Skip to main content

SERIKALI YAAHIDI KUPANDISHA MISHAHARA HALI YA UCHUMI ITAKAPOIMARIKA



Image result for Kapten George Mkuchika





Waziri wa Nchi ofisi ya Rais utumishi na utawala bora Kapten George Mkuchika amesema Serikali ya awamu ya tano inaendelea kuboresha masilahi ya watumishi wa umma na itapandisha mishahara kwa watumishi hao baada ya hali ya uchumi wa Nchi kuimarika.

Waziri Mkuchika ameyasema hayo leo Bungeni Jijini Dodoma wakati akijibu swali la Mbunge wa viti maalumu Mh. Catherin Magige aliehoji Serikali ya awamu ya tano ina mikakati gani ya kuwajali watumishi wa umma katika masilahi yao.

Kapten Mkuchika amesema Serikali imekuwa ikifanya juhudi mbalimbali katika kuboresha masilahi ya watumishi wa umma kwa kuwapatia mikopo, kuwapeleka mafunzo katika taaluma mbalimbali na zoezi la kupandisha mishahara litafanyika wakati wowote hali ya uchumi wa Nchi utakapo ruhusu.

Katika hatua nyingine Kapten Mkuchika amekanusha taarifa za zuio kwa wakurugenzi wa Halimashauri, Manispaa pamoja na Majiji juu ya kuto kuwatangaza wapinzani iwapo wameshinda katika chaguzi mbalimbali kutokana na wakurugenzi hao kulipwa mishahara na Serikali hoja iliyoibuliwa na Mbunge wa Jimbo la Ukonga Mh. Mwita Waitala

Kapten Mkuchika amesema swala hilo halina ukweli wowote na badala yake wakurugenzi katika Halmashauri zote Nchini wamepatiwa mafunzo ya uongozi kwa kuzingatia sheria, kanuni na taratibu za Nchi ili kutekeleza majukumu yao ipasavyo kwa mjibu wa sheria.

Na Pius Jayunga                                                      DODOMA FM

Comments

Popular posts from this blog

WAJAWAZITO WASHAURIWA KUTUMIA VIDONGE VYA FOLIC ACID KUEPUKA WATOTO VILEMA

                                                                  Mama wajawazito wameshuriwa kutumia dawa aina ya FOLIC ACID katika kipindi cha miezi mitatu ya mwanzo ya ujauzito ili kuepuka kupata mtoto mwenye   mapungufu. Rai hiyo imetolewa na Daktari kutoka Hospitali ya Matovyolwa mjini Dodoma   Dk.MUBARACK ISSA ALI wakati akizungumza na Dodoma FM juu ya athari zitokanazo na mama kutotumia dawa hizo. Dr Mubarack amesema katika kipindi cha ujauzito mama huwa anapitia changamoto nyingi hivyo ni vyema akatumia dawa aina ya FOLIC ACID ili kuepuka kupata mtoto mwenye tatizo la mgongo wazi, kichwa kikubwa pamoja na upungufu wa damu. Aidha Dk. Mubarack amesema   ili kuepuka kupata mtoto njiti   kipofu na kusababisha kifo kwa mtoto   ni vyema mama akaepuka matumizi ya pombe, dawa za kulev...

MIKOA INAYOONGOZA KWA UKEKETAJI TANZANIA YATAJWA

Mila potofu   katika jamii ya kimasai imetajwa kuwa changamoto kwa maafisa ustawi wa jamii wa halimashauri ya wilaya ya Ngorongoro  kutokana na kukosa ushirikiano wa kutatua Tatizo la ukeketaji kwa jamii hiyo. Akizungumza na waandishi ya habari Afisa Ustawi Wa jamii Bwana ALOYCE  LOLIKISWALI katika semina iliyoandaliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu Sanyansi na Utamaduni UNESCO kwa lengo la kupinga ukeketaji wa wanawake amesema kukosekana kwa ushirikiano kwa jamii imekuwa ni changamoto ambayo imepelekea kushindwa kudhibiti ukeketaji pamoja na ukatili wa kijinsia. Kwa upande wake Mwenyekiti wa Malaigwanan Bwana JOSEPH TIRIPAI amebainisha kuwa mila na desturi zao zitabadilika kulingana na wakati lakini watahakikisha wanalinda watoto wanaozaliwa kutokeketwa na kusisitiza elimu kuendelea kutolewa hususani shuleni. Katika hatua nyingine mratibu wa afya ya mama na mtoto ameeleza kuwa wanawake wajawazito waliokeketwa wanalazimika   kujifug...

MITI YA KIVULI MAARUFU KAMA PANGA UZAZI YAZUA TAHARUKI WILAYANI BAHI DODOMA

                                                  Mganga Mkuu wa Wilaya ya Bahi Jijini Dodoma Dk.Philipina Philipo amewatoa hofu wakazi   wa Wilaya hiyo juu ya taarifa za kuwepo kwa madhara katika miti ya kivuli maarufu kama PANGA UZAZI ambayo imezua hofu kwa wananchi hao. Hoja hiyo imeibuliwa katika kikao cha Baraza la Madiwani wa halmashauri hiyo ambapo baadhi ya madiwani wameomba kupatiwa ufafanuzi kuhusu kuwepo kwa fununu kuwa mti huo una madhara na kuongeza kuwa baadhi ya wananchi wameanza kuikata wakihofia kupatwa na madhara hayo. Akitoa ufafanuzi kuhusu miti hiyo Mganga Mkuu wa Wilaya Dk.Philipina Philipo amesema hadi hivi sasa hakuna utafiti wowote uliofanyika na kubainisha kuwa mti huo hauna madhara hivyo wananchi hawana haja ya kuhofia chochote. Kutokana na Majibu hayo ya DK PHILIPINA yamepelekea kuibua kwa hoja nyingine kwa madi...