Katika kuelekea kilele cha
maadhimisho ya wiki ya maji jamii mkoani Dodoma imetakiwa kuwa karibu,kujiunga
na kutumia mfumo wa mtandao wa maji safi na maji taka.
Mkuu wa kitengo cha uhusiano na
mawasiliano mamlaka ya Maji na usafi wa
mazingira Dodoma DUWASA Bwana Sebastian Warioba amesema wanatumia maadhimisho
haya katika kuelimisha jamii kujiunga na mfumo wa maji safi na maji taka katika
kila nyumba.
Amesema mamlaka ya maji na usafi wa
mazingira mjini Dodoma tangu kuanza kwa mwaka huu 2018 wananchi wameanza
kutumia mfumo wa malipo wa kielekroniki ambapo wanaweza kulipa bili kwa kutumia
mitandao ya simu.
Sambamba na hayo amewataka wananchi
kutokusita kutoa taarifa pindi wanapoona vitendo vinavyoathiri miundombinu ya
maji na kwamba kila mtoa taarifa moja sahihi atapewa zawadi ya sh laki moja.
wiki ya maji imeanza tangu tarehe 16
mwezi huu na itafikia kilele kesho tarehe 22 march 2018 ikiwa na kaulimbiu
hifadhi maji na mfumo wa kiikolojia kwa maendeleo ya jamii.
Mariam Matundu Dodoma
FM
Comments
Post a Comment