Skip to main content

WATU 10 WAFARIKI KUFUATIA AJALI YA BASI LA ABIRIA NA TRENI YA MIZIGO KIGOMA



Image result for AJALI BASI NA TRENI KIGOMA









Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli ametuma salamu za rambirambi kwa familia, ndugu, jamaa na marafiki kufuatia vifo vya watu 10 vilivyosababishwa na ajali ya basi la abiria kugongana na treni ya mizigo Mjini Kigoma.

Ajali hiyo imetokea leo tarehe 06 Juni, 2018 majira ya saa 12:15 asubuhi katika eneo la Gungu Mjini Kigoma wakati basi la abiria la kampuni ya Prince Hamida lililokuwa linatoka Kigoma Mjini kwenda Tabora lilipoigonga treni ya mizigo iliyokuwa ikitoka Kazuramimba kwenda Kigoma Mjini.

Mhe. Rais Magufuli amemtaka Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Brig. Jen. Mstaafu Emanuel Maganga kufikisha salamu hizo kwa wafiwa wote, na amewaombea kuwa na moyo wa subira, uvumilivu na ustahimilivu katika kipindi hiki kigumu cha majonzi ya kuondokewa na wapendwa wao.

Mapema asubuhi leo kamanda wa Polisi mkoani Kigoma Martin Otieno amethibitisha kutokea kwa ajili hiyo ambayo Watu 10 wamefariki papo hapo na wengine 27 kujeruhiwa.

Kamanda wa polisi amesema, basi hilo lilitupwa mita 100 kutoka kwenye eneo la ajali na kueleza kuwa waokoaji wamewatoa watu walionaswa kwenye mabaki ya basi hilo, na huenda idadi ya watu waliofariki ikaongezeka.

Na Zania Miraji                           Chanzo:Ikulu /DODOMA FM

Comments