Skip to main content

DODOMA YAANZISHA MAONYESHO YA KAMPUNI ZA VIFAA VYA UJENZI

     Image result for mkurugenzi mtendaji jiji la dodoma


Kampuni zinazotengeneza vifaa vya ujenzi Dodoma zimeshauriwa kutumia fursa ya kufanya biashara katika kipindi hiki ambacho serikali inahamia Dodoma.

Ushauri huo umetolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa Jiji la Dodoma, Godwin Kunambi wakati akizungumzia juu ya maandalizi ya maonyesho kwa kampuni zinazotengeneza vifaa vya ujenzi na samani za ndani pamoja na wadau wa sekta ya ujenzi.

Akizungumza na waandishi wa habari Kunambi amezitaka kampuni hizo kutumia fursa ya ujio wa makao makuu kwa kujitambua, ili mashirika, taasisi na watu binafsi wanaojenga Dodoma wafahamu ni bidhaa gani bora kwa ajili ya ujenzi.

Maonyesho hayo yanafahamika kama Dodoma Builders Expo 2018, na amesisitiza kwamba fursa hiyo ni kubwa na wafanyabiashara wa vifaa vya ujenzi waitumie kuonyesha bidhaa bora.

Kunambi amesema ni kosa kulifananisha jiji la Dodoma na mikoa mingine nchini kwani linatakiwa kufananishwa na Jiji la Nairobi Kenya na Pretoria Afrika ya Kusini.

Kwa upande wake mratibu wa maonyesho hayo, Victor Simon amewataka makandarasi wa jiji hili kuwatumia mafundi na vibarua wa Dodoma, na kuacha tabia ya kutumia wale wa kutoka maeneo mengine. 

Na Benard Filbert                                                  DODOMA FM



Comments