo cha afya kufungwa kwa kukosa watumishi wa afya ni vema
taarifa zikatolewa mapema ili kufanyia kazi changamoto hiyo.
Mh. Kandege amesema
baadhi ya maeneo yatakayopatiwa kipaumbele cha kujengewa vituo vya afya ili
kuepusha msongamano katika hospitali za Wilaya ni pamoja na mkoa wa Kigoma
ikiwa ni mkakati unaotegemea bajeti pamoja na kibali cha ajira kwa waganga
wapatao 1667.
Na
Pius Jayunga Chanzo: Dodoma Fm
Comments
Post a Comment