Wadau wanaoshughulika na udhibiti wa uharibifu wa mazingira nchini wametakiwa kutumia Takwimu
zinazozotolewa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu
kuishauri Serikali kupambana na matumizi ya mkaa kutokana na kuonekana
kuwa chanzo kikubwa cha uharibifu wa mazingira.
Akiongea na Dodoma
Fm Mtakwimu kutoka Ofisi ya Taifa ya TAKWIMU Bw. GODBLESS WILLIAM amesema
utafiti uliofanyika mwaka 2016 unaonesha asilimila kubwa ya Watanzania
wanatumia mkaa ambapo mkoa wa Dar es salaam unaongoza kwa
asilimia 88 huku Dodoma ikiwa na asilimia 21.
Bw. GODBLESS
amesema kwa upande wa matumizi ya kuni Takwimu zinaonesha Lindi ikiongoza kwa
asilimia 90 ikifuatiwa na Dodoma yenye asilimia 86. 7 na kwamba misitu imekuwa
ikivamiwa kwa asilimia kubwa na wananchi kwa ukataji wa miti kwa ajili ya kuni
pamoja na mkaa.
Amesema lengo la
Ofisi ya Taifa ya Takwimu ni kuishauri serikali pamoja na wadau wanaopambana na
uharibufu wa mazingira kufuatilia takwimu zinazotolewa na kuangalia uwezekano wa kutokomeza uharibifu wa mazingira.
Ili kupata
ufafanuzi zaidi juu ya Takwimu za uharibifu wa Mazingira wananchi wa Dodoma
wametakiwa kufika katika Ofisi ya Taifa ya Takwimu zilizopo Hazina.
Na
Phina Nimrod DODOMA FM
Comments
Post a Comment