Tawala
za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) kwa kushirikiana na Mradi wa
Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3) wanatoa mafunzo ya kina ya wiki
tatu kwa watumishi wa kada ya uhasibu
kutoka mamlaka 185 za Serikali za Mitaa
Tanzania.
Akifungua
mafunzo hayo yanayohusu mfumo mpya wa Epicor 10.2, leo Jijini
Dodoma Katibu Tawala wa Mkoa wa Dodoma Bibi. Rehema Madenge
amesema mafunzo hayo ya mfumo wa Epicor yamelenga kuwapa uelewa Wahasibu juu ya
mabadiliko ya maboresho makubwa yaliyofanywa katika mfumo huo.
“Historia
inaonesha kuwa Halmashauri zetu zilianza matumizi ya mfumo katika toleo
lililojulikana kama Platnum mwaka 1999/2000 na baadaye mfumo ulifanyiwa
maboresho na kufungwa epicor toleo Na 7.2 mwaka 2001 wakati huo mfumo ukiwa
umefungwa katika Halmashauri 38 tu.” Anasema Bibi
Rehema Madenge.
Aidha ameongeza kwa kufafanua kuwa mwaka 2014/15 mfumo uliboreshwa na kuwa epicor toleo la
7.3.5 na kufungwa katika Halmashauri 44 zaidi hivyo kuwa na Jumla ya Halmashauri
82 zilizokuwa zinatumia mfumo, Rehema Madenge.
Julai Mwaka 2012, TAMISEMI ilifanya
maboresho makubwa kwa kuunganisha Halmashauri 133 zilizokuwepo
wakati huo kupitia kampuni ya simu ya taifa TTCL na kuweka epicor
toleo namba 9.05 ambalo limeendelea kutumika hadi sasa. Hata hivyo Halmashauri
zilizoongezeka baadaye zilifungwa epicor toleo namba 10.1 ambalo limeboreshwa
sasa na kuwa 10.2 inayofungwa Halmashauri zote.
Aidha
amesema, matumizi ya epicor toleo namba 10.2 ni hatua kubwa sana katika
utekelezaji wa dhana nzima ya uwazi uwajibikaji na utawala bora katika
usimamizi wa fedha za umma. Hata hivyo amesema, mfumo huo utasaidia Halmashauri
kuondokana na vyeti vya hati chafu na zile zenye mashaka kutokana na mapato na
matumizi ya fedha zote kutakiwa kuingizwa katika mfumo huo.
Kwa
upande wake, Msimamizi wa Mifumo ya Fedha Ofisi ya Rais TAMISEMI Augustino
Manda amesema uboreshaji wa mfumo wa Epicor ni muendelezo wa uboreshaji wa
mifumo ya Serikali kama ilivyofanyika kwa mifumo mingine kama vile mifumo ya
Afya.
Maboresho
mengine yaliyofanyika katika mfumo huo wa Epicor 10.2 ni kwamba
mifumo yote ya msingi ya usimamizi wa fedha katika sekta za umma kwa sasa
itaweza kuwasiliana na kushirikishana taarifa ambapo hapo awali, uongozi na
maafisa katika Mamlaka za Serikali za Mitaa walilazimika kupitia mipango na
bajeti katika mfumo mmoja, mapato katika mfumo mwingine na matumizi kwenye
mfumo mwingine, hivyo kuleta ugumu katika kudhihirisha uwajibikaji, ufanisi na
thamani ya fedha katika matumizi ya fedha za Serikali.
Vile vile utaunganishwa
na mfumo unaowezesha mabenki kulipana Tanzania (TISS) ambao utaruhusu malipo
yote kufanyika kwa njia ya kielektroniki.
Mafunzo
hayo yanafanyika katika vituo sita ambavyo ni Dodoma, Mwanza,
Mtwara, Iringa, Kagera na Mbeya yakijumuisha watumiaji wa mfumo huo ambao ni
Waweka Hazina na Wahasibu na baadaye Maafisa TEHAMA, Maafisa Manunuzi na
Wakaguzi wa Ndani.
Na Zania Miraji DODOMA FM
Comments
Post a Comment