Skip to main content

WANANCHI WATAKIWA KUKAA MBALI NA SIMU /KOMPUTA KUEPUKA KUUMWA MACHO


            
Image result for MAGONJWA YA MACHO





Wananchi wanaotumia simu na Komputer kwa muda mrefu wameshauriwa kukaa umbali wa sentimita 25 kutoka macho yalipo mpaka katika vifaa hivyo ili kuepuka magonjwa ya Macho.

Ushauri huo umetolewa na Daktari bingwa wa macho kutoka Hospitali ya Charity Vision Tanzania iliyopo Jijini Dodoma Dokta EDMUND MUSHUMBUSI  wakati akizungumza na Dodoma FM.

Dr Mushumbusi  amesema ili kuepuka matatizo yatokanayo na matumizi ya muda mrefu ya vifaa hivyo kama maumivu ya kichwa ni vyema mtu akaweka umbali wa sentimita 25 pamoja na kupumzika kila baada ya muda ili kuyapumzisha macho.

Akizungumzia shida anayoweza kuipata mtu anayetumia vifaa hivyo kwa muda mrefu ni maumivu ya kichwa,kuchoka au kuuma kwa macho, kutokuona vizuri pamoja na maumivu ya shingo na mgongo.

Amesema kama ilivyo kawaida ya kupumzisha viungo vingine vya mwili macho pia yana takiwa kupumzika kutokana na kuwa na umuhimu mkubwa kwa binadamu.

Na Phinna Nimrod                                                     DODOMA FM

Comments

  1. This is exactly what I was looking for. Thanks for sharing this great article! That is very interesting Smile I love reading and I am always searching for informative. you can cheak this W3fmradio

    ReplyDelete
  2. Latest platform for web marketing and search engine marketing (SEM) and (SEO) tool. This tool provides a complete SEO skill. The mostly person uses search engine marketing for online marketing. this totally depends on latest trends in search engine marketing.

    ReplyDelete

Post a Comment

Popular posts from this blog

WAJAWAZITO WASHAURIWA KUTUMIA VIDONGE VYA FOLIC ACID KUEPUKA WATOTO VILEMA

                                                                  Mama wajawazito wameshuriwa kutumia dawa aina ya FOLIC ACID katika kipindi cha miezi mitatu ya mwanzo ya ujauzito ili kuepuka kupata mtoto mwenye   mapungufu. Rai hiyo imetolewa na Daktari kutoka Hospitali ya Matovyolwa mjini Dodoma   Dk.MUBARACK ISSA ALI wakati akizungumza na Dodoma FM juu ya athari zitokanazo na mama kutotumia dawa hizo. Dr Mubarack amesema katika kipindi cha ujauzito mama huwa anapitia changamoto nyingi hivyo ni vyema akatumia dawa aina ya FOLIC ACID ili kuepuka kupata mtoto mwenye tatizo la mgongo wazi, kichwa kikubwa pamoja na upungufu wa damu. Aidha Dk. Mubarack amesema   ili kuepuka kupata mtoto njiti   kipofu na kusababisha kifo kwa mtoto   ni vyema mama akaepuka matumizi ya pombe, dawa za kulev...

MIKOA INAYOONGOZA KWA UKEKETAJI TANZANIA YATAJWA

Mila potofu   katika jamii ya kimasai imetajwa kuwa changamoto kwa maafisa ustawi wa jamii wa halimashauri ya wilaya ya Ngorongoro  kutokana na kukosa ushirikiano wa kutatua Tatizo la ukeketaji kwa jamii hiyo. Akizungumza na waandishi ya habari Afisa Ustawi Wa jamii Bwana ALOYCE  LOLIKISWALI katika semina iliyoandaliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu Sanyansi na Utamaduni UNESCO kwa lengo la kupinga ukeketaji wa wanawake amesema kukosekana kwa ushirikiano kwa jamii imekuwa ni changamoto ambayo imepelekea kushindwa kudhibiti ukeketaji pamoja na ukatili wa kijinsia. Kwa upande wake Mwenyekiti wa Malaigwanan Bwana JOSEPH TIRIPAI amebainisha kuwa mila na desturi zao zitabadilika kulingana na wakati lakini watahakikisha wanalinda watoto wanaozaliwa kutokeketwa na kusisitiza elimu kuendelea kutolewa hususani shuleni. Katika hatua nyingine mratibu wa afya ya mama na mtoto ameeleza kuwa wanawake wajawazito waliokeketwa wanalazimika   kujifug...

MITI YA KIVULI MAARUFU KAMA PANGA UZAZI YAZUA TAHARUKI WILAYANI BAHI DODOMA

                                                  Mganga Mkuu wa Wilaya ya Bahi Jijini Dodoma Dk.Philipina Philipo amewatoa hofu wakazi   wa Wilaya hiyo juu ya taarifa za kuwepo kwa madhara katika miti ya kivuli maarufu kama PANGA UZAZI ambayo imezua hofu kwa wananchi hao. Hoja hiyo imeibuliwa katika kikao cha Baraza la Madiwani wa halmashauri hiyo ambapo baadhi ya madiwani wameomba kupatiwa ufafanuzi kuhusu kuwepo kwa fununu kuwa mti huo una madhara na kuongeza kuwa baadhi ya wananchi wameanza kuikata wakihofia kupatwa na madhara hayo. Akitoa ufafanuzi kuhusu miti hiyo Mganga Mkuu wa Wilaya Dk.Philipina Philipo amesema hadi hivi sasa hakuna utafiti wowote uliofanyika na kubainisha kuwa mti huo hauna madhara hivyo wananchi hawana haja ya kuhofia chochote. Kutokana na Majibu hayo ya DK PHILIPINA yamepelekea kuibua kwa hoja nyingine kwa madi...