Jeshi
la polisi Mkoa wa Dodoma linawashikilia watu 14 kwa makosa mbalimbali wakiwemo
wanne kati yao kwa kujifanya maafisa wa jeshi la wananchi wa Tanzania JWTZ na
usalama wa Taifa huku wakitumia nyadhifa hizo kujipatia mali kwa njia za
udanganyifu.
Kamanda wa Jeshi la
polisi Mkoa wa Dodoma Gilles Muroto akizungumza na waandishi wa habari ofisini
kwake amewataja waliokamatwa katika tukio hilo kuwa ni Shaban Ramadhan Kwiyela
(58) mkazi wa Igunga Tabora, Emmanuel Kasunga ( 45) mkazi wa Mtera Iringa, Juma
Almasi Pembambili (33) mkazi wa Sai jijini Mbeya pamoja na Emmanuel Hassan
Mwangolela (50) mkazi wa mtaa wa Ghana jijini Mbeya.
Katika tukio la
pili wamekamatwa watu wawili kwa kujihusisha na wizi wa pikipiki huku wakitumia
mbinu ya kuiba pikipiki kutoka Dodoma na kwenda kuziuza Kiteto Manyara na nyingine
wakiiba kutoka Kiteto na kuzileta kuziuza hapa Mkoani Dodoma.
Kamanda Muroto
amesema tukio la tatu wamemkamata kijana Abdalah Hamza Salum (20) dreva wa
bodaboda mkazi wa Area A Dodoma kwa kosa la unyang’anyi ambapo hutumia pikipiki
yake yenye namba za usajiliu MC. 366 BJR aina ya boxer kukwapua mikoba ya
wapita njia na akipakia abiria huwapeleka katika maficho na kuwatishia sime
kisha kuwapora vitu mbalimbali zikiwemo simu za mkononi, mikufu na vito vya
thamani.
Katika tukio la
mwisho kamanda Muroto amesema wanawashikilia watu 6 akiwemo raia wa china kwa
kosa la kuchezesha mchezo wa kamari bila kibali maalumu katika mkoa wa Dodoma
na hivyo kuikosesha serikali mapato na katika matukio yote kamanda Muroto
amesema mkoa wa Dodoma utaendelea kukabiliana na kila aina ya uhalifu
utakaojitokeza katika mkoa wa dodoma.
NA
PIUS JAYUNGA
DODOMA FM
Comments
Post a Comment