Skip to main content

WANANCHI WASHAURIWA KUFUATA KANUNI ZA UNUNUZI WA ARDHI


Image result for ARDHI
       





Jamii imetakiwa kufuata taratibu za kisheria katika ununuzi wa ardhi ili kuepuka migogoro ya ardhi inayojitokeza mara nyingi miongoni mwa familia.

Rai hiyo imetolewa na Mwanasheria wa Kujitegemea Bwana Goodluck Ludala ambapo amesema migororo mingi ya ardhi inatokana na watu kutokufuata taratibu za kisheria za manunuzi ambapo inaweza kupelekea mtu kupoteza haki yake .

Amesema iwapo mtu atapata migogoro ya ardhi anatakiwa kupeleka shauri lake baraza la kata na baada ya uamuzi kutoka mlalamikaji anapaswa kukaza hukumu katika baraza la ardhi la wilaya jambo ambalo watu wengi huwa hawafanyi na kupoteza haki zao.

Aidha amesema kumekuwa na baadhi ya watu wanaopuuza hukumu ya mahakama pasipo kukata rufaa ambapo ameeleza kuwa kufanya hivyo ni kosa kisheria na hapo mlalamikaji anapaswa kutoa taarifa katika mahakama iliyotoa hukumu ili hatua zaidi zichukuliwe.

Haya Yamejiri ikiwa ni siku chache baada ya Dodoma FM  kupokea kisa cha migogoro ya ardhi katika familia ambako kulionekana kuwa na tatizo la  kupuuza amri ya mahakama.


Mariam Matundu                                                         DODOMA FM

Comments

  1. Crytpcurrency ethereum to bank account live instant conversion with 0% fee from the worlds most trusted website. You can sell your ether coin to receive money into your bank account in form of local cash. (:O:) feel blessed

    ReplyDelete
  2. Latest platform for web marketing and search engine marketing (SEM) and (SEO) tool. This tool provides a complete SEO skill. The mostly person uses search engine marketing for online marketing. this totally depends on latest trends in search engine marketing.

    ReplyDelete

Post a Comment

Popular posts from this blog

WAJAWAZITO WASHAURIWA KUTUMIA VIDONGE VYA FOLIC ACID KUEPUKA WATOTO VILEMA

                                                                  Mama wajawazito wameshuriwa kutumia dawa aina ya FOLIC ACID katika kipindi cha miezi mitatu ya mwanzo ya ujauzito ili kuepuka kupata mtoto mwenye   mapungufu. Rai hiyo imetolewa na Daktari kutoka Hospitali ya Matovyolwa mjini Dodoma   Dk.MUBARACK ISSA ALI wakati akizungumza na Dodoma FM juu ya athari zitokanazo na mama kutotumia dawa hizo. Dr Mubarack amesema katika kipindi cha ujauzito mama huwa anapitia changamoto nyingi hivyo ni vyema akatumia dawa aina ya FOLIC ACID ili kuepuka kupata mtoto mwenye tatizo la mgongo wazi, kichwa kikubwa pamoja na upungufu wa damu. Aidha Dk. Mubarack amesema   ili kuepuka kupata mtoto njiti   kipofu na kusababisha kifo kwa mtoto   ni vyema mama akaepuka matumizi ya pombe, dawa za kulev...

MIKOA INAYOONGOZA KWA UKEKETAJI TANZANIA YATAJWA

Mila potofu   katika jamii ya kimasai imetajwa kuwa changamoto kwa maafisa ustawi wa jamii wa halimashauri ya wilaya ya Ngorongoro  kutokana na kukosa ushirikiano wa kutatua Tatizo la ukeketaji kwa jamii hiyo. Akizungumza na waandishi ya habari Afisa Ustawi Wa jamii Bwana ALOYCE  LOLIKISWALI katika semina iliyoandaliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu Sanyansi na Utamaduni UNESCO kwa lengo la kupinga ukeketaji wa wanawake amesema kukosekana kwa ushirikiano kwa jamii imekuwa ni changamoto ambayo imepelekea kushindwa kudhibiti ukeketaji pamoja na ukatili wa kijinsia. Kwa upande wake Mwenyekiti wa Malaigwanan Bwana JOSEPH TIRIPAI amebainisha kuwa mila na desturi zao zitabadilika kulingana na wakati lakini watahakikisha wanalinda watoto wanaozaliwa kutokeketwa na kusisitiza elimu kuendelea kutolewa hususani shuleni. Katika hatua nyingine mratibu wa afya ya mama na mtoto ameeleza kuwa wanawake wajawazito waliokeketwa wanalazimika   kujifug...

MITI YA KIVULI MAARUFU KAMA PANGA UZAZI YAZUA TAHARUKI WILAYANI BAHI DODOMA

                                                  Mganga Mkuu wa Wilaya ya Bahi Jijini Dodoma Dk.Philipina Philipo amewatoa hofu wakazi   wa Wilaya hiyo juu ya taarifa za kuwepo kwa madhara katika miti ya kivuli maarufu kama PANGA UZAZI ambayo imezua hofu kwa wananchi hao. Hoja hiyo imeibuliwa katika kikao cha Baraza la Madiwani wa halmashauri hiyo ambapo baadhi ya madiwani wameomba kupatiwa ufafanuzi kuhusu kuwepo kwa fununu kuwa mti huo una madhara na kuongeza kuwa baadhi ya wananchi wameanza kuikata wakihofia kupatwa na madhara hayo. Akitoa ufafanuzi kuhusu miti hiyo Mganga Mkuu wa Wilaya Dk.Philipina Philipo amesema hadi hivi sasa hakuna utafiti wowote uliofanyika na kubainisha kuwa mti huo hauna madhara hivyo wananchi hawana haja ya kuhofia chochote. Kutokana na Majibu hayo ya DK PHILIPINA yamepelekea kuibua kwa hoja nyingine kwa madi...