
Serikali imeombwa kuzingatia vigezo
muhimu vinavyotakiwa wakati wa zoezi la kusajili Waganga wa tiba asili ili
kuondoa sintofahamu iliyopo kati ya serikali na waganga wa tiba asili ambao
wamekuwa wakituhumiwa kujihusisha na imani za kishirikina zinazopelekea uwepo
wa mauaji ya watu wenye ualbino nchini.
Kauli hiyo imetoewa na mke wa waziri
mkuu mstaafu mama Tunu Pinda wakati akifungua semina ya siku moja mjini Dodoma
iliyoandaliwa na shirika la Hope
Derivery Foundation iliyowakutanisha watu wenye ualbino na waganga wa tiba
asili kwa lengo la kuondoa sintofahamu iliyopo baina ya makundi hayo mawili.
Amesema kuwa serikali ni vyema
ikazingatia mambo muhimu wakati wa kuwasajili waganga hao kwa kuwashirikisha
viongozi mbalimbali wa maeneo husika ili
kwatambua waganga halali na matapeli na sio kutumia vigezo vya mganga kuwa na matunguli
pekee hali itakayosaidia kukomesha mauaji hayo kwanni wengi wao wanaojuhusisha
na vitendo hivyo ni wale matapeli.
Kwa upande wake katibu wa waganga wa
tiba asili Joseph Lucas Mlitu amesema
kuwa ili kuwabaini waganga wanaojihusisha na vitendo vya mauaji kwa watu wenye
ualbino ni vyema serikali ikawashirikisha waganga wenyewe kwani wao ndio
wanaowatambua yupi ni mganga wa kweli na yupi ambaye ni tapeli.
Naye mkurugenzi wa shirka la hope
derivery foundation bw, Michael
Salali amesema kuwa lengo la kuandaa semina hiyo ni kutoa uelewa kwa waganga wa
tiba asili juu ya watu wenye ualbino ili kuondokana na imani potofu kwani tangu
mwaka 2006 hadi 2018 tayari zaidi ya watu 79 wenye ualbino wameuawa na wengine
kujeruhiwa kwa kukatwa viungo vyao.
NA ALFRED BULAHYA DODOMA FM
Comments
Post a Comment