Skip to main content

SABABU ZINAZOPELEKEA SHULE YA MSINGI KIZOTA KUTOKUWA NA UFAULU MZURI

Imeelezwa kuwa uhaba wa madarasa shuleni wanafunzi kutofika shule kwa wakati kutohudhuria darasani wakati wa vipindi na utoro, ni changamoto zinazosababisha ufaulu mdogo na hivyo kushuka kitaaluma kwa mwanafunzi.


Hayo yamebainishwa na mwalimu mkuu msaidizi wa shule ya msingi Kizota iliyopo manispaa ya Dodoma Bi Olimpia Mpunga  wakati akizungumza na Dodoma FM juu ya sababu za shule hiyo kushuka kitaaluma.

Mwl Olimpia amesema upungufu wa vyumba ya madarasa unawafanya wanafunzi  kusoma kwa awamu ili kupeana nafasi,  jambo ambalo ni changamoto kubwa.

Mwalimu Olimpia  amebainisha kuwa sababu zinazosababisha kuwepo kwa utoro kwa wanafunzi shuleni hapo ni pamoja na  wanafunzi  kuwa na makundi mitaani  na wengine kuwa na visingizio vya kuwa na matatizo .

Aidha amesema tayari wanao mpango mkakati wa kudhibiti utoro huo kwa kushirikiana na shirika la WWU ambao linashirikisha wazazi na walimu na kuwa kazi ya wazazi ni kujadili mbinu za kutumia katika kudhibiti utoro na mbinu za kuleta maendeleo katika taaluma.

Kwa upande wao wanafunzi wamewaasa wanafunzi wenzao ambao wamekuwa na tabia ya utoro kwenye vipindi na wengine kutohudhuria shuleni kuwa ni vyema wakajijengea mazoea ya kwenda  shule kwani wasipohudhuria vipindi darasani hukosa uelewa wa baadhi ya masomo na hivyo kufeli katika mitihani yao ya mwisho

Rweikiza katebalirwe                                                         Dodomafm

Comments