Skip to main content

WAKAZI KIJIJI CHA CHIKOPELO DODOMA WASUBIRI MILIONI 50 ZA KILA KIJIJI


Image result for MAMILIONI YA PESA



Serikali kuchelewa kutoa milioni 50 katika vikundi ndani ya kila kijiji na mtaa kumechangia baadhi ya vikundi ambavyo tayari vilikuwa vimeundwa kusambaratika.

Wakizungumza na Dodoma fm baadhi ya vijana wa kijiji cha chikopelo wilaya ya Bahi katika mkoa wa dodoma wamesema kuwa yapata zaidi ya miaka miwili ahadi ya serikali ya awamu ya tano bado haijatimia ya kuwagawia hizo million 50 jambo linalochangia baadhi ya vikundi vilivyokuwa vimeundwa kuanza kusambaratika kwa kukosa uhakika wa hiyo fedha.

Vijana hao wamesema kuwa awali   baada ya kuunda vikundi hivyo walianza kuchangishana pesa na kukutana mara kwa mara kwa ajili ya kuimarika huku wakisubiri hiyo fedha kutoka serikalini lakini baadaye washirika walianza kutohudhuria na mwisho kusambaratika baada ya kusubiri kwa muda mrefu.

Aidha akitolea ufafanuzi juu wa uwepo wa vikundi vilivyokwisha sambatratika katika kijiji hicho mwenyekiti wa kijiji cha chikopelo Bwana CORNELIUS MAHINYILA amekanusha taarifa hizo na kusema kuwa vikundi bado viko imara huku vikiendelea kusubiri kutimia kwa ahadi hiyo ya kupokea milioni 50.

Mnamo mwaka 2015 serikali iliyoko madarakani ikiomba lidhaa kwa wananchi ya kuongoza nchi kupitia ilani ya chama cha mapinduzi (CCM) ilitamka kuwa itatoa shilingi milioni 50 kwa vikundi katika kila kijiji na mtaa fedha ambayo itasaidia mwananchi kujikwamua kiuchumi na kumletea maendeleo.

Hata hivyo serikali kupitia kwa waziri wa fedha na mipango, Dk PHILIP MPANGO imesema ahadi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ya kutoa Shilingi milioni 50 kila kijiji na mtaa itaanza kutekelezwa mara baada ya mfumo wa kuanza kuzitoa utakapokamilika na kuwakumbusha wananchi kuwa hiyo ni ahadi ya chama kwa kipindi cha miaka mitano.

Na RWEIKIZA  KATEBALIRWE                                 DODOMA FM

Comments

Popular posts from this blog

WAJAWAZITO WASHAURIWA KUTUMIA VIDONGE VYA FOLIC ACID KUEPUKA WATOTO VILEMA

                                                                  Mama wajawazito wameshuriwa kutumia dawa aina ya FOLIC ACID katika kipindi cha miezi mitatu ya mwanzo ya ujauzito ili kuepuka kupata mtoto mwenye   mapungufu. Rai hiyo imetolewa na Daktari kutoka Hospitali ya Matovyolwa mjini Dodoma   Dk.MUBARACK ISSA ALI wakati akizungumza na Dodoma FM juu ya athari zitokanazo na mama kutotumia dawa hizo. Dr Mubarack amesema katika kipindi cha ujauzito mama huwa anapitia changamoto nyingi hivyo ni vyema akatumia dawa aina ya FOLIC ACID ili kuepuka kupata mtoto mwenye tatizo la mgongo wazi, kichwa kikubwa pamoja na upungufu wa damu. Aidha Dk. Mubarack amesema   ili kuepuka kupata mtoto njiti   kipofu na kusababisha kifo kwa mtoto   ni vyema mama akaepuka matumizi ya pombe, dawa za kulev...

MIKOA INAYOONGOZA KWA UKEKETAJI TANZANIA YATAJWA

Mila potofu   katika jamii ya kimasai imetajwa kuwa changamoto kwa maafisa ustawi wa jamii wa halimashauri ya wilaya ya Ngorongoro  kutokana na kukosa ushirikiano wa kutatua Tatizo la ukeketaji kwa jamii hiyo. Akizungumza na waandishi ya habari Afisa Ustawi Wa jamii Bwana ALOYCE  LOLIKISWALI katika semina iliyoandaliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu Sanyansi na Utamaduni UNESCO kwa lengo la kupinga ukeketaji wa wanawake amesema kukosekana kwa ushirikiano kwa jamii imekuwa ni changamoto ambayo imepelekea kushindwa kudhibiti ukeketaji pamoja na ukatili wa kijinsia. Kwa upande wake Mwenyekiti wa Malaigwanan Bwana JOSEPH TIRIPAI amebainisha kuwa mila na desturi zao zitabadilika kulingana na wakati lakini watahakikisha wanalinda watoto wanaozaliwa kutokeketwa na kusisitiza elimu kuendelea kutolewa hususani shuleni. Katika hatua nyingine mratibu wa afya ya mama na mtoto ameeleza kuwa wanawake wajawazito waliokeketwa wanalazimika   kujifug...

MITI YA KIVULI MAARUFU KAMA PANGA UZAZI YAZUA TAHARUKI WILAYANI BAHI DODOMA

                                                  Mganga Mkuu wa Wilaya ya Bahi Jijini Dodoma Dk.Philipina Philipo amewatoa hofu wakazi   wa Wilaya hiyo juu ya taarifa za kuwepo kwa madhara katika miti ya kivuli maarufu kama PANGA UZAZI ambayo imezua hofu kwa wananchi hao. Hoja hiyo imeibuliwa katika kikao cha Baraza la Madiwani wa halmashauri hiyo ambapo baadhi ya madiwani wameomba kupatiwa ufafanuzi kuhusu kuwepo kwa fununu kuwa mti huo una madhara na kuongeza kuwa baadhi ya wananchi wameanza kuikata wakihofia kupatwa na madhara hayo. Akitoa ufafanuzi kuhusu miti hiyo Mganga Mkuu wa Wilaya Dk.Philipina Philipo amesema hadi hivi sasa hakuna utafiti wowote uliofanyika na kubainisha kuwa mti huo hauna madhara hivyo wananchi hawana haja ya kuhofia chochote. Kutokana na Majibu hayo ya DK PHILIPINA yamepelekea kuibua kwa hoja nyingine kwa madi...