Skip to main content

MICHEZO

  SIMBA WATINGA BUNGENI ,WATAMBULISHWA RASMI MABINGWA WA LIGI KUU

Mabingwa wapya wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara timu ya Simba imetinga bungeni asubuhi hii baada ya kupata mwaliko wa Spika, Job Ndugai.

Hii ni kawaida kwa Bunge la Jamhuri ya Muungano kuikaribisha timu au wana michezo wanaofanya vizuri kwa ajili ya kuwapongeza na kuwapa motisha.

Simba imefanikiwa kutwaa ubingwa huo baada ya kufikisha pointi 68 huku ikisalia na mechi mbili ili kukamilisha ligi.

Naibu Waziri wa TAMISEMI, Joseph Kakunda aliwasifu Wekundu hao kwa uwezo mkubwa walio onyesha huku akisema wataweza kuiwakilisha vizuri nchi katika michuano ya klabu bingwa Afrika mwakani.

Mbali na Kakunda Wabunge Idd Azan wa Ilala, George Lubereje wa Mpwapwa nao hawakusita kuimwagia sifa timu hiyo kwa kufanikiwa kutwaa ubingwa.

Simba imepitia Dodoma ikitoka Singida iliposhinda bao moja dhidi ya Singida United katika mchezo wa ligi uliofanyika uwanja wa Namfua.

Jana Wekundu hao walicheza mechi ya kirafiki dhidi ya Dodoma Combine uliomalizika kwa sare ya mabao 2-2 uliopigwa uwanja wa Jamhuri. 
 
 
Add caption
Pazia la ligi kuu nchini Uingereza (EPL) limefungwa rasmi hii leo huku Chelsea ikikubali kipigo cha mabao 3-0 kutoka kwa Newcastle United.

Chelsea ambao walikuwa mabingwa watetezi wa michuano hiyo wamemaliza nje ya timu nne bora hivyo msimu ujao watashiriki michuano ya Europa.

Mabingwa watetezi Manchester City wamemaliza ligi hiyo kwa kufikisha pointi 100 kufuatia ushindi wa bao moja dhidi ya Southampton.

Manchester United ilipata ushindi wa bao moja mbele ya Watford huku wakitumia mchezo huo kumuaga nahodha wao Michael Carrick ambaye ametangaza kustaafu soka.

Kwa upande wa Liverpool imeibuka na ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Brighton wakati Tottenham Hotspur  ikipata mabao 5-4 dhidi ya Leicester City.

Matokeo ya mechi zote za EPL

Burnley 1-2 Bournemouth
Crystal Palace 2-0 West Bromwich
Huddersfield 0-1 Arsenal
Liverpool 4-0 Brighton
Man United 1-0 Watford
Newcastle United 3-0 Chelsea
Southampton 0-1 Manchester City
Swansea City 1-2 Stoke City
Tottenham 5-4 Leicester City
West Ham United 3-1 Everton 

Huddersfield wabaki ligi kuu huku Gurdiola akiivunja rekodi ya Mourinho

 

Alama moja katika uwanja wa Stamford Bridge umeihakikishia klabu ya Huddersfield kuwepo katika ligi kuu nchini Uingereza katika msimu ujao, matokeo ya leo yanawafanya kufikisha alama 37 katika msimamo wa ligi alama ambazo zinawahakikishia uwepo katika ligi kuu.

 

Habari nyingine kubwa katika mchezo wa leo ni namna ambavyo kocha wa Chelsea Antonio Conte alikipanga kikosi chake akimuacha Eden Hazard nje pamoja na Olivier Giroud na alama moja waliyoipata hii leo inawaweka katika hatihati kushiriki Champions League msimu ujao.

 

Suluhu ya leo ya Huddersfield inamaanisha kwamba timu zote zilizopanda daraja msimu huu zinabaki ligi kuu na hii ikiwa ni mara ya tatu katika historia ya Epl kwa jambo kama hili kutokea ambapo ilishatokea msimu wa 2001/2002(Blackburn, Fulham na Bolton) na ikatokea pia 

2011/2012(Swansea, Norwich na Qpr)

 

. 

 

Kwingineko mabao mawili ya Riyad Mahrez na moja la Jamie Vardy yalitosha kuiua Arsenal bao 3 kwa 1, ambapo matokeo haya yanawafanya Arsenal kuwa timu ambayo inaongoza kwa matokeo mabovu ugenini kuliko timu yeyote katika ligi kuu 5 kubwa barani Ulaya kwa mwaka 2018.

 

Manchester City waliipiga Brighton & Hove Albion mabao 3 na hii kuwafanya City kushinda michezo 31 katika msimu huu wakiifikia rekodi ya Tottenham waliyoiweka 1960/1961 ya kushinda idadi ya michezo kama hiyo katika ligi, lakini pia Gurdiola anakuwa ameivunja rekodi ya Jose Mourinho ya kumaliza ligi akiwa na alama nyingi ambapo Pep amefikisha 97, huku Mou alifikisha 95 msimu wa 2004/2005.

SIMBA WAANZA SAFARI KUELEKEA SINGIDA, KIKOSI KITAPITA BUNGENI KUPOKEA BARAKA ZA MCHEZO


Kikosi cha Simba kimeanza safari ya kuelekea Singida kwa ajili ya mtanange wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Singida United.

Simba itapitia katika Makao Makuu ya nchi, Dodoma, kuweka kambi fupi kabla ya kuendelea na safari ya kuelekea mjini Singida.

Taarifa kwa mujibu wa Meneja wa kikosi hicho cha wekundu wa Msimbazi, Richard Robert, amesema kuwa kikosi kitapita jijini hapo ili kuweka kambi fupi kabla ya kuendelea na safari.

Inaelezwa kuwa Simba wamepanga kupitia Bungeni kwa ajili ya kupata baraka za kuelekea mechi yao na Singida itakayopigwa Mei 12 kwenye Uwanja wa Namfua.

Tayari kikosi hicho kipo njiani hivi sasa kuelekea jijini humo na kesho kitaanza tena safari ya Singida.

Kocha wa Prisons aivua ubingwa Yanga

Kuelekea mchezo wa VPL kati ya Tanzania Prisons dhidi ya Yanga, Kocha mkuu wa Prisons Abdallah Mohamed ‘Bares’ ameivua ubingwa Yanga na kuipa Simba nafasi ya kushinda taji la ligi kuu msimu huu.

                         

Bares amesema Simba inahitaji pointi moja kuwa bingwa wa ligi huku ikiwa na mechi tatu jambo ambalo linaiondoa Yanga katika mbio za ubingwa wa VPL 2017/18.

 

“Tunaona tayari Yanga ameshaondoka kwenye mbio za ubingwa kwa sababu Simba anahitaji pointi moja kuwa mabingwa, mchezo dhidi ya Yanga ni muhimu sana kwetu kupata pointi tatu.”

 

“Nadhani Yanga wanakuja wakiwa wanajiandaa zaidi kwa mechi yao ya kimataifa, huu utakuwa mchezo wa kuandaa mazoezi ambayo yatawasaidia na mapungufu ambayo wameona kwenye mchezo waliofungwa 4-0 USM Alger. Nadhani kikubwa mwalimu atatazama hicho zaidi.”

 

“Kikosi changu kipo vizuri isipokuwa tutamkosa mchezaji mmoja Salum Kimenya ambaye anakabiliwa na kadi tatu za njano kwa hiyo hatutaweza kumtumia lakini tuna vijana wengi ambao wako vizuri na tunaamini watafanya vizuri.”

 

“Kila timu imejipanga kwa namna yake, sisi tumejipanga kukamata nafasi za juu nadhani Yanga kama kawaida yake haitaki kushuka chini zaidi inataka kubaki palepale nadhani mchezo utakuwa ni mkubwa lakini tuangalie dakika 90 zitaamua nini.”

 

“Tunacheza na Yanga ambayo jina lake ni kubwa lakini timu ya kawaida kabisa, sisi kama unavyoona mwenendo wetu sio mbaya kwa hiyo tunataka kuendeleza hiyo rekodi yetu.”

 

 

MWENYEKITI ABAJALO AFUNGULIWA KUJIHUSISHA NA SOKA, MMOJA RUFAA YAKE YATUPILIWA MBALI

                              

Kamati ya Rufaa ya Maadili imeitupilia mbali rufaa ya Dustan Mkundi Ditopile na kuiagiza Sekretariati kulipeleka suala kake katia vyombo vya ulinzi kwa uchunguzi zaidi.

Dustan alifungiwa kutokana na kuwasilisha fomu ya mapato tofauti na fomu halisi ya Bodi ya Ligi.

Wakati huohuo Mwenyekiti wa Abajalo FC na mjumbe wa Bodi ya Ligi alikiri kutoa maneno makali mbele ya vyombo vya habari akiwa kama kiongozi.

Kutokana na kukiri kwake, Kamati imemfungulia kifungo cha kutojihusisha na soka Edgar Chibula na kumpa onyo kali.

NIYONZIMA AMWAHIDI AHADI HII KOCHA WAKE

Baada ya kurejea uwanjani, kiungo wa Simba, Haruna Niyonzima raia wa Rwanda amemuahidi makubwa kocha wake Pierre Lechantre kwa kusema kuwa ni nafasi nzuri kwake kuonyesha kiwango baada ya kupata nafasi ya kucheza.

Niyonzima alikaa nje ya uwanja tangu na kukosa baadhi ya mechi baada ya kuumia enka kulikom­sababishia kupelekwa nchini India kwa matibabu kabla ya kurejea kikosini.

Kiungo huyo machachari alipewa nafasi ya kucheza kwa mara ya kwanza tangu arudi majeruhi katika mchezo dhidi ya Njombe Mji, Jumatatu wiki hii kwenye Uwanja wa Sabasaba, aki­chukua nafasi ya Shiza Kichuya dakika ya 81, ambapo Simba ilishinda mabao 2-0 yaliyofungwa na John Bocco.

Niyonzima alisema, amefurahi kuona amerejea uwanjani kwa mara nyingine baada ya kukaa nje kwa muda mrefu.

 

YANGA YATUA MOROGORO KWA AJILI YA DICHA 

 

Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Bara, Young Africans, wameweka tena kambi nyingine maalum mjini Morogoro kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Welayta Dicha FC.

Yanga ilitua Morogoro jana ikitokea mkoani Singida kucheza mchezo wa Kombe la FA dhidi ya Singida United kwenye hatua ya robo fainali ambapo iliondolewa kwa changamoto ya mikwaju ya penati (4-2).

Kikosi hicho kimeshindwa kufika Dar es Salaam na kuamua kuishia Morogoro kwa ajili ya mawindo dhidi ya Welayta Dicha FC kutoka Ehtiopia inayotaraji kuwasili nchini wiki hii.

Yanga itacheza na Waethiopia hao Jumamosi ya Aprili 7 2018 katika Uwanja wa Taifa Dar es Salaam, kabla ya kurudiana nao huko Ethiopia baada ya wiki moja mbele.

 

KUMBE KOCHA NJOMBE NI MJANJA, AMETUMIA MBINU HII KUIMALIZA SIMBA LEO

Wakati pambano la Ligi Kuu Bara likisubiriwa jioni ya leo kati ya Njombe Mji FC dhidi ya Simba kwenye Uwanja wa Sabasaba mjini Njombe, Kocha Msaidizi wa timu ya Njombe, Mrage Kabange, ameeleza mbinu alizoziandaa kupata matokeo.


Mrage ameeleza kuwa walilazimu kupeleka nusu kikosi mjini Shinyanga kwa ajili ya mchezo wa Kombe la Shirikisho dhidi ya Stand United na kubakisha kingine mjini Njombe.

Kocha huyo amesema iliwabidi wafanye hivyo ili wapate nguvu ya kupambana na Simba kwenye ligi kutokana na hali ya kikosi chao kuwa mbaya kwasababu wako kwenye mazingira ya kushuka daraja.

Taarifa zinaeleza kuwa kikosi cha Njombe kilichopelekwa Shinyanga kilikuwa na wachezaji wengi wa akiba na waliosalia Njombe walikuwa ni wale wa kikosi cha kwanza.

Uamuzi huo ulifanywa ili kuipa timu nguvu ya kupigania alama tatu muhimu dhidi ya Simba ambayo imekosa ubingwa wa ligi kwa miaka mitano sasa.

Mechi hiyo inachezwa leo Uwanja wa Sabasaba kuanzia majira ya saa 10 kamili jioni.

      

ZLATAN AWASILI MAREKANI NA KUPOKELEWA KWA SHANGWE NA MASHABIKI WA LA GALAXY

 



Aliyekuwa Mshambuliaji wa klabu ya Manchester United, Zlatan Ibrahimovic, amewasilini jijini California, Marekani, na kupokelewa na mashabiki wa LA Galaxy.
Zlatan alitangaza kuhamia Marekani baada ya kukubaliana na klabu yake ya zamani kuvunja mkataba kufuatia kuwa nje ya dimba kwa muda mrefu sababu ya majeraha.
Mshambuliaji huyo atasaini mkataba wa kuicheza LA Galaxy iayoshiriki ligi kuu nchini humo na inaelezwa anaweza kumaliza maisha yake ya soka akiwa na klabu hiyo.

UCHUNGUZI WA URAI WA KIDAO BADO UNAENDELEA                  

 

                      

 

Idara ya uhamiaji nchini bado inaendelea kuchunguza uraia wa Kaimu Katibu Mkuu wa TFF Wilfred Kidao, afisa habari wa uhamiaji Ally Mtanda amesema uchunguzi bado unaendelea na utakapo kamilika watatoa taarifa rasmi.


“Bado tunaendelea na suala lake la uchunguzi na litakapokuwa tayari tutawaarifu, masuala ya uchunguzi hatuwezi kuyaweka wazi hadi pale tutakapokuwa tumekamilisha ndipo mambo yote yatakuwa hadharani.”


“Wanamicheo wawe na uvumilivu muda sio mrefu mambo yote tutayaweka wazi.”


Mara kadhaa Kidao amekuwa akihojiwa na idara hiyo kutokana na kinachoelezwa kuwa ni kuchunguzwa uraia wake.

                                  YANGA YAMKANA MUDATHIR

                      

Mudathir Yahya anazidi kutawala kwenye vichwa vya habari za michezo akihusishwa kujiunga na Yanga ambao ni mabingwa watetezi wa taji la VPL.

Kiungo huyo anaecheza kwa mkopo Singida United amemaliza mkataba wake na klabu ya Azam hivyo kwa sasa ni mchezaji huru na anaweza kujiunga na timu yoyote atakayoamua mwenyewe.

Mara baada ya uongozi wa Azam kupitia msemaji wake Jafar Idd kutangaza kumruhusu mudathir kuendelea na maisha yake ya soke sehemu nyingine, Yanga inatajwa kuanza kuiwinda saini ya mchezaji huyo wa Zanzibar Heroes na Taifa Stars.

Mwenyekiti wa kamati ya mashindano Yanga Hussein Nyika amesema hadi sasa klabu yao haijaongea na mchezaji yeyote wala hawajafanya usaji wa aina yoyote.

“Hakuna kitu kama hicho sisi (Yanga) tunaelekeza nguvu zetu kwenye mashindano, hatujafika kipindi cha usajili. Yanga inafanya usajili kwa taratibu zake, baada ya mashindano kumalizika lazima mwalimu atuletee ripoti yake anahitaji maeneo gani yajazilizwe hapo ndipo tutaingia msituni kwa ajili ya usajili.”

“Hadi sasa hivi hatujaongea na mchezaji wa aina yoyote na hatujafanya usajili wa aina yoyote. Hatuwezi kufanya usajili kwa sababu mchezaji yupo huru, usajili wetu huwa tunafanya baada ya kupokea ripoti ya mwalimu na mapendekezo yake. Mwalimu ndio anafanya usajili sisi tunatekeleza ambayo mwalimu anaagiza.”

Uongozi wa Singida United umesema, pamoja na Mudathir Yahya kumaliza mkataba na Azam wao wana mipango nae na huenda wakaingia mkataba wa muda mrefu na mchezaji huyo

   

                  WAMBURA :KESHO KUJUA MBIVU NA MBICHI

                 

Kamati ya rufaa ya maadili ya shirikiso la soka Tanzania TFF imetangaza kukutana Jumamosi kwa ajili ya kusikiliza rufaa ya aliyekuwa makamu wa Rais wa shirikisho hilo Michael Wambura aliyefungiwa maisha kujishughulisha na masuala ya soka.


Kaimu afisa habari wa TFF Clifford ndimbo amethibitisha kuhusiana na taarifa hiyo.


“Kamati ya rufdaa ya maadili inataraji kukaa Jumamosi ya Machi 31 ambapo itakuwa saa 5 asubuhi, pamoja na mambo mengine pia itasikiliza rufaa ya Michael Wambura ambaye alikata rufaa.”


“Anaruhusiwa kuja kutoa utetezi wake kwa njia ya mdomo, maandishi au kuleta vielelezo vyote vya utetezi wake pia anaweza kuleta mwakilishi akiwa na barua ya uwakilishi au anaweza kuamua kutokuja kabisa.”


“Tayari wito wake ameshapelekewa na bila shaka atakuwa amesha upokea, kuelekea katika shauri hilo siku ya Jumamosi gharama zitakuwa juu yake mwenyewe.”


Wakili wa Wambura Emanuel Muga amesema mteja wake amepokea wito kutoka kamati ya rufaa ya maadili na atakwenda kutetea haki yake mbele ya kamati hiyo.


“Ni kweli Michael Wambura amenieleza kwamba amepata wito na wito huo ni kwa ajili ya kikao cha Machi 31 saa 5 asubuhi pale TFF atakapoenda kusikilizwa.”


“Wambura amesema yupo tayari kwenda kutetea haki yake mbele ya kamati na ana hoja zake na amethibitisha kwamba atakwenda.”

 

MKUTANO MKUU YANGA KUFANYIKA MEI 5 DAR ES SALAAM KUJADILI MUSTAKABALI MPYA WA KLABU

KLABU ya Yanga inatarajiwa kufanya Mkutano wake Mkuu wa mwaka Mei 5 mwaka huu katika ukumbi utakaotajwa baadaye mjini Dar es Salaam.

  Mkutano huo ni matokeo ya kikao cha Kamati ya Utendaji ya Yanga kilichofanyika Jumapili iliyopita mjini Dar es Salaam chini ya Kaimu Mwenyekiti, Clement Sanga ambacho kimewataka wanachama kujindaa kwa ajenda zitakazotangazwa baadaye.

  Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu wa Yanga SC, Charles Boniface Mkwasa alipozungumza na Waandishi wa Habari makao makuu ya klabu, Jangwani mjini Dar es Salaam.

  Mkwasa, mchezaji na kocha wa zamani wa Yanga pamoja na timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars amesema kwamba mkutano huo utakuwa maalum kwa wanachama kujadili masuala mbalimbali na kwa ujumla mustakabali wa klabu.

               AZAM YATANGAZA KUACHANA NA MUDATHIR YAHAYA



Uongozi wa klabu ya Azam FC umetangaza kuwa mchezaji wake, Mudathir Yahaya, yupo huru kuelekea sehemu nyingine baada ya kumaliza mkataba wake.

Kupitia Afisa Habari wa Azam FC, Jaffer Idd, amesema mchezaji huyo yupo huru hivi sasa na kama timu nyingine ikimuhitaji, ruksa kumsajili.

Yahaya aliondoka Azam FC na kutimkia Singida United kwa mkopo Julai 17 2017 baada ya mkataba wake wa miezi mitatu uliokuwa umesalia ndani ya Azam kumalizika.

Mpaka sasa Yahaya yuko Singida United akijiandaa na wenzake kuelekea mchezo wa Kombe la Shirikisho utakaopigwa Aprili Mosi 2018 dhidi ya Yanga kwenye Uwanja wa Namfua.
 


Wachezaji wa Simba waliokuwa wanaitumikia Taifa Stars wanatarajiwa kujiunga na kikosi cha Simba kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Njombe Mji.

Simba inajiandaa kucheza na Njombe Aprili 3 2018 katika Uwanja wa Sabasaba mjini Njombe, mchezo ambao ulikuwa ni wa kiporo.

Wachezaji hao waliokuwa Stars ni Erasto Nyoni, Aishi Manula, Shiza Kichuya, Shomari Kapombe pamoja na Said Ndemla.

Simba inaendelea na mazoezi jioni ya leo kwenye Uwanja wa Boko Veterani kabla haijakabiliana na Njombe Mji FC Aprili 3 2018.
 

LIGI YA WILAYA YA DODOMA MJINI MAMBO NI MOTO SASA

baada ya semini ya hapo jana ya viongozi wa vilabu shiriki wa ligi ya wilaya ya Dodoma  chama cha soka wilaya ya Dodoma mjini Dufa kimetoa ratiba rasmi pamoja na makundi ya ligi hiyo ambayo inashirikisha vilabu 20


omaroo Omary materazi ni katibu msaidizi wa dufa anabainisha juu ya malengo ya semina ya jana pamoja na ratiba nzima ya ligi ya wilaya ya dodoama mjni ambayo inatarajia kuanza kutimua vumbi aprili 4 2018

Na Selemani Juma 



BINGWA WA MKOA WA DODOMA NI GWASSA NATO


Baada ya kutangaza bingwa hapo jana wa ligi ya mkoa wa Dodoma Chama cha soka mkoani Dodoma dorefa  kimeshukuru wadau pamoja na wanamichezo wote ambao walijitokeza tangu lingi hiyo ianze mpaka kufiko ukomo hivi karibuni


Akizungumza na sport bomba Katibu wa chama cha soka mkoani Dodoma dorefa ham isi kisoi amesema kuwa bingwa wa mkoa wa Dodoma ni Gwassa nato lakini tangu kwa kuanza kwa ligi hiyo kumekuwa na mwitikio wa wadau kuunga mkono licha ya changamoto zilizojitokeza katikati mwa ligi hiyo


Hamisi kisoi huyu hapa akibainisha namna walivyojipanga kuhakikisha ligi ijayo inakuwa na maandalizi ya kutosha tofauti na msimu huu

Na Selemani Juma


KOCHA MTIBWA SUGAR :DFC WANAWEZA KUPANDA LIGI KUU


Na leo katika uwanja wa ccm jamhuri kulikuwa na mchezo wa kirafiki baina ya klabu ya Dfc dhidi ya mtibwa sugar kutoka mkoani morogoro.
Mchezo huo umekamilika jioni ya leo kwa kushuhudia Mtibwa sugar wakiibuka na ushindi wa goli 2 dhidi ya sifuri kwa wenyeji wao Dfc


Baada ya mchezo huo kocha wa mtibwa sugar zubery katwilla amesema kuwa mchezo wao huo ni miongoni mwa maandalzi ya mchezo wao wa kombe la shirikisho dhidi ya azam huku pia akitoa somo kwa klabu ya dfc namna gani wafanye ili waweze kufanikiwa katika harakati za kupanda ligi kuu


 


Pia tuliweza kumtafuta katibu wa klabu ya dfc Super Fortu kujua baada ya mchezo huo wa leo klabu wanamipango gani katika kuhakikisha wanacheza michezo mingine kama ilivyokuwa ahadi yao kwa wadau wa soka na mashabiki wa dfc .
Clip super fortu

 

MKUDE :NJE WIKI MOJA

Kiungo wa klabu ya Simba, Jonas Mkude, imearifiwa anaweza akakosekana dimbani kwa takribani wiiki moja kufuatia kuumia juzi mazoezini.

Simba imekuwa ikifanya mazoezi katika Uwanja wa Boko Veterani jijini Dar es Salaam ambapo hivi sasa inajiandaa na mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Njombe Mji FC utakaopigwa Aprili 3 2018.

Kwa mujibu wa Daktari wa timu, Yassin Gembe, amesema Mkude anaweza akachukua wiki moja badala ya siku mbili au tatu zilizotajwa awali.

Mkude aliumia mguu wakati wa mwazoezi baada ya kukutana na Mzamiru Yassin wakati wakiwania mpira.

 

 TFF YATUMA MAOMBI TLS IKIOMBA WAKILI WA WAMBURA APIGWE 'STOP' MARA MOJA

                        

Shirikisho la Soka nchini (TFF), limekiomba Chama cha Wanasheria Tanzania (TLS), kumzuia Wakili Emmanuel Muga, kumuwakilisha aliyekuwa Makamu wa Rais wa TFF, Michael Richard Wambura, katika rufaa yake inayotegemewa kusikilizwa muda wowote kuanzia wiki hii.

Taarifa hiyo iliyosambaa inaeleza kuwa Wakili Emmanuel Muga alikuwa ana mkataba na TFF, na suala la Ndug. Wambura lilitendeka enzi za uhai wa mkataba wake.

TFF inaiomba TLS imuagize Muga asitishe mara moja uwakilishi wake katika mashauri mengine yanayoihusisha TFF na viongozi wake, wanachama au walalamikaji wengine ili kuondoa mgonagano huu wa kimaslahi.

Wakili Muga anamuwakilisha Wambura aliyefungiwa kujihusisha na masuala ya soka baada ya TFF kugundua kuwa aliutumia kinyume na matwaka fedha za shirikisho hilo, pamoja na makosa mengine mbalimbali.

 =======================================================

 

Kikosi cha Taifa Stars kinashuka Uwanjani 'Mustapha Tchaker Stadium' kucheza mchezo wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya Algeria jioni ya leo huko Blida, nchini humo.

Mchezo huo ambao ni wa kalenda ya FIFA, utakuwa unaipa nafasi Tanzania ya kulipiza kisasi baada ya kupoteza kwa mabao 7-0 wakati timu hizo zilipokutana mara ya mwisho 2015.

Tanzania ilifungwa idadi hiyo ya mabao wakati wa kuwania kufuzu kuelekea michuano ya Kombe la Dunia kuelekea Urusi mwaka huu.

Licha ya kufungwa, timu zote hazijafanikiwa kufuzu kushiriki michuano hiyo inayotarajia kuanza miezi kadhaa ijayo.
Lakini wakati hayo yakijiri ni kwamba shirikisho la soka tz limeanza mchakato wa kutafuta kocha mpya wa kukinoa kikosi cha starz kutokana mkataba wa salum mayanga kufika ukingoni
====================================================

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa  Tanzania (Takukuru),  imeieleza mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa imeshakamilisha upelezi wa kesi ya Rais wa  Simba, Evans Aveva na makamu wake, Geofrey Nyange 'Kaburu' na wapo tayari  kuanza kusikilizwa.
Aveva leo ameshindwa kuhudhuria tena mahakamani katika kesi  yake utakatishaji fedha inayomkabili ikiwa ni mara ya saba mfululizo kutokana kutokana na kulazwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili  kufuatia hali yake ya kiafya kutokuwa nzuri.
Aveva anakabiliwa na mashtaka matano ya kughushi, kuwasilisha nyaraka ya uongo na kutakatisha fedha  kiasi cha dola 300,000 za Kimarekani akiwa na  makamu wake wa rais Geofrey Nyange 'Kaburu'.
Katika kesi hiyo ambayo itakuwa ikisikilizwa mbele ya   Hakimu Mkazi wa Makahama  ya Kisutu, Thomas Simba badala ya  Victoria Nongwa ambapo wakili wa Takukuru, Nassor Katuga ameiambia mahakama hiyo kwamba kesi hiyo ilikuja kwa ajili ya kutajwa lakini wameshakamilisha upepelezi hivyo wapotayari kuendelea kwa hatua ya kuanza kusikilizwa.
Katuga  alisema kuwa kusema kuwa lakini wapokea taarifa kuwa mshitakiwa namba moja (Aveva) ameshindwa kufika mahakamani kwa kuwa anaumwa na melazwa Muhimbili nabadala yake yupo Kaburu peke yake ambaye ni mshitakiwa namba mbili.
Kwa upande wa  hakimu Simba alisema kuwa ni vyema kufuatilia hali yake kwa kuwa kesi ipo tayari kusilizwa ili iweze kuendana na muda kutona na kuwa ni ya muda mrefu ambapo amepanga kuanza kusilizwa  Aprili 5, mwaka huu.
@@@@@@@@@@@@@@@@@@@
Baada ya Yanga kupangwa na Welayta Dicha ya Ethiopia kwenye Kombe la Shirikisho Afrika na CAF jana Machi 21 2018, timu hiyo imeguwa gumzo kwa watu.
Welayta Dicha ni timu inayoshiriki Ligi Kuu Ethiopia na msimu huu ipo nafasi ya nane kwenye Msimamo wa Ligi Kuu nchini humo ikiwa imecheza jumla ya michezo 15 na kujikusanyia alama 19.
Kupitia mitandao mbalimbali na hata vijiweni baadhi ya watu wamekuwa wakihoji kuhusiana na timu hii kama itaweza kusonga mbele kutokana na kutokujulikana kwake zaidi.
Kuna baadhi pia wapo wanaoona kama Yanga imepata mteremko wa kupita kirahisi kwa nafasi iliyopo kwenye Msimamo wa Ligi.
Yanga imepangwa kucheza na klabu hiyo baada ya kuondoshwa kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika, kufuatia kichapo cha mabao 2-1.

====================================================
Gor Mahia (Kenya), Young Africans (Tanzania) na Rayon Sport (Rwanda) zimefahamu wapinzani wake katika mechi za mtoano zitakazoamua timu za kushiriki hatua ya makundi ya kombe kwa shirikisho la vilabu barani Afrika.
Katika droo iliyochezeshwa jana mjini Cairo, Young Africans imepangwa kucheza na Wolaita Dicha ya Ethiopia, Rayon Sport itacheza dhidi ya Costa do Sol ya Msumbiji na Gor Mahia dhidi ya Supersport United ya Afrika Kusini.
Kwenye mechi za kwanza za hatua hiyo, timu zote tatu zitakuwa nyumbani kati ya Aprili 6-8 na kwenda ugenini Aprili 17-18 na endapo zitafuzu basi moja kwa moja zitaingia kwenye droo ya hatua ya makundi.
===================================================

Bingwa wa uzito wa juu katika mchezo wa Ngumi Anthony Joshua AJ wa Uingereza amemuonya Joseph Parker wa New Zealanand ambaye ni mpinzani wake katika pambano litakalofanyika machi 31 mjini Cardiff.
Katika maneno yake, AJ amemwambia Joseph ajiandae na pambano gumu ambalo litaamua bingwa wa mkanda wa WBO.
Katika hatua nyingine AJ amekubali uwezo mkubwa wa kupigana alionao Joseph.
===============================================
Mshambuliaji wa Manchester United, Alexis Sanchez, amesema alitarajia mambo kwenda sawa baada ya kujiunga na Manchester United January 2018.
Mchezaji huyo ameeleza hayo baada ya kuona mambo yanaenda tofauti na alivyotarajia mpaka sasa tangu aondoke Arsenal na kutua Old Trafford.
Sanchez mpaka sasa amepata nafasi moja tu ya kucheka na nyavu katika michezo 10 aliyoichezea Manchester United tangu ajiunge.
Aidha, Mshambuliaji huyu amekiri kuwa anahitaji kupambana zaidi ili kuweza kuzoea maisha mapya ndani ya United ambayo bado ni klabu ngeni kwake hivi sasa.

BAADA YA KUBEBA TUZO YA MCHEZAJI BORA WA MWAKA URENO, RONALDO ASEMA YEYE NI BORA SIKU ZOTE



Kwa mara ya pili mfululizo, Mshambuliaji wa Real Madrid na timu ya taifa ya Ureno, Cristiano Ronaldo, ametwaa tuzo ya mchezaji bora wa mwaka 2017 katika taifa lake maarufu kama Quinas de Ouro.

Tuzo hiyo ambayo alikabidhiwa jana Jumatatu, Ronaldo alikuwa akiiwania na wachezaji Bernardo Silva wa Manchester City pamoja na Golikipa wa Sporting CP ya Ureno, Rui Patricio.


Baada ya kuzawadiwa, Ronaldo alisema yeye anaamini bado ni bora na ataendelea kuwa hivyo, hata kama atasemwa kwa namna gani, na hilo atazidi kuwaonesha Uwanjani.

"Naamini kuwa mimi ni bora, vyovyote watakavyosema mimi nitawaonesha ubora wangu Uwanjani" alisema.


Ronaldo ametwaa tuzo hiyo kutokana na mafanikio makubwa ya soka mwaka 2017 kwa kuweza kuisaidia Real Madrid kubeba taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya na kuchukua ubingwa wa La Liga.


Mbali na mataji hayo, Ronaldo pia alifanikiwa kutwaa tuzo ya mchezaji bora wa dunia 'Ballon d'Or kwa mara ya pili mfululizo na kufanya awe na jumla ya tuzo 5 sawa na Lionel Messi.

 

MAKOCHA WAFUNGIWA BAAADA YA VURUGU 


                         Related image

Kamati tendaji ya chama cha soka mkoani dodoma imewafungiwa miezi sita  na kuwatoza faini  makocha wa vilabu vya gwassa nato ya chang’ombe na Watumishi ya mpwapwa kutokana na makosa mbalimbali ikiwemo tukio la vurugu katika mchezo wa Gwassa dhidi ya watumishi


Kupitia taarifa  ya DOREFA kwa vyombo vya habari imesema kuwa  katika mchezo wa gwassa dhidi ya watumishi uliofanyika tarehe 18 mwezi wa 3 mwaka 2018 wameabaini matukio mbalimbali,1mashabiki kufanya vurugu,walimu wa timu mbili hizo kugombana,kumtukana msimamizi wa kituo,kocha msaidizi wa timu ya watumishi kuzuia wachezaji kutoendelea na mchezo,timu ya watumishi kugoma kuendelea na mchezo  na baadhi ya wachezaji kujihusisha na vurugu.


Kupitia kamati tendaji  ambayo imekata hapo juzi wamatoka na maamuzi ya timu ya gwassa pamoja na timu wa watumishi vimetozwa faini ya shilingi laki moja kila mmoja kutoka na msahbiki wake kuhusika na  vurugu na fedha hizo zinatakiwa kulipwa kabla ya michezo inayofutia.

Baada ya taarifa hiyo nilimtafuta mtendaji mkuu wa chama cha soka mkoani dodoma Hamisi kisoi Amesema kuwa kutoka na maamuzi hayo ,wataendelea kuhakikisha wanasimamia ligi hiyo kwa misingi ya usawa na uwazi na haki mpaka bingwa hapatikane

Pia tumezungumza na kocha wa Gwsaa nato Juma ikaba ambaye amefungiwa miezi Sita na kutozwa faini ya shilling laki moja amesema kuwa kutoka na maamuzi hayo ameyapokea hana budi kukubali juu ya hilo

Wadau wa soka wanasemaje juu ya maamuzi haya,super fortu ambaye pia ni katibu wa timu ya DFC yeye ni mdau wa soka ametoa pongezi kwa chama cha soka mkoani dodoma juu ya maamuzi hayo

NA SELEMANI JUMA

    

                                LIGI YA DUFA KUANZA APRIL 4

                   Image result for Soccer image 

Ligi ya wilaya ya dodoma mjini maarufa kama ligi ya DUFA inatarajia kuanza kutimua vumbi kuanzia april 4 kwa kushirikisha vilabu 20 vya wilaya ya dodoma mjini


Kupitia taarifa kutoka kwa katibu wa Msaidizi wa  DUFA Omaroo amesema kuwa kwa sasa DUFA wapo kwenye mipango ya mwisho ya kuhakikisha  vilabu vinakamilisha ada ya ushiriki kabla ya kuanza kutoa semina kwa vilabu ,viongozi na waamuzi ambao watacheza ligi hiyo.


Amesema kuwa tayari wameshafanya vikao vitatu ambavyo vimelenga kumaliza mchakato wakuanza ligi ya wilaya ya dodoma mjini


Omaroo amesema ligi ya msimu hii itafanyika kwa mtindo wa siku tatu toafuti na msimu uliopita ambapo utachezwa kwa siku jumamosi,jumapili pamoja na jumatano hiyo ni kutokana na vilabu kukosa fedha za kumuda kila siku kushiriki ligi.


Aidha amesema kiwanja ambacho kitatumika katika ligi hiyo ni uwanja wa Ccm Jamhuri ambao utatumika kwa siku zote tofauti na wiki ya maandalizi ya siku ya muungano ambapo watawajulisha vilabu kuhusu uwanja utakaotumika kuchezwa kwa wiki ya muungano.

NA SELEMANI JUMA KODIMA 

 

 

KILA LA HERI SIMBA NA YANGA MISRI NA BOTSWANA LEO…TUNAWATAKIA USHINDI NA KUSONGA MBELE


WAWAKILISHI wa Tanzania kwenye michuano ya Afrika, Simba na Yanga leo wapo ugenini kwa michezo ya marudiano ya hatua ya 32 Bora.

 
Yanga watakuwa wageni wa Township Rollers Uwanja wa Taifa mjini Gaborone, Botswana kuanzia Saa 10:45 jioni katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa na Simba watakuwa wageni wa Al Masry Uwanja wa Port Said nchini Misri kuanzia Saa 2:30 usiku.

 
Yanga wanahitaji lazima ushindi wa mabao 2-0 ili kwenda hatua ya makundi, baada ya kufungwa 2-1 kwenye mchezo wa kwanza Jumanne ya wiki iliyopita Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Simba SC wanataka ushindi wowote, hata wa 1-0 ili kusonga mbele katika hatua ya mwisho ya mchujo baada ya sare ya kufungana mabao 2-2 kwenye mchezo wa kwanza Dar es Salaam.

 
Yanga ikiitoa Rollers itakwenda hatua ta makundi ya Ligi ya Mabingwa, ambayo kihistoria itakuwa mara yake ya pili baada ya mwaka 1998, lakini tolewa itaingia kwenye kapu la kuwania kucheza hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho.

 
Simba SC ikishinda leo itacheza na moja ya timu zilizotolewa kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika kuwania nafasi ya kucheza Kombe la Shirikisho, lakini ikitolewa itarejea nyumbani moja kwa moja.
Kila la heri wawakilishi wetu. Mungu zibariki Simba na Yanga. Mungu ibariki Tanzania. Amin.  

 

BREAKING: RAIS WA FIFA ATHIBISHA RASMI KUTUMIKA KWA VAR KOMBE LA DUNIA 2018 RUSSIA

Teknolojia ya Video Assistant Referees (VAR), imethibitishwa rasmi kutumika kwenye michuano ya Kombe la Dunia mwaka huu nchini Russia.
                        

Rais wa Shirikisho la Soka Duniani (FIFA), Gianni Infantino amethibisha hilo leo.
Majaribio ya teknolojia hiyo ya VAR yalifanyika katika nchi za Germany na Italy katika msimu huu.
Infantino amesema inabidi mpira wa soka uishi kuendana na wakati hivyo amefikia hatua hiyo ili kuwasaidia Waamuzi kutoka maamuzi sahihi Uwanjani.
"Tunahitaji kuishi kuendana na wakati, tulihitaji kuwapa Waamuzi vifaa ambavyo vitawasaidia kutoa maamuzi sahihi Uwanjani" alisema.

 

KISA MESSI, LAWAMA ZOTE ATUPIWA MLINDA MLANGO THIBAUT COURTOIS

                        

Baada ya Chelsea kuondoshwa kwenye Ligi ya Mabingwa Barani Ulaya dhidi ya FC, Barcelona kwa jumla ya mabao 3-0, lawama zote zinatupiwa kwa mlinda mlango, Thibaut Courtois.

Kupitia mitandao mbalimbali mashabiki wengi wa Chelsea wamemuandama Golikipa huyo, wapo wengine wanasema amechoka na pengine aondoke klabuni hapo na akatafute maisha mahala pengine.

Courtois aliruhusu mabao matatu ya Lionel Messi aliyefunga mawili, pamoja na Oeusman Dembele aliyefunga moja na jumla kuwa 3-0.

Mabao aliyofungwa na Messi yamekuwa gumzo zaidi, kutokana na baadhi kudai Courtois angeweza kuokoa mipira hiyo iliyopita katikati ya miguu yake.

Kitendo cha kuruhusu mabao hayo kimekuwa kero kubwa kwa mashabiki wa Chelsea ambao timu yao ishatolewa rasmi kwenye mashindano.

Baada ya Barcelona kufuzu kuingia robo fainali, droo ya timu zitakazokutana kwenye hatua hiyo inataraji kupangwa kesho.

Timu zilizofuzu ni Liverpool, Real Madrid, Manchester City, Bayern Munich, AS Roma, Sevilla, Juventus na FC. Barcelona.

 

 

RASMI WAMBURA AFUNGIWA MAISHA KUTOJIHUSISHA NA SHUGHULI ZA SOKA

Kamati ya Maadili ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), imemfungia maisha kutojihusisha na shughuli za Soka Makamu wa Rais wa TFF, Michael Wambura.

Wambuwa amefungiwa kutokana na kupokea fedha zisizo halali kiasi cha Shilingi milioni 84, kugushi nyaraka za malipo, na kula njama kulipwa fedha na waliokua viongozi wa TFF Jamal Malinzi na Selestin Mwesigwa.


KOCHA MRUNDI WA SIMBA ANAAMINI WATAFANYA HIVI MAAJABU MISRI KWA AL MASRY

Kocha Msaidizi wa Simba Mrundi, Masoud Djuma amesema nguvu zao wamezielekeza kwenye mchezo wao wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Al Masry ya Misri na baada ya hapo wanarejea kwenye Ligi Kuu Bara kupambana na Yanga.




Kauli hiyo ameitoa kocha huyo baada ya Yanga kuwafikia kwa pointi 46 katika msimamo wa ligi huku Simba wakiongoza kwa idadi ya mabao ya kufunga ambayo ni 49 huku watani wao wakiwa na 38.


Simba leo inatarajiwa kusafiri kwenda Misri kuwafuata Al Masry watakaovaana Jumamosi hii kwenye Uwanja wa Port Said unaoingiza mashabiki 17,988.




Djuma alisema hivi karibuni walikutana na kufanya kikao na wachezaji wao na kikubwa waliwasisitiza kusahau matokeo ya watani wao Yanga katika ligi na badala yake kuelekeza akili zao mchezo dhidi ya Al Masry.

 

 =============================================

Kikosi cha Simba kinataraji kusafiri jioni ya leo kuelekea Misri, kwa ajili ya mchezo wa marudiano dhidi ya Al Masry SC katika mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika.


Wafuatao ndiyo watakuwa kwenye msafara huo




1. Said Mohamed Nduda
2. Aishi Manula
3. Shomari Kapombe
4-Mohamed Hussein
5. Asante Kwasi
6. Juuko Murushid
7. Yussuf Mlipili
8. Erasto Nyoni
9. Paul Bukaba
10. Jonas Mkude
11. James Kotei
12. Said Ndemla
13. Muzamiru Yassin
14-Mwinyi Kazimoto
15. Shiza Kichuya
16. John Bocco
17. Emmanuel Okwi
18. Nicholaus Gyan
19. Laudit Mavugo
20. Juma Luizio


Kocha Mkuu - Pierre Lechantre
Kocha Msaidizi - Masoud Djuma
Kocha wa Viungo - Mohammed Aymen
kocha wa Makipa - Muharami Mohammed
Docta wa Timu - Yassin Gembe
Meneja wa Timu - Richard Robert
Mtunza Vifaa - Yassin Mtambo


KOCHA WA STAND AISIFIA TFF YA KARIA KWA KUSEMA HAYA

 

Kocha Msaidizi wa Stand United, Athuma Bilal 'Bilo', ametoa mtazamo wake kuhusiana na mwenendo wa Shirikisho la Soka nchini namna unavyoenda tangu uingie madarakani Agosti 2017.

Bilo ameeleza kuwa TFF ya sasa iliyo chini ya Rais Wallace Karia, imejitahidi kufanya marekebisho kadhaa ambayo hayakuwa yanaonekana kipindi cha uongozi uliopita.

Kocha amesema wakati wa uongozi uliopita ilikuwa ni ngumu kwa timu nyingi kwenye ligi kupata matokeo au pointi tatu halali kama ambavyo imekuwa hivi sasa.

Bilo ambaye kikosi cha Stand United kipo katika nafasi ya 11 kwenye msimamo wa ligi, ametoa sifa pia kwa waamuzi walio chini ya watala wa awamu hii kuwa wamekuwa wakijitahidi ukiachana na kipindi cha nyuma.

Licha ya hayo, Bilo ameliomba Shirikisho kuendelea kuboresha mabadiliko haswa kwa waamuzi ambao wengi wamekuwa wakiharibu taswira ya timu kupata matokeo halali, pia kudhorotesha mpira wa Tanzania.

 

Yanga timu pekee iliyoshinda mechi nyingi mfululizo VPL hadi sasa

                       

Kwa mujibu wa takwimu za michezo ya ligi kuu Tanzania bara (VPL) Yanga ndiyo timu pekee ambayo imeshinda mechi nyingi mfululizo kati ya timu tatu za juu zinazowania ubingwa wa ligi hadi sasa.

Yanga imeshinda mechi nane zilizopita mfululizo na kujikusanyia alama 24. Tangu Januari 21, 2018 iliposhinda 1-0 dhidi ya Ruvu Shooting, mabingwa hao mara tatu mfululizo wa VPL wameendelea kushinda mechi zao za ligi hadi Machi 12 walipoishinda Stand United kwa magoli 3-1.

Mara ya mwisho Yanga kushindwa kupata ushindi kwenye mchezo wa ligi ilikuwa Januar 17, 2018 Mwadui ilipowalazimisha suluhu kwenye uwanja wa Uhuru, Dar.

  • 21/01/2018 Ruvu Shooting 0-1 Yanga

  • 27/01/2018 Azam 1-2 Yanga

  • 03/02/2018 Lipuli 0-2 Yanga

  • 06/02/2018 Yanga 4-0 Njombe Mji

  • 14/02/2018 Yanga 4-1 Majimaji

  • 18/02/2018 Ndanda 1-2 Yanga

  • 09/03/2018 Yanga 3-0 Kager Sugar

  • 12/03/2018 Yanga 3-1 Stand United

Simba inafuata nyuma ya yanga, wekundu wa msimbazi wameshinda mechi tano mfululizo kati ya nane lakini imeshinda mechi sita kwa ujumla kati ya hizo nane (kuna mechi ambayo walishinda lakini haikuwa kwenye mfululizo wa mechi za ushindi) walijikuta wakilazimishwa sare mbili na timu za shinyanga (mwadui 2-2 simba, simba 3-3 stand united).

Simba bado inashikilia rekodi ya klabu ambayo bado haijapoteza mchezo hata mmoja wa ligi baada ya kucheza mechi 20.

Vinara hao wa ligi hadi sasa wamefanikiwa kutengeneza alama 20 kati ya 24 ambazo walikuwa wakiziwania katika michezo nane iliyopita.

  • 18/01/2018 Simba 4-0 Singida United

  • 22/01/2018 Kagera Sugar 0-2 Simba

  • 28/01/2018 Simba 4-0 Majimaji

  • 04/02/2018 Ruvu Shooting 0-3 Simba

  • 07/02/2018 Simba 1-0 Azam

  • 15/02/2018 Mwadui 2-2 Simba

  • 26/02/2018 Simba 5-0 Mbao

  • 02/03/2018 Simba 3-3 Stand United

Azam bado ipo kwenye mbio za ubingwa wa ligi licha ya mwendo wake wa kusuasua, katika mechi nane ziliopita imeshinda mechi tatu tu mfululizo, lakini katika hizo mechi nane wameshinda michezo minne wamepoteza mechi mbili na kutoka sare michezo miwili.

Katika michezo nane iliyopita, azam wamepata jumla ya pointi 14.

  • 27/01/2018 Azam 1-2 Yanga

  • 03/02/2018 Azam 3-1 Ndanda

  • 07/02/2018 Simba 1-0 Azam

  • 11/02/2018 Kagera Sugar 1-1 Azam

  • 16/02/2018 Lipuli 0-0 Azam

  • 03/03/2018 Azam 1-0 Singida United

  • 08/03/2018 Azam 1-0 Mwadui

  • 11/03/2018 Azam 2-1 Mbao

 

KLABU BINGWA BARANI ULAYA,SEVILLA JE WANAVUNJA UBABE WA MANCHESTER UNITED.

 

Rekodi zinaonesha kwamba asilimia 70 ya timu ambazo zilitoka suluhu ya bila kufungana ugenini katika mechi ya kwanza, zilifanikiwa kufudhu kwa hatua inayofuata katika michuano ya Champions League.

Kuna njaa sana ya mabao kwa Manchester United dhidi ya vilabu vya kutoka Hispania kwani katika michezo 15 kati ya United na timu za Hispania, United wameshindwa kufunga bao zaidi ya moja, wakifunga 7 katika michezo yote.

Jose Mourinho katika michezo yake 69 ya Champions League amepoteza michezo saba tu nyumbani, na katika michezo hiyo saba aliyopoteza, michezo 5 ni dhidi ya timu kutoka Hispania.

Katika hatua kama hii Manchester United wamepoteza mchezo mmoja tu dhidi ya timu kutoka Hispania katika mechi zao 9 zilizopita na ilikuwa mchezo wao vs Real Madrid msimu wa 2012/2013.

Ni Barcelona tu (mabao 2) ndio ambao wameruhusu nyavu zao kuguswa mara chache zaidi katika msimu huu wa Champions League kuliko Manchester United ambao wameruhusu mabao 3.

Sevilla wanaelekea katika mchezo huu wakiwa na mkosi nchini Uingereza kwani katika michezo yao minne nchini humo hawajawahi kupata ushindi, wakiwa wametoka suluhu mara tatu na kusuluhu mara moja.

 

TSHISHIMBI ATANGAZWA KUWA MCHEZAJI BORA LIGI KUU MWEZI FEBRUARI

                         Image result for papy kabamba

Shirikisho la Mpira wa Miguu (TFF) kupitia Bodi ya Ligi, limemtangaza Mchezaji, Kiungo wa Yanga, Papy Kabamba Tshishimbi, kuwa mchezaji bora wa Ligi Kuu Bara kwa mwezi Februari.
Tshishimbi ametwaa tuzo hiyo baada ya kuisaidia timu yake kuvuna alama 12 huku akifunga mabao matatu na akitengeneza moja.
Mechi ambazo Tshishimbi alihusika kwenye ushindi katika mwezi Februari ni dhidi ya Majimaji, Njombe Mji, Ndanda na Lipuli ya Iringa.
Pius Buswita (Young African) na Emmanuel Okwi (Simba SC) ni wachezaji ambao waliokuwa kwenye kinyang'anyiro cha tuzo hiyo kwa mwezi huu wa pili.
Tshishimbi ambaye ni mshindi wa tuzo hii, atazawadiwa kitita cha milioni moja sambamba na king'amuzi cha Azam TV.

 

WANAOISUBIRI SIMBA WALAZIMISHWA SULUHU KWAO KWENYE LIGI

                Related image

Klabu ya Al Masry imelazimishwa suluhu ya 0-0 dhidi ya El Entag El Harby katika mchezo wa Ligi Kuu Misri uliopigwa jana.

Al Masry wamelazimishwa suluhu hiyo wakiwa wanajiandaa kuwakabili vinara wa Ligi Kuu Bara, Simba SC, Jumamosi ya wiki hii kwenye mchezo wa Kombe la Shirikisho Africa.

Kuelekea mechi hiyo, Al Masry sasa ipo nafasi ya 4 katika msimamo wa Ligi Kuu nchini humo ikiwa na pointi 49 wakiwa wamecheza michezo 26.

Mechi yao dhidi ya Simba itafanyika Machi 17 2018 kwenye Uwanja wa Port Said Jumamosi ya wiki hii.


 

KUKWEPA KUONDOLEWA KIBARUANI, CARRAGHER AOMBA RADHI BAADA YA KUMTEMEA MATE SHABIKI WA MANCHESTER


Mkongwe aliyewahi kuichezea Liverpool, Jammie Carragher, ameomba radhi kutokana na kitendo cha kumtemea mate binti mwenye miaka 14 ambaye ni shabiki wa Manchester United.

Carragher alionekana akimtemea mate binti huyo aliyekuwa kwenye gari na baba yake, ikiwa ni mapema baada ya mechi iliyowakutanisha Manchester United na Liverpool Jumamosi iliyopita.

Binti huyo alimtania Carragher kuhusiana na matokeo ambayo Liverpool alifungwa 2-1, jambo lililosababisha mkongwe huyo kupandwa na hasira.




Carragher ambaye ni Mchambuzi kwenye kituo cha Sky Sports TV, alimpigia msichana huyo Jumapili ya jana kumuomba msamaha kwa kitendo alichokifanya na binti huyo alipokea msamaha wake.

Kwa mujibu wa Sky Sports TV, Msemaji wa Chombo hicho amesema kitendo alichokifanya Carragher si cha kuchukuliwa kawaida, hivyo watakutana naye na ikiwezekana watachukua hatua dhidi yake.


MMILIKI WA TIMU YA LIGI KUU UGIRIKI AINGIA NA BASTOLA UWANJANI AMFYATUE MWAMUZI ALIYEKATAA BAO LA TIMU YAKE





Mechi ya Ligi Kuu nchini Ugiriki imesitishwa ghafla baada ya mmiliki wa timu moja iliyokuwa inacheza kuingia na bastola uwanjani akitaka kumfyatulia mwamuzi.

Mechi hiyo kati ya Paok Salonika dhidi ya AEK Athens ilivunjika dakika za nyongeza baada ya Paok kupata bao dakika za nyongeza lililofungwa na Ferndando Varela.

Wakati huo Paok walikuwa nyuma kwa bao 1-0 na hilo lilikuwa bao la kusawazisha. Lakini mwamuzi alisema halikuwa sahihi sababu ilikuwa ni offside.

Mmiliki wa Paok, Ivan Savvidis ambaye ni mfanyabiashara mkubwa nchini Ugiriki aliamua kuingia uwanjani akiwa na bastola yake tayari kufyatua.

Hata hivyo zilifanyika juhudi kubwa kumuwahi na kumzuia aisitimize alichotaka kukifanya. Walinzi wake ndiyo waliofanya kazi hiyo kuhakikisha wanamdhibiti.

Mashabiki walitakiwa kutoka na kwenda makwao mara tu baada ya mechi hiyo kutoendelea.

Hata hivyo kulikuwa na mkanganyiko kwamba mwamuzi Giorgos Kominis alilikubali bao hilo lakini kukawa na hali ya kutoeleweka.

AEK walikuwa kileleni kwa tofauti ya pointi 3 dhidi ya Paok jambo lilimfanya mmiliki huyo kuona kama wanaonewa.

         

LIGI YA MKOA WA DODOMA YAENDELEA KUSHIKA KASI

                Image result for CHAMA CHA SOKA MKOANI DODOMA DOREFA 

Baada ya hapo jana Ligi ya mkoa wa dodoma kumaliza hatua ya kwanza ya makundi kwa vituo vya dodoma mjini na kituo cha mpwapwa.


ligi hiyo inaingia katika hatua nyingine ya sita bora ambayo inatarajia kuanza kutimua vumbi mwezi huu tarehe 14 ,huku pia dirisha la usajili likiwa limefunguliwa kwa vilabu ambavyo vimeingia hatua ya sita bora

Ni WATUMISHI,AREA D,GURRENS,SHELI AJAX,GWASSA.

Katibu wa chama cha soka mkoani dodoma akizungumzia hayo baada ya hatua ya awali kukamilika hapo jana nini kinafuata katika ligi hiyo.


Amesema kuwa ligi ya mkoa wa dodoma hatua ya sita bora inatarajia kuendelea siku ya jumatano tarehe 14 ambapo kwa sasa vilabu vimepewa nafasi ya kufanya usajili wa wachezaji

 

      

Kikosi cha Simba kimeonesha kweli kimedhamiria kuibuka na ushindi dhidi ya Al Masry SC katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika kesho.

Katika hali isiyo ya kawaida, kikosi hicho kilifanya mazoezi kuanzia majira ya saa moja mpaka mbili usiku wa jana kwenye uwanja wa Boko Vetarani, Dar es Salaam.

Taarifa zinaeleza kuwa wachezaji wapo katika morali nzuri kuelekea mchezo huo utakaopigwa majira ya saa 12 jioni.

Aidha wachezaji Emmanuel Okwi, John Bocco na Haruna Niyonzima wote walijumuika na wenzao kujifua kuelekea mechi hiyo kubwa.

Simba watafanya mazoezi ya mwisho leo kabla ya kuwavaa Al Masry jioni ya kesho.

 

MAN UNITED IMERUDI MAFASI YA PILI                    

                         

Manchester United imerudi kwenye nafasi yake ya pili katika msimamo wa Ligi Kuu Uingereza baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya Crystal Palace.

Mchezo huo ambao ulikuwa na matokeo hasi kwa Manchester United katika kipindi cha kwanza, ulimalizika huku Palace akiwa na bao moja lililofungwa na Townsend dakika ya 11.

Mpaka mapumziko Palace alikuwa mbele kwa bao 1-0.

Kipindi cha pili kilipoanz, Palace walifunga bao la pili na kuufanya mchezo uwe mgumu kwa United baada ya van Aanholt kufunga bao dakika ya 48 ya mchezo.

United walirudi kwa kasi mnamo dakika ya 55 Smalling alifunga, baadaye dakika ya 76 Lukaku naye akacheka na nyavu na mchezo kuwa sare ya 2-2.

Dakika za mwisho kabisa ikiwa imeongezwa moja mchezo umalizike, Matic alipigilia msumari wa mwisho na kufanya matokeo yawe 2-3.

United sasa imerudi tena nafasi ya pili kwa kufikisha alama 62, juu ya Liverpool iliyo na 60.

===========================================

NEYMAR MTABA WAKE NA KAMPUNI YA NIKE WAVUJA

Yuko majeruhi na sasa inadaiwa kwamba Neymar itabidi afanyiwe operesheni ambayo inaweza kumuweka nje ya uwanja kwa kipindi cha miezi mitatu hali ambayo inaweka mashakani kiwango chake.

 


Lakini wakati Neymar akiwa majeruhi, mkataba wake na kampuni ya vifaa vya michezo ya Nike umevuja, mkataba wa Neymar na Nike unaonesha kila kitu atakachopewa katika soka lake kuanzia sasa.

 


Mwanzo Nike walikuwa wakilipana kiasi cha €40m kwa mwaka na sasa Nike wako tayari kutoa $1million kwa Neymar kama atachukua tuzo ya mchezaji bora wa dunia (Ballon D’or) mwakani kama Bonus.

                        


Kiasi hiki ambacho Neymar atapewa na Nike kama akichukua Ballon D’Or kitakuwa kikiongezeka kwa 100% kila mwaka atakayobeba tuzo hiyo na hii ina maana kwamba hadi 2022 anaweza pokea hadi bonus $4million.

 


Nike hawajaishia hapo kwani bado wana mpunga mrefu wameutenga kwa ajili ya mchezaji huyo wa Kibrazil katika michuano ya kombe la dunia inayotarajiwa kuanza hivi karibuni nchini Urusi.

 


Endapo Neymar atabeba kombe la dunia Nike watamkabidhi kiasi cha $50,000 na kama nyota huyo atamaliza michuano hiyo mikubwa zaidi duniani akiwa kama mfungaji bora wa michuano hiyo atachukua $200,000.

 

 

MAN CITY MICHEZI 4 ZAKUWAPA UBINGWA

Klabu ya Manchester city jana Jumapili wakiwa uwanja wao wa nyumbani wa Etihad walifanikiwa kuchomoza na ushidi wa bao 1-0 dhidi ya Chelsea bao lilifungwa na Bernardo Silva Dakika ya 46 kipindi cha pili cha mchezo.

 

Ushindi huo Manchester City umezidi kuwaimarisha kileleni mwa ligi kuu ya England kwa kujikusanyia alama 78 wakifuatiwa na klabu za Liverpool alama 60, Manchester United alama 59,Tottenham Hotspurs alama 58, Tottenham alama 53,huku klabu za West Bromwich Albion,Stoke city na Crystal Palace zikiendelea kushikiria nafasi za mwisho.

                           Man City yakaribia ubingwa ligi kuu ya England

Katika mchezo mwingine Brighton wakiwa ni wenyeji wa Arsenal walifanikiwa kupata alama tatu kwa ushindi wa mabao 2-1, Magoli ya Brighton yakifungwa na Lewis Dunk pamoja na Glenn Murray huku bao la Arsenal bao lao la kufutia machozi likifungwa na Pierre-Emerick Aubameyang.

 

Ligi hiyo ya England inaratarajia kuendelea tena leo jumatatu kwa mchezo mmoja ambapo Crystal Palace wanawakaribisha Manchester United.

 

 

YANGA WAJIANDAA KWA ASILIMIA 100 KUWAVAA ROLLER 

Katibu Mkuu wa Yanga, Boniface Mkwasa amewaondoa hofu mashabiki wa Yanga akiwataka mashabiki wa timu hiyo kujitokeza kwa wingi uwanjani kesho.


Mkwasa alisema shabiki ni mchezaji wa 12, hivyo kujitokeza kwa wingi kutaongeza kutoa hamasa  kwa wachezaji kupambana.
Aliongeza kuwa, kikosi chao kipo fiti kwa ajili ya mchezo huo, amewataka mashabiki kujitokeza kwa wingi.

                             Image result for yanga picha


KIINGILIO cha chini katika mchezo wa kwanza wa Raundi ya Kwanza Ligi ya Mabingwa Afrika baina ya Yanga na Township Rollers ya Botswana Jumanne kitakuwa ni Sh. 5,000.


Taarifa ya Yanga leo imesema kwamba viingilio vingine vitakuwa ni Sh. 20,000 kwa VIP A na Sh. 15,000 kwa VIP B na C.  


Mchezo huo unatarajiwa kufanyika Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam kuanzia Saa 10:30 na timu hizo zitarudiana siku 10 baadaye nchini Botswana.


Yanga itakabiliana na Township Rollers ya Botswana katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika katika uwanja wa taifa, Dar es Salaam, saa 10 kamili jioni.

Upande wa township rollers


Kuelekea mechi ya kesho kati ya Yanga dhidi ya Township Rollers ya Botswana katika mchezo wa Ligi Ya Mabingwa Afrika, Kocha Nikola Kavazovic, amesema analijua soka la Afrika.

                   


Kavazovic amesema amekuwa akilifuatilia vizuri soka la Afrika, na timu yake ipo tayari kupambana na wapinzani katika mchezo wa kesho.

Licha ya kulijua soka la Afrika, Kavazovic, amesema amekuwa akiifuatilia pia Yanga katika michezo mbalimbali ya kimataifa iliyocheza, huku akieleza ameshaitazama ikicheza miwili ya nyumbani na miwili ya ugenini.

==============================================

                         Related image 

WACHEZAJI wawili wa Azam FC, Nahodha Himid Mao ‘Ninja’ na mshambuliaji Wazir Junior, wamerejea rasmi mazoezini jana baada ya kukosekana dimbani kwa muda mrefu wakiuguza majeraha yanayowakabili.

  Himid alikuwa akisumbuliwa na maumivu chini ya goti la mguu wake wa kulia huku Junior akikabiliana na tatizo kwenye kifundo chake cha mguu wa kulia, na tayari nyota hao wameanza kupata nafuu na sasa wanamalizia programu ya mazoezi mepesi kabla ya kuruhusiwa kurejea rasmi katika ushindani.

  Nyota hao wamerejea wakati kikosi cha Mabingwa hao wa Afrika Mashariki na Kati (CECAFA Kagame Cup) kikijiandaa na mchezo ujao wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) dhidi ya Singida United, utakaofanyika Uwanja wa Azam Complex Jumamosi hii saa 1.00 usiku.

Junior anayetakiwa kufanya programu hiyo ya mazoezi mepesi kwa muda wa wiki moja, alisema anamshukuru Mungu kurejea tena dimbani huku akikiri kuwa ‘amemiss’ kucheza mpira.

 
“Kikubwa ni kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kurudi tena na nitaendelea kujituma kama ilivyokuwa awali kutokana na majeruhi haya ndo ilikuwa hivyo lakini tutapambana kama ilivyokuwa mwanzo, nimeumiss sana mpira nimemiss sana kucheza mpira na kuonyesha vile mashabiki wanataka.

 
“Lakini naamini kwa rehema za mwenyezi Mungu tutakaporejea tena basi mashabiki watafurahia vile walivyokuwa wakivisubiria,” alisema Junior
Mchezo huo unatarajia kuwa mkali na wa aina yake kutokana na ushindani wa timu hizo uliokuwa kwa siku za hivi karibuni, tokea Singida United irejee Ligi Kuu msimu huu, ambapo katika mtanange wa mzunguko wa kwanza uliofanyika Uwanja wa Jamhuri, Dodoma, timu hizo zilitoka sare ya bao 1-1.

 

YANGA KUVUNJA MWIKO? AU NDANDA KUENDELEZA UNDAVA?

LIGI Kuu ya Vodacom Tanzania Bara inatarajiwa kuendelea leo kwa mchezo mmoja tu, mabingwa watetezi, Yanga SC wakiwa wageni wa Ndanda FC Uwanja wa Nangwanda Sijaona mjini Mtwara.  

  Huo ni mchezo wa kiporo wa mzunguko wa 19, ambao Yanga ilishindwa kuucheza kutokana na kukabiliwa na mechi za Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Saint Louis Suns United ya Shelisheli.

  Na baada ya kuvuka Raundi ya Awali kwa ushindi wa jumla wa 2-1, ikishinda 1-0 nyumbani na sare ya 1-1 ugenini, Yanga inakuja kumalizia kiporo chake kabla ya kwenda kucheza mechi ya Raundi ya Kwanza ya Ligi ya Mabingwa dhidi ya Township Rollers ya Botswana.

  Lakini Yanga itateremka Uwanja wa Nangwanda jioni ya leo ikiwa kumbukumbu ya kutoshinda mechi nyumbani kwa Ndanda kati ya nne zilizotangulia, wakifungwa mbili na sare mbili.

  Kwa ujumla, katika Ligi Kuu Yanga imekutana na Ndanda mara nane tangu hiyo ipande msimu wa  2014/2015 – huku mabingwa hao watetezi, wakishinda mechi tatu, kufungwa mbili na sare tatu. 

  Yanga itajaribu kusaka ushindi wa kwanza leo Uwanja wa Nangwanda ikiwa inabakiliwa na wimbi la majeruhi na matatizo mengi ndani ya timu.

RAIS WA FIFA ALIVYOPOKELEWA NA NGOMA ZA ASILI KABLA YA KUFUNGUA MKUTANO

                        
Rais wa Shirikisho la Soka Duniani (FIFA), Gianni Infantino, amepokelewa na ngoma za kiasili kutoka kwa kabila la Wamasai, ambao walimbatana na zawadi mbalimbali za kiasili.

Infantino alipokea zawadi hizo leo mapema, kabla ya kufungua mkutano wa FIFA Excutive Summit, katika ukumbi wa JNICC jijini Dar es Salaam.

Infantino amewasili hapa akiwa na viongozi wengine mbalimbali, ikiwemo Rais wa CAF, Mr. Ahmad, kwa ajili ya mkutano wa mwaka wa FIFA unaoanza leo February 22.

Ujio wa Rais huyo ni maalum kwa ajili ya majadiliano kuhusu Soka la Wanawake, Vijana, Mipango ya kukuza soka kwa nchi za Afrika, pamoja na kusaidia vilabu kujiendeleza kisoka kiujumla.

Infantino ataondoka nchini mara tu baada ya mkutano huo kumalizika.

Tazama hapa namna alivyopokelewa na kabila la Wamasai waliombatanisha zawadi mbalimbali kwake.

ALLIANCE GIRLS:TUNAOMBA TFF WATAZAME RATIBA KWA UPANDE WETU
                         Image result for klabu ya alliance girls

Wawakilishi wa kanda ya ziwa kunako Ligi soka wanawake nchini Tanzania   kutoka jijini Mwanza Alliance Girls wamesema kuwa wamejipanga vilivyo kwenda kufanya kweli kunako  ligi soka ya wanawake hatua ya nane bora ambayo inatarajia kuanza kutimua vumbi tarehe 24 mwezi huu


Hayo yamesemwa na kocha wa klabu hiyo Ezekiel Chobanga wakatia akizungumza na michezo ya dodoma mapema leo Ambapo amesema wamejipanga kwenda kufanya vema katika mchezo wao wa kwanza jijini dar es salaam.


Amesema licha ya kutarajia kuanza kushiriki ligi hiyo lakini bado changamoto kubwa ambayo inawakabili ni Ratiba kuwabana kutoka na kushiriki mechi ya kwanza dar es salaam ,Mwanza na hatimaye ten Dodoma


Naye Nahodha wa timu hiyo ameelezea namna walivyojipanga yeye pamoja na wachezaji wenzake kuelekea nane bora ya ligi ya soka upande wa wanawake ambayo inatarajia kuanza mwezi wa pili tarehe 24 .


Kwa upande mwingine Amesema kuwa jamii wamekuwa wakitoa ushirikiano kwakuhakikisha watoto wa kike wanashiriki katika mchezo wa mpira wa miguu.


Na Selemani Juma Kodima


DOREFA DODOMA: LIGI YA MKOA WA DODOMA KUANZA FEBRUARY 23.
                          Image result for CHAMA CHA SOKA MKOANI DODOMA DOREFA
Ligi ya mkoa wa dodoma inatarajia kuanza kutimua vumbi siku ya ijumaa feb 24 baada ya ratiba ya ligi hiyo kutoka rasmi hapo jana ambapo mechi nne zitaanza kuchezwa katika viwanja vya ccm jamhuri na ccm mgambo wilayani mpwapwa.
Ratiba hiyo inaoneshwa kuwa Timu kutoka wilayan kondoa ambapo wapo kituo cha dodoma mjini watacheza saa nane kamili mchana dhidi ya timu ya Dom city kutoka zuzu hku jioni kukiwa na mchezo baina ya Derby ya Chamwino ya zamani Ila kwa sasa kila timu ipo kata yake ,Gwasa nato kutoka chang'ombe wakicheza na Sheli Fc matajiri kutoka chamwino katika mchezo wa jioni tarehe 23.
Wakati katika kituo cha Mpwapwa kutakuwa na michezo miwili ambayo itapingwa katika dimba la CCM mgambo kwa muda husika wa saa nane kwa mchezo wa kwanza na saa kumi kamili jioni kwa mchezo wa jioni.
Ligi ya mkoa wa dodoma ilitarajia kuanza  mwezi wa kwanza lakini kutoka na vilabu shiriki kushindwa kutekeleza kwa wakati vigezo vya chama cha soka dodoma Pamoja na Tff imepelekea kuchelewa kwa ligi hiyo.
Na Selemani Juma Kodima

                         Chelsea iligonga mwamba wa goli mara mbili huku Willian akitekeleza mashambulizi kutoka nje kabla ya raia huyo wa Brazil kufunga katika jaribio lake la tatu 

Mkufunzi Antonio Conte amesema kuwa Chelsea "itajaribu kufanya kitu cha kipekee'' na kuitoa Barcelona katika Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya baada ya sare 1-1 katika awamu ya kwanza

Willian aliiweka kifua mbele The Blues lakini Lionel Messi alisawazisha dakika 15 kabla ya mechi kukamilika baada ya makosa ya Andreas Christensen katika mechi ya kufuzu katika robo fainali ya kombe hilo.

Barcelona ambayo iko pointi saba mbele kileleni La Liga haikutekeleza mashambulizi yoyote makali hadi waliposawazisha.

''Tulikuwa tunakaribia kuwafunga," alisema mkufunzi huyo wa Chelsea. ''Tulifanya kosa moja, ni aibu na tumevunjwa moyo na matokeo''.

 

                  Image result for OKWI SIMBA SPORT

Simba imeibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Gendamarie na kusonga mbele katika michuano ya Kombe la Shirikisho kwa idadi ya mabao 5-0.

Katika mechi ya kwanza kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, Simba ilishinda kwa mabao 4-0.

Bao la leo la Simba lilifungwa na  Emmanuel Okwi, Simba ikiwa imekianza kipindi cha pili kwa kasi kubwa.

Mechi hiyo ilikwenda mapumziko kwa sare ya bila bao huku Gendamarie wakipoteza nafasi moja ya kufunga na Simba wakipoteza tatu ikiwemo ya Okwi aliyekuwa nahodha katika mchezo wa leo.

 

HATUA ya 16 Bora michuano ya Azam Sports Federation Cup (ASFC) inatarajiwa kuanza kesho

            Image result for azam sport federation cup

 HATUA ya 16 Bora michuano ya Azam Sports Federation Cup (ASFC) inatarajiwa kuanza kesho kwa mchezo mmoja tu kufanyika Uwanja wa Saba Saba mjini baina ya wenyeji, Njombe Mji FC na Mbao FC ya Mwanza,utakaoanza Saa 10:00.


Mechi nyingine za Kombe la Shirikisho la Azam zitaendelea Jumamosi Februari 24, wakati Singida United watakapowakaribisha Polisi Tanzania kwenye Uwanja wa Namfua saa 10 jioni na KMC watawaalika Azam FC saa 1 usiku Azam Complex

 
Jumapili Februari 25, 2018 Buseresere watakuwa uwanja wa Nyamagana Mwanza saa 8 mchana kucheza dhidi ya Mtibwa Sugar ya Morogoro, Majimaji FC ya Ruvuma watakuwa nyumbani kwenye uwanja wa Majimaji kuwakaribisha Young Africans ya Dar es Salaam saa 10 jioni wakati Ndanda FC watakuwa ugenini kucheza na JKT Tanzania saa 1 usiku Azam Complex Chamazi.


Jumatatu Februari 26, 2018 kutachezwa mechi mbili Kiluvya United dhidi ya Tanzania Prisons saa 8 mchana Uwanja wa Mabatini na Stand United watawaalika Dodoma FC saa 10 jioni uwanja wa Kambarage.

 

CONTE: NI NGUMU KUMZUIA MESSI

                      
Kocha wa Chelsea, Antonio Conte, ameweka wazi kuelekea mchezo wa kwanza katika hatua ya 16 bora dhidi ya FC. Barcelona katika UEFA Champions League utakuwa si rahisi.

Conte ameeleza kukutana na timu kama Barcelona ambayo ipo juu ya msimamo mwa Ligi huku ikiwa haijapoteza hata mchezo mmoja inabidi kazi ya ziada ifanyike.

Mbali na hilo ameongeza pia kwa kusema kuwa amekuwa anashindwa kupata usingizi kufikiria mbinu zipi na mipango gani ifanyike ili waweze kuizuia Barcelona leo huku akiongeza kwa kumtaja Messi kuwa ni ngumu kumzuia.

Mara ya mwisho Chelsea na Barcelona kukutana ilikuwa April 2012 ambapo Chelsea iliibuka na ushindi wa mabao 3-2 (On Aggregate).




======================================================

Kenya yamsaka kocha mpya wa Harambee Stars baada ya Paul Put kujiuzulu

                  Kenya inamsaka mkufunzi mpya wa timu yake ya taifa baada ya kocha Paul Put kujiuzulu miezi mitatu baada ya kuzinduliwa.

Kenya inamsaka mkufunzi mpya wa timu yake ya taifa baada ya kocha Paul Put kujiuzulu miezi mitatu baada ya kuzinduliwa.

Hii ilithibitishwa Jumatatu jioni na taarifa iliotolewa na shirikisho la soka nchini humo FKF kupitia meneja wa mawasiliano na uhusiano mwema Barry Otieno ambaye alielezea kwamba mkufunzi huyo alijiuzulu kutokana na matatizo ya kibinafsi huku Stanley Okumbi akichukua mahala pake kwa muda.

''Shirikisho la soka la Football Kenya lingependa kuwaambia mashabiki wa soka nchini Kenya kwamba bwana Pual Put amejiuzulu rasmi kama mkufunzi wa timu ya taifa kutokana na maswala ya kibinafsi.

''Hatahivyo kujiuzulu kwa kocha huyo ni pigo katika harakati za timu ya taifa kuelekea katika kufuzu mashindano ya AFCON 2019 kwa kuwa alikuwa kiungo muhimu cha timu''.




MBUNGE WA DODOMA MJINI AENDELEA KUHIMIZA MICHEZO ATOA JEZI KWA VILABU 

                     

Kuelekea mshikemshike wa ligi ya mkoa wa dodoma ngazi ya taifa, Naibu Waziri, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu, Anthony Mavunde ambaye pia Mbunge wa dodoma Mjini  Antony Mavunde katika kuongeza hamasa katika ligi hiyo leo amekabidhi jezi kwa vilabu vinavyoshiriki ligi hiyo kutoka manispaa ya dodoma.


Mh Mavunde amesema kuwa katika kuongeza hamasa katika mchezo wa mpira wa miguu imemfanya kushiriki kwa kutoa jezi kwa timu za manispaa ya dodoma kuelekea ligi ya mkoa ambayo inatarajia kuanza kutimua vumbi Feb 21 mwaka huu.


Aidha ametoa pongezi kwa timu ya AREA C  pamoja na Klabu ya DFC kwa juhudi zao katika medani ya soka kupitia ngazi za mashindano ambayo wameshiriki kwa msimu wa 2018/2019 .


Kwa upande wa vilabu ambavyo vimekabidhi jezi na mbunge huyo wametoa shukrani zao kupitia kwa moja ya viongozi wa timu ya sheli fc bw Mohamed abdalah  ambaye amesema  kuwa kutoka na uwepo changamoto hiyo ambayo mbunge ameitazama na kuwasaidia basi wamejipanga kulipa fadhila kwa  kuhakikisha ubingwa wa mkoa unabaki dodoma mjini



Na Selemani Juma Kodima



LIGI YA MKOA WA DODOMA INATALAJIWA KUANZA TAREHE 24 MWEZI WA PILI


Dodoma

Na ligi ya mkoa wa dodoma  inatarajia kuanza kutimua vumbi tarehe 24 mwezi wa pili mwaka huu kwa mfumo wa makundi mawili.

Hayo yamesemwa na katibu wa chama cha soka mkoani dodoma Dorefa Hamis kisoi wakati akielezea  ligi ya mkoa wa dodoma, na namna chama kimefikia hatua gani katika maandalizi ya ligi hiyo

Hamisi kisoi amesema kuwa kutokana na ligi hiyo kuwa na Muda mchache wamejipanga kuhakikisha wanaisimamia vizuri ili kupata bingwa ambaye ataweza kwenda kuwakilisha mkoa wa dodoma kunako mabingwa wa mikoa

Na Selemani Juma Kodima

KLABU YA SOKA YA WANAWAKE YA MKOA WA DODOMA BAOBAO FC IMEWAOMBA WAKAZI WA MKOA WA DODOMA KUENDELEA KUISAIDIA TIMU HIYO

                            

Klabu ya soka ya wanawake ya mkoa wa dodoma Baobao fc imewaomba wakazi wa mkoa wa dodoma kuendelea kuisupport timu  hiyo ambayo inashiriki ligi kuu hatua ya nane bora kwa mahitaji mbalimbali ikli iweze kufanya vema katika ligi hiyo

Hayo yamesemwa na mwenyekiti wa klabu hiyo Inocensi Massawe wakati akizungumza na sport bomba juu ya maandalizi yao na namna walivyojipanga katika kujianda na ligi hiyo ambayo inatarajia kuanza feb 24 mwaka ambapo baobao queen wanaanzia  nyumbani wakicheza na klabu ya mlandizi  ya mkoani pwani https://www.hulkshare.com/xsjmi4g7usqo

Na Selemani Juma Kodima

 



YAKUBU MOHAMMED ASEMA ATAENDELEZA MOTO KATIKA  MICHEZO YA LIGI



Na Dodoma Fm
BAADA ya kushinda tuzo Mchezaji Bora wa Mwezi Agosti wa Azam FC, beki Mghana Yakubu Mohammed amepania kufanya mambo makubwa zaidi kuisaidia timu hiyo.
Yakubu ametwaa tuzo hiyo inayojulikana kama ‘NMB Player of the Month’ ikidhaminiwa na wadhamini wakuu wa timu hiyo Benki ya NMB, na anakuwa mchezaji wa kwanza wa Azam FC kuitwaa ikiwa imeanzishwa msimu huu.
Kwa upande wa timu ya vijana ya Azam FC (Azam FC U-20) tuzo hiyo imekwenda kwa kiungo Twaha Ahmed, ambayo inadhaminiwa na wadhamini namba mbili wa timu hiyo Maji safi ya Uhai Drinking Water ikijulikana kama ‘Uhai Player of the Month’.
Tuzo hizo za kwanza za Azam FC, zilitolewa na mgeni rasmi kwenye mchezo wetu wa jana dhidi ya Lipuli, Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Wallace Karia.
Akizungumza jana mjini Dar es Salaam, Yakubu aliishukuru Azam FC kwa kuanzisha tuzo hiyo akidai inaongeza ushindani kikosini pamoja na kujenga wasifu wa wachezaji (CV).



MILIONI 47 KUIPANDISHA DARAJA TIMU YA AREA C


Na Dodoma Fm
Timu ya Soka ya  AREA C  ya mkoani dodoma ambayo itashiriki ligi daraja la pili katika msimu wa 2017/2018 imetoa shukrani kwa serikali ya mkoa wa dodoma  baada ya kuwa nao bega kwa bega katika hatua zote  za michezo yao ya ligi ya mabingwa wa mikoa  iliyomalizika hivi karibuni.
Pongezi hizo na shukrani zimetolewa na Uongozi wa  Timu ya Area C  walipokuta na Mkuu wa mkoa wa dodoma Mh Jordani Rugimbana pamoja na viongozi wengine wa mkoa ambapo wamekabidhi nishani ya shukrani kwa kila ambacho wamewasaidia  kuweza kupanda daraja .
Licha ya shukrani hizo ,timu hiyo imewasilisha bajeti yao kuu mbele ya mkuu  wa mkoa ambayo itawawezesha kufanikiwa kushiriki vema ligi daraja la pili  na hatimaye kupanda daraja la kwanza kuwa Millioni 47 na Elfu 90 .

Comments

Popular posts from this blog

MITI YA KIVULI MAARUFU KAMA PANGA UZAZI YAZUA TAHARUKI WILAYANI BAHI DODOMA

                                                  Mganga Mkuu wa Wilaya ya Bahi Jijini Dodoma Dk.Philipina Philipo amewatoa hofu wakazi   wa Wilaya hiyo juu ya taarifa za kuwepo kwa madhara katika miti ya kivuli maarufu kama PANGA UZAZI ambayo imezua hofu kwa wananchi hao. Hoja hiyo imeibuliwa katika kikao cha Baraza la Madiwani wa halmashauri hiyo ambapo baadhi ya madiwani wameomba kupatiwa ufafanuzi kuhusu kuwepo kwa fununu kuwa mti huo una madhara na kuongeza kuwa baadhi ya wananchi wameanza kuikata wakihofia kupatwa na madhara hayo. Akitoa ufafanuzi kuhusu miti hiyo Mganga Mkuu wa Wilaya Dk.Philipina Philipo amesema hadi hivi sasa hakuna utafiti wowote uliofanyika na kubainisha kuwa mti huo hauna madhara hivyo wananchi hawana haja ya kuhofia chochote. Kutokana na Majibu hayo ya DK PHILIPINA yamepelekea kuibua kwa hoja nyingine kwa madiwani ambapo baadhi yao wametoa maoni tofauti tofauti juu ya ufafanuzi huo. Kufuatia hayo katibu  tawala msaidizi mkoa anayesh

YANGA KESHO KUJUA ANACHEZA NA NANI KOMBE LA SHIRIKISHO AFRIKA

MAJINA ya vigogo wa soka Afrika, wakiwemo mabingwa wa Afrika 1998, Raja Casablanca yametawala katika orodha ya wapinzani wapya wa Yanga kwenye michuano ya Afrika. Yanga SC imeangukia kwenye kapu la kuwania kucheza hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika, ambako watamenyana na moja ya timu zilizofuzu hatua ya 16 Bora ya michuano hiyo. Hiyo ni baada ya kutolewa kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya sare ya 0-0 na wenyeji, Township Rollers Jumamosi jioni Uwanja wa Taifa mjini Gaborone nchini Botswana. Matokeo hayo yanamaanisha Rollers inakwenda hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa kwa mara ya kwanza historia hiyo kwa ushindi wa jumla wa 2-1 uliotokana na matokeo ya mchezo wa                              kwanza Dar es Salaam Machi 6. Na Yanga SC itamenyana na moja ya timu zilizofuzu hatua ya 16 Bora ya michuano hiyo, ambazo ni CR Belouizdad, USM Alger za Algeria, Al-Masry ya Misri, Djoliba ya Mali, Raja Casablanca, Enyimba ya Nigeria, SuperSport United ya Afrika K

MIKOA INAYOONGOZA KWA UKEKETAJI TANZANIA YATAJWA

Mila potofu   katika jamii ya kimasai imetajwa kuwa changamoto kwa maafisa ustawi wa jamii wa halimashauri ya wilaya ya Ngorongoro  kutokana na kukosa ushirikiano wa kutatua Tatizo la ukeketaji kwa jamii hiyo. Akizungumza na waandishi ya habari Afisa Ustawi Wa jamii Bwana ALOYCE  LOLIKISWALI katika semina iliyoandaliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu Sanyansi na Utamaduni UNESCO kwa lengo la kupinga ukeketaji wa wanawake amesema kukosekana kwa ushirikiano kwa jamii imekuwa ni changamoto ambayo imepelekea kushindwa kudhibiti ukeketaji pamoja na ukatili wa kijinsia. Kwa upande wake Mwenyekiti wa Malaigwanan Bwana JOSEPH TIRIPAI amebainisha kuwa mila na desturi zao zitabadilika kulingana na wakati lakini watahakikisha wanalinda watoto wanaozaliwa kutokeketwa na kusisitiza elimu kuendelea kutolewa hususani shuleni. Katika hatua nyingine mratibu wa afya ya mama na mtoto ameeleza kuwa wanawake wajawazito waliokeketwa wanalazimika   kujifugua kwa upasuaji na