
Wilaya 93 nchini
zilizokuwa zinahitaji kinga tiba kwa ajili ya magojwa zimefanikiwa kutokomeza magojwa yaliyokuwa
hayapewi kipaumbele yakiwemo ya mabusha pamoja na matende.
Katibu mkuu Wizara
ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Mpoki Ulisubisya ameyasema
hayo katika uzinduzi wa mkutano wa kujadili, kupata na kupanga utekelezaji wa
mpango kazi katika kutokomeza magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele.
Dk. Mpoki amesema
serikali kupitia Wizara ya Afya imetoa dawa kwa watanzania wapatao milioni 21
kati ya milioni 50 na kupiga hatua kubwa katika kudhibiti magonjwa hayo hapa
nchini.
Amesema mkutano huo
umelenga kukutanisha wadau wa afya wa ndani na nje ya nchi wenye lengo la
kutoka na mikakati ya kupambana na magojwa hayo hasa katika maeneo ya vijijini.
Nae Mratibu wa
Taifa wa mpango wa kutokomeza magojwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele nchini
Dkt. Upendo Mwingira amesema wananchi wanatakiwa kujitokeza katika mazoezi ya
kupata dawa za kuzuia mabusha pamoja na matende pindi serikali itakapotangaza
zoezi la utoaji wa dawa hizo.
Sambamba na hayo
Mwingira amesema katika kuhakikisha magonjwa hayo yanapotea nchini wamejitahidi
kuzindua kampeni ya kuwafanyia upasuaji watu wapatao 350 kisarawe Mkoani Pwani.
Na
Phina Nimrod DODOMA
FM
Comments
Post a Comment