
Waziri wa afya maendeleo ya jamii jinsia wazee na watoto Mh.
Ummy Mwalimu amewataka wazazi na walezi nchini kutokuwaficha watoto waliozaliwa
wakiwa na mapungufu katika miili yao badala yake wawafikishe hospitalini kwa
matibabu zaidi.
Waziri Ummy ametoa rai hiyo
ikiwa ni siku chache baada ya kufariki Dunia kwa mapacha walioungana Maria
pamoja na Consolata huko Mkoani Iringa huku kukiwa na taarifa za kuzaliwa kwa watoto
wengine walioungana huko Mkoni Kagera swala ambao limeibuka leo katika vikao
vya Bunge jijini Dodoma.
Amesema Serikali kupitia wizara ya afya inayo taarifa ya
kuzaliwa kwa watoto mapacha walio ungana na maelekezo yamekwisha kutolewa kwa
mganga mkuu wa Serikali pamoja na mganga mkuu wa Mkoa wa Kagera ili kuhakikisha
watoto hao wanafikishwa katika Hospitali ya Mhimbili ili kufanyiwa taratibu za
kuwatenganisha.
Na Pius Jayunga Bunge/Dodoma FM
Comments
Post a Comment