Skip to main content

Posts

KISHINDO CHA SERIKALI YA AWAMU YA SITA MKOA WA DODOMA CHINI YA MKUU WA MKOA MH.ROSEMARY SENYAMULE.

                                     MKUU WA MKOA  MH.ROSEMARY SENYAMULE. Na Shadaiya S Hassan   ELIMU YA MSINGI   Katika mkoa wa DODOMA bajeti ya fedha za mpango wa elimu bila malipo kwa shule za msingi imeongezeka kutoka sh.4,466,566,533.72 mwaka 2022/2021 hadi sh.6,903,484,140.63 mwaka 2022/2023 sawa na ongezeko la asilimia 54.56  Shule za msingi za serikali zimeongezeka Kutoka shule 736 mwaka  2022/2021 hadi shule 784 mwaka 2022/2023  sawa na ongezeko la asilimia 6.52  Zimeanzishwa shule mbili za msingi zinazofundisha kwa kutumia lugha ya kingereza yaani ENGLISH MEDIUM katika halmashauri ya Bahi na Dodoma jiji. Vyumba vya madarasa kwa shule za msingi kutoka 5812 mwaka 2020/2021 hadi 6205 mwaka 2022/2023 hili ni ongezeko la vyumba 393, madarasa haya yamejengwa kupitia mradi wa waTCRP ,mradi wa LANES ,kupitia serikali kuu na mapato ya ndani ya halmashauri 💪💪.  ELIMU YA SEKONDARI  Fedha za mpango wa elimu ya sekondari bila malipo imeongezeka kutoka sh.4,585,462,268.12 mwaka 2020/202
Recent posts

RAIS SAMIA ATOA POLE KWA WAFIWA WA AJALI ILIYOTOKEA TANGA NA WATU 17 KUPOTEZA MAISHA

                                                                                  MH.DKT SAMIA SULUHU. "Nimesikitishwa na vifo vya watu 17 vilivyotokea jana saa 4:30 usiku eneo la Magila Gereza, wilaya ya Korogwe , Mkoa wa Tanga .Nawapa pole wafiwa na wote walioguswa na vifo hivi.Nawaombea ndugu zetu hawawapunzike mahala pema na majeruhi wapone haraka."Ameyasema hayo MH.DKT Samia Suluhu. Katika taarifa iliyotolewa na Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Omary Mgumba leo imeeleza kuwa ajali hiyo imehusisha magari mawili na kusababisha vifo vya watu 17 na Majeruhi 12. Ambao majina yao wote hayajafahamika, miili ya marehemu imehifadhiwa katika Hospitali yetu ya Wilaya ya Korogwe na majeruhi 10 wamehamishiwa Hospitali ya Mkoa wa Tanga, Bombo na majeruhi wawili wamebaki Hospitali ya Korogwe kwa matibabu. “Ajali hii imehusisha gari aina ya Mitsubishi Fuso na Coaster iliyokuwa imebeba mwili wa marehemu na abiria 26 ikitokea Dar kwenda Moshi kwenye mazishi” imeeleza taarifa hiyo. Na Martha Mgaya.

HABARI MOTOMOTO KUTOKA KATIKA MAGAZETI YA LEO FEBRUARY 4,2023

 

Serikali Haitafumbia Macho Maswala ya Adhabu Kali Mashuleni

            Waziri Mkuu Kassim Majaliwa katika kipindi cha maswali na majibu Bungeni mjini Dodoma.      Ametoa wito juu ya Maafisa Elimu wa mikoa na Maafisa  Elimu wilaya kuwakumbusha walimu kote nchini kuzingatia muongozo wa utoaji wa adhabu shuleni chini ya kifungu namba 61 cha sheria ya elimu sura ya 353 ya sheria pamoja na kanuni zake. Na Martha Mgaya Serikali imetoa wito huu kufuatia kusambaa kwa video fupi katika mitandao ya kijamii iliyomuonesha mwalimu wa shule ya msingi Kakanja iliyopo Wilaya ya Kyerwa, Mkoa wa Kagera akimpiga vikali mwanafunzi wa shule hiyo. Akizungumzia juu ya tukio hilo, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alieleza kuwa vitendo kama hivyo, vimesababisha madhara mengi ikiwemo kuleta taharuki kwa jamii ,athari ya kimwili ,kiakili na msongo wa  “Serikali haitofumbia macho na wala kukubaliana na aina hiyo ya adhabu kali. Tayari serikali imechukua hatua za kinidhamu kwa wahusika.’’ anaeleza Waziri Mkuu Kassim Majaliwa. Anasema serikali imekuwa ikitekeleza afua mbalimbal

KHERI YA SIKUKUU YA KUZALIWA RAIS WETU KIPENZI DKT. SAMIA SULUHU HASSAN

Sisi familia ya DODOMA MEDIA GROUP, DODOMA TV NA DODOMAFM  RADIO tunaungana na familia ya Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais Ikulu na watanzania wote kukutakia Kheri ya Siku ya kuzaliwa kwako. Tunakuombea kwa Mwenyezi Mungu Maisha marefu, azidi kukulinda na kukufanikisha katika kuyatekeleza majukumu yako ya kuwahudumia watanzania, na kuliongoza Taifa letu kwa Amani, Happy Birthday Rais wetu, Dkt. Samia Suluhu Hassan.

WANANCHI WATAKIWA KUKAA MBALI NA SIMU /KOMPUTA KUEPUKA KUUMWA MACHO

             Wananchi wanaotumia simu na Komputer kwa muda mrefu wameshauriwa kukaa umbali wa sentimita 25 kutoka macho yalipo mpaka katika vifaa hivyo ili kuepuka magonjwa ya Macho. Ushauri huo umetolewa na Daktari bingwa wa macho kutoka Hospitali ya Charity Vision Tanzania iliyopo Jijini Dodoma Dokta EDMUND MUSHUMBUSI  wakati akizungumza na Dodoma FM. Dr Mushumbusi   amesema ili kuepuka matatizo yatokanayo na matumizi ya muda mrefu ya vifaa hivyo kama maumivu ya kichwa ni vyema mtu akaweka umbali wa sentimita 25 pamoja na kupumzika kila baada ya muda ili kuyapumzisha macho. Akizungumzia shida anayoweza kuipata mtu anayetumia vifaa hivyo kwa muda mrefu ni maumivu ya kichwa,kuchoka au kuuma kwa macho, kutokuona vizuri pamoja na maumivu ya shingo na mgongo. Amesema kama ilivyo kawaida ya kupumzisha viungo vingine vya mwili macho pia yana takiwa kupumzika kutokana na kuwa na umuhimu mkubwa kwa binadamu. Na Phinna Nimrod                                 

WASHAURIWA KUTUMIA MBOLEA KULIMA KILIMO BORA

      Wakulima katika kijiji cha chikopole wilaya ya Bahi mkoani Dodoma wameshauriwa kutumia njia mbadala ya kufikisha mbolea mashambani mwao ili   kulima kilimo bora. Ushauri huo unakuja baada ya kuwepo na changamoto za kutokuwa na nyenzo za kuwasaidia wakulima hao kufikisha mbolea kwa wingi na kwa muda husika mashambani mwao jambo linalopelekea kutofikia dhamira katika kilimo chao. Akizungumza na Dodoma FM ofisini kwake afisa kilimo na mifugo wa kijiji cha Chikopelo Bwana DANIEL CHUNGA amesema ni kweli changamoto hiyo ipo lakini kila mara wamekuwa wakiwashauri wakulima hao kuanza mapema kusogeza mbolea karibu na mashamba yao kufuatia kuishi karibu na wanapofanyia shughuli zao za kilimo. Bwana CHUNGA amesema pamoja na changamoto hizo wakulima hao wanakabiliwa na mwingiliano kati yao na wafugaji kwani katika kijiji hicho hakuna mpangilio maalumu wa sehemu gani wafugaji wanapaswa kuchungia mifugo yao na badala yake mashamba ya wakulima hutumika kwa ajili ya mal