Skip to main content

WAZIRI MBARAWA ASEMA SERIKALI HAITAMVUMILIA MTUMISHI ATAKAYEKWAMISHA BAJETI

                                   Image result for WAZIRI MBARAWA


Waziri wa ujenzi uchukuzi na mawasiliano prof Makame Mbarawa amesema serikali haitasita kumchukulia hatua mtumishi yeyote atakayeonekana kuwa chanzo cha kukwamisha malengo ya bajeti wakati wa kufanya mapitio ya bajeti ya nusu mwaka hapo baadae.

kauli hiyo imetolewa leo na Eng. Joseph Nyamhanga alipokuwa akitoa hotuba kwa niaba ya Waziri wa ujenzi uchukuzi na mawasiliano prof Makame Mbarawa wakati wa kufungua mkutano wa baraza la wafanyakazi wa sekta ya uchukuzi mjini Dodoma.

Amesema kuwa serikali itakapokuwa ikifanya mapitio ya bajeti ya nusu mwaka hapo baadae na kugundua uwepo ukiukwaji wa taratibu zilizowekwa haitosita kumwajibisha mtumishi yeyote atakayeonekana kutotimiza malengo ya bajeti hiyo hivyo ni vyema watumishi wakazingatia maelekezo ili kila mmoja atekeleze majukumu yake ipasavyo.

Hata hivyo ameitaka menejimenti ya wizara na chama cha wafanyakazi TUGHE kuhakikisha kuwa zinafanya kazi kwa mshikamano thabiti katika kufikia maamuzi mbalimbali ya kisera na kitaaluma ambayo yatafanikisha shughuli za sekta ya uchukuzi na tabiri za hali ya hewa kufikia malengo yao.

Awali akisoma taarifa ya baraza la wafanyakazi wa sekta ya uchukuzi mwenyekiti wa baraza la wafanyakazi la wizara ya uchukuzi dkt Leonard Chamriho amesema kuwa sekta ya uchukuzi kwa mwaka mpya wa fedha unaokuja 2017/18 imejiwekea malengo ya kuboresha miundombinu ya hali ya hewa, ununuzi wa ndege mpya 4 kwa ajili ya kuboresha huduma za ATCL pamoja na kutekeleza awamu ya pili na ya tatu ya serikali kuhamia Dodoma.

Na Alfred Bulahya                                                         DODOMA FM

Comments