Diwani wa kata ya Hombolo bwawani Manispaa
ya Dodoma Bwana Asedi Mathayo amewashukuru wanafunzi wa chuo cha serikali za mitaa Hombolo
kwa kuelimisha wanachi wa eneo hilo juu ya matokeo chanya ya utunzaji wa
mazingira.
Bwana Ased ameyasema hayo wakati
akizungumza na Dodoma FM juu ya siri ya mafanikio ya wakazi wa kata hiyo
kuhamasika kutunza mazingira kwa kiasi kikubwa.
Amewashukuru wanafunzi wa chuo cha
serikali za mitaa Hombolo kuwa mstari wa mbele kuelimisha wananchi hadi
kuwapelekea kuwa na hamasa kubwa ya kutunza mazingira.
Aidha Bwana Ased Mathayo
amewashukuru wananchi ambao walikuwa wanafanya shughuli za kilimo karibu na
Bwawa la Hombolo kwa kutii agizo la serikali lilikuwa likiwataka kuacha mara
moja.
Hata hivyo ameendelea kuwasisitiza
wakazi wa mkoa wa Dodoma na Tanzania kwa ujumla kuepuka ukataji miti kiholela
kwani hupelekea madhara makubwa ikiwemo jangwa.
Na
Benard Filbert Dodoma
FM
Comments
Post a Comment