Skip to main content

HABARI KUU NDANI YA KIPINDI CHA TASWIRA YA HABARI

Mauaji ya mwanafunzi Tanzania: Polisi wawahoji maafisa wakuu wa Chadema

                     Marehemu Akwilina Akwiline

Maafisa wa polisi mjini Dar es Salaam wamewataka viongozi wakuu wa chama cha upinzani nchini humo Chadema kufika mbele yake ili kuhojiwa kutokana na kifo cha mwanafunzi wa chuo kikuu cha usafirishaji nchini humo Akwilina Akwiline.

Bi Akwiline alifariki baada ya kupigwa risasi kimakosa wakati wa maandamano ya viongozi wa chama hicho yaliotibuliwa na maafisa wa polisi siku ya Ijumaa.

Mauaji hayo kwa sasa ndio swala linalozungumziwa sana nchini Tanzania huku raia kupitia mitandao tofauti ya kijamii wakishutumu kisa hicho.

Chanzo Bbc Swahili



 


Jamii imeombwa kusaidia makundi yenye uhitaji mbalimbali katika jamii zao ikiwemo watoto wanoishi katika mazingira magumu na hatarishi. 

Mbunge wa viti maalumu mkoa wa Dodoma Fatma Toffic ameyasema hayo katika halfa ya kukabidhi kadi za bima ya afya kwa watoto wanaoishi katika mazingira hatarishi waliopo katika kituo cha safina street network zilizotolewa na taasisi ya Miriam supporting society .

Aidha amesema jamii inapaswa kujitoa katika kusaidia watoto wanaishi katika mazingira hatarishi huku akiwataka wazazi kuepuka mifarakano ambayo ndio imekuwa chanzo cha kuwa na watoto wengi wa mitaani.

Awali mkurugenzi wa taasisi ya Miriam supporting society Miriam Nteko amesema watoto wanaoishi katika mazingira magumu wamekuwa wakipata changamoto kupata matibabu kutokana na kukosa bima za afya na hivyo kuwaomba wadau wa maendeleo kuunga mkono suala hilo kwa kuendelea kuwakatia bima watoto hao.

Baadhi ya watoto waliopata bima hizo katika kituo cha safina street network akiwemo Amani Abdala ameshukuru kwa kupata bima hiyo na kusema itamsaidia pale atakapo pata matatizo ya kiafya

Jumla ya watoto 142 wamekatika bima za afya za CHF na taasisi ya Miriam supporting society kwa kushirikia na watu waliguswa kuwasaidia watoto hao.


Wananchi mkoani Dodoma wametakiwa kutoa taarifa dawati la jinsia juu ya vitendo vya kikatili vinavyoendelea kufanyika mkoani hapa ili kusaidiwa kutatuliwa matatizo yanayowakumba.

Akizungumza na kituo hiki mkaguzi msaidizi wa polisi dawati la jinsia na watoto Bi.Teresia Mdendemi amesema kwa kipindi kilichopita hakukuwa na kesi nyingi ambazo zilikuwa zinawafikia tofauti na kipindi hiki ambapo elimu imekuwa ikitolewa kwa jamii.

Bi. Mdendemi ametaja baadhi ya matukio ya kikatili ambayo yanaongoza kufanywa mkoani Dodoma kuwa ni  pamoja na ubakaji,kulawiti, utelekezaji wa familia pamoja na ndoa za utotoni.

Kutokana na Elimu inayoendelea kutolewa dhidi ya upigaji vita matukio ya ukatili wa kijinsi wananchi mkoani Dodoma wametakiwa kuendelea kutoa ushirikiano dawati la jinsia kwa kufikisha malalamiko yao ili kubaini mwitikio wa

HALMASHAURI YA MANISPAA YA DODOMA KUAJIRI ASKARI MIGAMBO 30.




Na Dodoma fm

Kamati ya fedha na mipango katika Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma kwa kauli moja imekubaliana kuajiri askari migambo wapatao 30 watakao gawanywa katika tarafa 4 za Manispaa ya Dodoma ili kudhibiti ujenzi holela.

Mkurugenzi wa Manispaa ya Dodoma Bw. Godwin Kunambi amewaambia waandishi wa habari kuwa lengo la kuajiri migambo hao ni kuhakikisha wanadhibiti ujenzi holela ambao umekuwa ukiendelea katika mji wa Dodoma ambao ndio kitovu cha Nchi.

Miongoni mwa mambo mengine ambayo uongozi wa Manispaa ya Dodoma unaendelea kuyafanyia kazi ni pamoja na kukamilisha ujenzi wa soko katika eneo la Makole litakalotumika kwa shughuli zote za wamachinga ili kupunguza kero pamoja na msongamano wa wafanyabiashara hao katika eneo moja.

Hata hivyo licha ya kuwahamishia wamachinga wote katika soko la Makole Mkurugenzi wa Manispaa ya Dodoma  amesema ulinzi mkali utaimarishwa katika maeneo ya barabara ili kudhibiti uzalishaji wa wamachinga wengine ndani ya mji wa Dodoma.

Baadhi ya wafanyabiashara maarufu kama wamachinga katika manispaa ya Dodoma licha ya kupongeza jitihada hizo wamesema hatua hiyo itawarudisha nyuma kiuchumi kutokana na wao kufanya biashara kwa kufuata maeneo yaliyo na mkuanyiko mkubwa wa watu.
               
VYOMBO VYA DOLA VYATAKIWA  KUTUMIA BUSARA KATIKA UTATUZI WA MIGOGORO.



Na Dodoma fm

Vyombo vya Dola vimetakiwa kuwa kipaumbele kwa kutumia nafasi zao katika kudumisha amani ya nchi hasa katika maandamano na migomo inayotokea ili kuepusha nchi kuingia katika machafuko yanayoweza kujitokeza.

Hayo yameelezwa na Mchambuzi wa maswala ya kisiasa Bw. Denis Nachipyangu wakati akizungumza na Taswira ya habari ambapo amesema kuwa mara nyingi machafuko yanatokea iwapo vyombo vya dola vikitumia nguvu katika kutatua migogoro au maandamano hivyo ni vyema vikatumia akili na busara ili kuepuka kutokea kwa machafuko ya nchi.

Bw. Nachipyangu amesema kuwa maandamano mengi yamekuwa yakipelekea machafuko kutokana na kuwa baadhi ya watu wamekuwa na mawazo tofauti juu ya matokeo ya maandamano hayo ambapo wengi wao wamekuwa wakihofia kutokea kwa vurugu na machafuko.

Sanjari na hayo Bw. Nachipyangu ametoa rai kwa  Wananchi pamoja na vyombo vya dola kutokukiuka haki za kikatiba katika kufuata taratibu na sheria za nchi badala yake vinatakiwa kutoa ulinzi kwa Wananchi ili waweze kuendelea kuwa na imani na vyombo hivyo.



  JAMII IMETAKIWA KUTUMIA VYOO VYA KISASA
                    
                             
Na Dodoma fm 

Wakazi wa maeneo ya vijijini mkoani Dodoma wameshauriwa kuacha kuendelea kutumia vyoo vya zamani na badala yake wajenge vyoo vya kisasa vinavyosafishika kwa urahisi ikiwa ni njia mojawapo ya kujikinga na magonjwa ya kuambukiza.



Ushauri huo umetolewa na afisa afya wa manispaa ya Dodoma Bwana Alek Saimon wakati akizungumza na kituo hiki ambapo amesema katika maeneo ya vijijini bado wanajamii hawana elimu ya kutosha juu ya ujenzi wa vyoo bora vya kisasa ambavyo ni rahisi  kuvisafisha.


Bwana Alek amesema katika kuhakikisha afya katika jamii inaendelea kuimarika manispaa ya Dodoma wanashirikiana na  wadau mbalimbali katika ujenzi wa vyoo bora na vya kisasa kwa gharama nafuu pamoja na utoaji wa elimu zitokanazo na matumizi ya vyoo hivyo.

Hata hivyo amesema maeneo mengi vijijini wanashirikiana na ngazi  ya kata ambao ni maafisa afya wa kata wanao pita kila nyumba kuhamasisha wananchi juu ya ujenzi wa  vyoo bora na vya kisasa.
 

Comments

Popular posts from this blog

MITI YA KIVULI MAARUFU KAMA PANGA UZAZI YAZUA TAHARUKI WILAYANI BAHI DODOMA

                                                  Mganga Mkuu wa Wilaya ya Bahi Jijini Dodoma Dk.Philipina Philipo amewatoa hofu wakazi   wa Wilaya hiyo juu ya taarifa za kuwepo kwa madhara katika miti ya kivuli maarufu kama PANGA UZAZI ambayo imezua hofu kwa wananchi hao. Hoja hiyo imeibuliwa katika kikao cha Baraza la Madiwani wa halmashauri hiyo ambapo baadhi ya madiwani wameomba kupatiwa ufafanuzi kuhusu kuwepo kwa fununu kuwa mti huo una madhara na kuongeza kuwa baadhi ya wananchi wameanza kuikata wakihofia kupatwa na madhara hayo. Akitoa ufafanuzi kuhusu miti hiyo Mganga Mkuu wa Wilaya Dk.Philipina Philipo amesema hadi hivi sasa hakuna utafiti wowote uliofanyika na kubainisha kuwa mti huo hauna madhara hivyo wananchi hawana haja ya kuhofia chochote. Kutokana na Majibu hayo ya DK PHILIPINA yamepelekea kuibua kwa hoja nyingine kwa madiwani ambapo baadhi yao wametoa maoni tofauti tofauti juu ya ufafanuzi huo. Kufuatia hayo katibu  tawala msaidizi mkoa anayesh

YANGA KESHO KUJUA ANACHEZA NA NANI KOMBE LA SHIRIKISHO AFRIKA

MAJINA ya vigogo wa soka Afrika, wakiwemo mabingwa wa Afrika 1998, Raja Casablanca yametawala katika orodha ya wapinzani wapya wa Yanga kwenye michuano ya Afrika. Yanga SC imeangukia kwenye kapu la kuwania kucheza hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika, ambako watamenyana na moja ya timu zilizofuzu hatua ya 16 Bora ya michuano hiyo. Hiyo ni baada ya kutolewa kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya sare ya 0-0 na wenyeji, Township Rollers Jumamosi jioni Uwanja wa Taifa mjini Gaborone nchini Botswana. Matokeo hayo yanamaanisha Rollers inakwenda hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa kwa mara ya kwanza historia hiyo kwa ushindi wa jumla wa 2-1 uliotokana na matokeo ya mchezo wa                              kwanza Dar es Salaam Machi 6. Na Yanga SC itamenyana na moja ya timu zilizofuzu hatua ya 16 Bora ya michuano hiyo, ambazo ni CR Belouizdad, USM Alger za Algeria, Al-Masry ya Misri, Djoliba ya Mali, Raja Casablanca, Enyimba ya Nigeria, SuperSport United ya Afrika K

MIKOA INAYOONGOZA KWA UKEKETAJI TANZANIA YATAJWA

Mila potofu   katika jamii ya kimasai imetajwa kuwa changamoto kwa maafisa ustawi wa jamii wa halimashauri ya wilaya ya Ngorongoro  kutokana na kukosa ushirikiano wa kutatua Tatizo la ukeketaji kwa jamii hiyo. Akizungumza na waandishi ya habari Afisa Ustawi Wa jamii Bwana ALOYCE  LOLIKISWALI katika semina iliyoandaliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu Sanyansi na Utamaduni UNESCO kwa lengo la kupinga ukeketaji wa wanawake amesema kukosekana kwa ushirikiano kwa jamii imekuwa ni changamoto ambayo imepelekea kushindwa kudhibiti ukeketaji pamoja na ukatili wa kijinsia. Kwa upande wake Mwenyekiti wa Malaigwanan Bwana JOSEPH TIRIPAI amebainisha kuwa mila na desturi zao zitabadilika kulingana na wakati lakini watahakikisha wanalinda watoto wanaozaliwa kutokeketwa na kusisitiza elimu kuendelea kutolewa hususani shuleni. Katika hatua nyingine mratibu wa afya ya mama na mtoto ameeleza kuwa wanawake wajawazito waliokeketwa wanalazimika   kujifugua kwa upasuaji na