Skip to main content

Conte: Tutailaza Barcelona mechi ya marudio Ligi ya Mabingwa Ulaya UEFA

                         Chelsea iligonga mwamba wa goli mara mbili huku Willian akitekeleza mashambulizi kutoka nje kabla ya raia huyo wa Brazil kufunga katika jaribio lake la tatu 

Mkufunzi Antonio Conte amesema kuwa Chelsea "itajaribu kufanya kitu cha kipekee'' na kuitoa Barcelona katika Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya baada ya sare 1-1 katika awamu ya kwanza

Willian aliiweka kifua mbele The Blues lakini Lionel Messi alisawazisha dakika 15 kabla ya mechi kukamilika baada ya makosa ya Andreas Christensen katika mechi ya kufuzu katika robo fainali ya kombe hilo.

Barcelona ambayo iko pointi saba mbele kileleni La Liga haikutekeleza mashambulizi yoyote makali hadi waliposawazisha.

''Tulikuwa tunakaribia kuwafunga," alisema mkufunzi huyo wa Chelsea. ''Tulifanya kosa moja, ni aibu na tumevunjwa moyo na matokeo''.

Comments

Popular posts from this blog

MITI YA KIVULI MAARUFU KAMA PANGA UZAZI YAZUA TAHARUKI WILAYANI BAHI DODOMA

                                                  Mganga Mkuu wa Wilaya ya Bahi Jijini Dodoma Dk.Philipina Philipo amewatoa hofu wakazi   wa Wilaya hiyo juu ya taarifa za kuwepo kwa madhara katika miti ya kivuli maarufu kama PANGA UZAZI ambayo imezua hofu kwa wananchi hao. Hoja hiyo imeibuliwa katika kikao cha Baraza la Madiwani wa halmashauri hiyo ambapo baadhi ya madiwani wameomba kupatiwa ufafanuzi kuhusu kuwepo kwa fununu kuwa mti huo una madhara na kuongeza kuwa baadhi ya wananchi wameanza kuikata wakihofia kupatwa na madhara hayo. Akitoa ufafanuzi kuhusu miti hiyo Mganga Mkuu wa Wilaya Dk.Philipina Philipo amesema hadi hivi sasa hakuna utafiti wowote uliofanyika na kubainisha kuwa mti huo hauna madhara hivyo wananchi hawana haja ya kuhofia chochote. Kutokana na Majibu hayo ya DK PHILIPINA yamepelekea kuibua kwa hoja nyingine kwa madiwani ambapo baadhi yao wametoa maoni tofauti tofauti juu ya ufafanuzi huo. Kufuatia hayo katibu  tawala msaidizi mkoa anayesh

MIKOA INAYOONGOZA KWA UKEKETAJI TANZANIA YATAJWA

Mila potofu   katika jamii ya kimasai imetajwa kuwa changamoto kwa maafisa ustawi wa jamii wa halimashauri ya wilaya ya Ngorongoro  kutokana na kukosa ushirikiano wa kutatua Tatizo la ukeketaji kwa jamii hiyo. Akizungumza na waandishi ya habari Afisa Ustawi Wa jamii Bwana ALOYCE  LOLIKISWALI katika semina iliyoandaliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu Sanyansi na Utamaduni UNESCO kwa lengo la kupinga ukeketaji wa wanawake amesema kukosekana kwa ushirikiano kwa jamii imekuwa ni changamoto ambayo imepelekea kushindwa kudhibiti ukeketaji pamoja na ukatili wa kijinsia. Kwa upande wake Mwenyekiti wa Malaigwanan Bwana JOSEPH TIRIPAI amebainisha kuwa mila na desturi zao zitabadilika kulingana na wakati lakini watahakikisha wanalinda watoto wanaozaliwa kutokeketwa na kusisitiza elimu kuendelea kutolewa hususani shuleni. Katika hatua nyingine mratibu wa afya ya mama na mtoto ameeleza kuwa wanawake wajawazito waliokeketwa wanalazimika   kujifugua kwa upasuaji na

SERIKALI IMEANZA KUANDAA KITINI CHA MASUALA YA JINSIA

                                             Serikali imeanza mchakato wa kuandaa kitini cha masuala ya jinsia kuendeleza kasi ya utekelezaji wa mpango wa kitaifa wa kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto. Akizungumza katika kikao cha wataalam na wadau wa maendeleo ya Jinsia Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Jinsia Bi. Mboni Mgaza amesema Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto umekithiri sana nchini   hivyo Serikali kuamua kutafuta njia tofauti za kupambana na tatizo hilo. Amesema   lengo la kuandaa kitini cha kufundishia masuala ya Jinsia “ni kwa ajili ya utekelezaji wa Mpango Kazi wa Kitaifa wa kutokomeza Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto ambao utatoa uelewa kwa wadau wa maswala ya jinsia na maafisa Maendeleo ya Jamii kuanzia ngazi ya Mkoa, Halmashauri na kata ili kutoa elimu ya masuala ya Jinsia katika jamii. Bi. Mboni amefafanua kuwa kwa mujibu wa takwimu ya Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2012 idadi ya wanawake nchini ilikuwa ni Milioni Is