Jamii imetakiwa kufuata taratibu za kisheria katika ununuzi wa ardhi ili kuepuka migogoro ya ardhi inayojitokeza mara nyingi miongoni mwa familia. Rai hiyo imetolewa na Mwanasheria wa Kujitegemea Bwana Goodluck Ludala ambapo amesema migororo mingi ya ardhi inatokana na watu kutokufuata taratibu za kisheria za manunuzi ambapo inaweza kupelekea mtu kupoteza haki yake . Amesema iwapo mtu atapata migogoro ya ardhi anatakiwa kupeleka shauri lake baraza la kata na baada ya uamuzi kutoka mlalamikaji anapaswa kukaza hukumu katika baraza la ardhi la wilaya jambo ambalo watu wengi huwa hawafanyi na kupoteza haki zao. Aidha amesema kumekuwa na baadhi ya watu wanaopuuza hukumu ya mahakama pasipo kukata rufaa ambapo ameeleza kuwa kufanya hivyo ni kosa kisheria na hapo mlalamikaji anapaswa kutoa taarifa katika mahakama iliyotoa hukumu ili hatua zaidi zichukuliwe. Haya Yamejiri ikiwa ni siku chache baada ya Dodoma FM kupokea kisa cha m...