Halmashauri
ya Manispaa ya Dodoma kupitia Idara ya Mazingira imesema kutokana na kuendelea
kukuwa kwa Mji kumekuwa na changamoto ya uvunaji holela wa madini ujenzi katika
maeneo mbalimbali ya Mji wa Dodoma.
Akiongea
na Dodoma Fm Afisa mazingira Idara ya mazingira na udhibiti wa taka ngumu wa
Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma Bw. ALLY MFINANGA amesema kazi moja wapo ya
Idara ya mazingira ni kudhibiti uchimbaji holela wa mchanga, Kokoto pamoja na
kifusi lakini kutokana na mji kukua kumekuwa na changamoto ya watu kufanya
shughuli hizo bila kufuata tarabitu.
Amesema
zipo taratibu zinazopaswa kufuatwa na mtu anayehitaji kufanya shuguli ya madini
ujenzi na kwamba anatakiwa kufika katika uongozi wa eneo husika pamoja na
kuwasiliana na afisa madini mkazi kwa ajili ya kupata kibali.
Sambamba
na hayo amesema kwa atakayekwenda kinyume na taratibu za uvunaji wa madini
ujenzi na kufanya shughuli hizo katika miundombinu ya maji, mashamba pamoja na
miundombinu ya umeme hatua stahiki zitachukuliwa dhidi yao ikiwa ni pamoja
na kupigwa faini.
Na Phina Nimrod Chanzo:Dodoma FM
Comments
Post a Comment