Wananchi mkoani Dodoma wametakiwa kutoa taarifa dawati la jinsia juu ya vitendo vya kikatili vinavyoendelea kufanyika mkoani hapa ili kusaidiwa kutatuliwa matatizo yanayowakumba.
Akizungumza na kituo hiki mkaguzi msaidizi wa polisi dawati la jinsia na watoto Bi.Teresia Mdendemi amesema kwa kipindi kilichopita hakukuwa na kesi nyingi ambazo zilikuwa zinawafikia tofauti na kipindi hiki ambapo elimu imekuwa ikitolewa kwa jamii.
Bi. Mdendemi ametaja baadhi ya matukio ya kikatili ambayo yanaongoza kufanywa mkoani Dodoma kuwa ni pamoja na ubakaji,kulawiti, utelekezaji wa familia pamoja na ndoa za utotoni.
Kutokana na Elimu inayoendelea kutolewa dhidi ya upigaji vita matukio ya ukatili wa kijinsi wananchi mkoani Dodoma wametakiwa kuendelea kutoa ushirikiano dawati la jinsia kwa kufikisha malalamiko yao ili kubaini mwitikio wa elimu inayotolewa kwa kila mmoja.
Comments
Post a Comment