Kampeni ya "MAGAUNI MANNE" yenye lengo la kupunguza mimba za
utotoni kwa wanafunzi wa shule za msingi na sekondari mjini Dodoma inatarajiwa
kuziduliwa kesho kwa awamu ya pili.
Taasisi ya vijana mkoani Dodoma (Doyodo)imesema imedhamiria
kusaidia kupunguza mimba za utotoni kwa mkoa wa Dodoma ambapo kampeni hiyo
itasaidia kutoa elimu kwa watoto wa kike juu ya madhara ya mimba za utotoni.
Charles Ruben ni afisa habari wa taasisi hiyo amesema baada
ya kampeni hiyo kuzinduliwa kwa awamu ya pili hapo kesho waatanza na shule za
msingi tano pamoja na shule za sekondari tano kutoa elimu hiyo.
Amesema wameamua kuwafikia wanafunzi wa shule za msingi
kutokana na kuwa kumekuwa na idadi kubwa ya mimba za utotoni jambo ambalo
linakatisha ndoto za wasichana wengi.
Nae afisa nidhamu wa taasisi hiyo Ambros Kiwale amesema
katika kampeni hiyo wataunda club katika shule mbalimbali lengo likiwa ni
kuwasaidia kufuatilia kwa ukaribu changamoto za watoto wa kike .
Kampeni ya magauni manne iliasisiwa na aliyekuwa mkuu wa
wilaya ya Dodoma Mjini Bi Christina Mdeme ambae kwa sasa ni mkuu wa Mkoa wa
Ruvuma kwa lengo la kuwasaidia watoto wa
kike kutimiza ndoto katika suala la elimu .
Mariam Matundu Chanzo: Dodoma FM
Comments
Post a Comment