Naibu mstahiki meya
wa jiji la Dodoma amewataka wadau wa nishati mbadala
kutembelea vijijni ili kuwafikia wananchi kutoa elimu juu ya matumizi ya nyenzo nyingine za kupata nishati mbadala.
Bwana JUMANNE NGEDE amesema
hayo wakati akikagua mabanda ya wadau wa kutoa elimu juu ya utumiaji nishati
mbadala katika kilele cha maadhimisho ya wiki ya mazingira yaliyofanyika Kimkoa katika
viwanja vya mwalimu nyerere jijini Dodoma .
Amesema ni vema
kila mtu akawa mlinzi wa mwenzake kwa kuhakikisha Dodoma inakuwa safi ikiwemo
kutotupa taka hovyo na kuwa atakayekiuka na kukamatwa atachukuliwa hatua za
kisheria ikiwemo faini au kifungo.
Akisoma Risala
mbele ya mgeni rasmi afisa mazingira wa jiji la Dodoma bwana ALLY MFINANGA amesema uharibifu wa mazingira umesababisha kuzorota kwa shughuri za kiuchumi
na kurudisha nyuma maendeleo ya jiji hilo.
Aidha akizungumza
kwa niaba ya wadau wa nishati mbadala katika maadhimisho hayo Afisa utawala wa
ACO-ACT PROJECT Bi BENEDICTA KIMBE amehaidi kufanyia kazi yote waliyojifunza na
kuagizwa ili kuhakikisha wanatokomeza swala la uharibifu wa mazingira.
Maadhimisho ya wiki
ya mazingira duniani hufanyika kila ifikapo june 5 kila mwaka na mwaka huu Kitaifa yamefanyika jiji Dar-es-salaam huku yakiwa yamebeba kaulimbiu isemayo
mkaa ni gharama tumia njia mbadala na Tupambane kutokomeza taka zitokanazo na
plastiki ikiwa ni kauli mbiu ya kimataifa.
NaRWEIKIZAKATEBALIRWE DODOMA F
The Best Slot Machines - The JTM Hub
ReplyDeleteThe 서산 출장샵 Best Slot 부천 출장마사지 Machines - The JTM 화성 출장마사지 Hub The Best Slot Machines If 울산광역 출장안마 you 경기도 출장안마 want to learn more about this game in our online slot machine guides.