
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli ametuma salamu
za rambirambi kwa familia, ndugu, jamaa na marafiki kufuatia vifo vya watu 10
vilivyosababishwa na ajali ya basi la abiria kugongana na treni ya mizigo Mjini
Kigoma.
Ajali
hiyo imetokea leo tarehe 06 Juni, 2018 majira ya saa 12:15 asubuhi katika eneo
la Gungu Mjini Kigoma wakati basi la abiria la kampuni ya Prince Hamida lililokuwa
linatoka Kigoma Mjini kwenda Tabora lilipoigonga treni ya mizigo iliyokuwa ikitoka
Kazuramimba kwenda Kigoma Mjini.
Mhe.
Rais Magufuli amemtaka Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Brig. Jen. Mstaafu Emanuel
Maganga kufikisha salamu hizo kwa wafiwa wote, na amewaombea kuwa na moyo wa subira,
uvumilivu na ustahimilivu katika kipindi hiki kigumu cha majonzi ya kuondokewa na
wapendwa wao.
Mapema asubuhi leo kamanda wa Polisi mkoani Kigoma Martin Otieno
amethibitisha kutokea kwa ajili hiyo ambayo Watu 10 wamefariki papo hapo na
wengine 27 kujeruhiwa.
Kamanda wa polisi amesema, basi hilo lilitupwa mita 100 kutoka
kwenye eneo la ajali na kueleza kuwa waokoaji wamewatoa watu walionaswa kwenye
mabaki ya basi hilo, na huenda idadi ya watu waliofariki ikaongezeka.
Na Zania Miraji Chanzo:Ikulu /DODOMA FM
Comments
Post a Comment