Imeelezwa kuwa suala la unyanyasaji
kwa watoto hususani wanafunzi mkoani Dodoma linachangiwa na baadhi ya wazazi na
walezi kutokuwa karibu na watoto hali inayowafanya watoto kujikuta wakiingia
katika makundi yasiyo salama .
Hayo yamebainishwa leo na afisa
elimu wa shule za msingi kutoka halmashauri ya jiji la Dodoma Mwisungu Kigosi
wakati akiongea katika kikao na walimu wakuu wa shule mbalimbali za mkoa wa
Dodoma kilicholenga kujadili suala la malezi kwa wanafunzi.
Afisa Elimu huyo amesema kuwa Wazazi na walezi mjini
Dodoma wanatakiwa kuwa karibu kwa kufuatilia mienendo ya watoto wao pindi
wawapo shuleni ili kuwaepusha na vishawishi mbalimbali wanavyokutana navyo
wakati wa masomo yao hali itakayosaidia kupunguza vitendo vya unyanyasaji.
Aidha amewataka walimu kufanya kazi
kwa ushirikiano na wazazi ikiwemo
kuitisha mikutano ya mara kwa mara ili kuwapa taarifa juu ya mienendo ya watoto
wao kwani wanaopaswa kutoa taarifa hizo kwa wazazi na walezi ni walimu wenyewe.
kwa upande wao baadhi ya walimu
walioshiriki kikao hicho wamekiri kuwepo kwa baadhi ya walimu wasiowajibika
kikamilifu ambapo wamesema kuwa umefika wakati sasa wa kuhakikisha wanatekeleza
majukumu yao ipasavyo ikiwemo kuvaa majukumu ya uzazi na sio kuwaachia wazazi
pekee jukumu la kutoa malezi bora.
NA ALFRED BULAHYA DODOMA
FM
Comments
Post a Comment