Skip to main content

SERIKALI :SIYO JUKUMU LETU KUGHARAMIA MAZISHI YA WAZAZI WA WATUMISHI

                                                         Image result for Naibu waziri ofisi ya Rais tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEM) Mh. Joseph Kakunda               






Serikali imesema haina jukumu la kugharamia huduma za mazishi wazazi  wa mtumishi wa umma wanapofariki kutokana na baadhi ya wazazi kuwa na watoto zaidi ya mmoja.

Naibu waziri ofisi ya Rais tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEM) Mh. Joseph Kakunda ameyasema hayo leo Bungeni Jijini Dodoma kwa niaba ya Waziri ofisi ya Rais utumishi na utawala bora wakati akijibu swali la Mbunge Kosato Chumi aliehoji ni lini Serikali itawajumuisha wazazi wa mtumishi kama wanufaika wa huduma mbalimbali anazopata mtumishi wa umma.

Amesema kwa mujibu wa kanuni za kudumu katika utumishi wa umma inaelekeza huduma za mazishi kutolewa kwa mtumishi mwenyewe pamoja na wategemezi wa nne na uwepo wa kanuni hiyo imesaidia Serikali kuepuka kulipa gharama zaidi ya mara moja kwa mzazi mmoja aliefariki kutokana na kuto kuwepo kwa mfumo wa kutambua wazazi wenye watoto zaidi ya mmoja katika utumishi wa umma.

Mh. Kakunda amesema ili kuziba pengo lililopo katika kuhudumia mazishi ya  wazazi Serikali imeruhusu watumishi wa umma kuchangiana kupitia vyama vya hiari michango ambayo hufunguliwa akaunti maalumu ili kupeana rambirambi wakati mtumishi anapofiwa na mzazi wake mfumo ambao ulianzishwa na umoja wa watumishi.

Katika hatua nyingine Mh. Kakunda ametoa rai kwa watumishi wa umma kujenga tabia ya mahusiano mazuri mahali pa kazi hatua inayoweza kurahisisha watumishi hao kusaidiana wao kwa wao badala ya kutegemea kuingizwaa katika mfumo rasmi wa kugharamiwa na Serikali hasa pale mtumishi anapofiwa na mzazi.

Na Pius Jayunga                                                            DODOMA  FM

Comments

Popular posts from this blog

WAJAWAZITO WASHAURIWA KUTUMIA VIDONGE VYA FOLIC ACID KUEPUKA WATOTO VILEMA

                                                                  Mama wajawazito wameshuriwa kutumia dawa aina ya FOLIC ACID katika kipindi cha miezi mitatu ya mwanzo ya ujauzito ili kuepuka kupata mtoto mwenye   mapungufu. Rai hiyo imetolewa na Daktari kutoka Hospitali ya Matovyolwa mjini Dodoma   Dk.MUBARACK ISSA ALI wakati akizungumza na Dodoma FM juu ya athari zitokanazo na mama kutotumia dawa hizo. Dr Mubarack amesema katika kipindi cha ujauzito mama huwa anapitia changamoto nyingi hivyo ni vyema akatumia dawa aina ya FOLIC ACID ili kuepuka kupata mtoto mwenye tatizo la mgongo wazi, kichwa kikubwa pamoja na upungufu wa damu. Aidha Dk. Mubarack amesema   ili kuepuka kupata mtoto njiti   kipofu na kusababisha kifo kwa mtoto   ni vyema mama akaepuka matumizi ya pombe, dawa za kulev...

MIKOA INAYOONGOZA KWA UKEKETAJI TANZANIA YATAJWA

Mila potofu   katika jamii ya kimasai imetajwa kuwa changamoto kwa maafisa ustawi wa jamii wa halimashauri ya wilaya ya Ngorongoro  kutokana na kukosa ushirikiano wa kutatua Tatizo la ukeketaji kwa jamii hiyo. Akizungumza na waandishi ya habari Afisa Ustawi Wa jamii Bwana ALOYCE  LOLIKISWALI katika semina iliyoandaliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu Sanyansi na Utamaduni UNESCO kwa lengo la kupinga ukeketaji wa wanawake amesema kukosekana kwa ushirikiano kwa jamii imekuwa ni changamoto ambayo imepelekea kushindwa kudhibiti ukeketaji pamoja na ukatili wa kijinsia. Kwa upande wake Mwenyekiti wa Malaigwanan Bwana JOSEPH TIRIPAI amebainisha kuwa mila na desturi zao zitabadilika kulingana na wakati lakini watahakikisha wanalinda watoto wanaozaliwa kutokeketwa na kusisitiza elimu kuendelea kutolewa hususani shuleni. Katika hatua nyingine mratibu wa afya ya mama na mtoto ameeleza kuwa wanawake wajawazito waliokeketwa wanalazimika   kujifug...

MITI YA KIVULI MAARUFU KAMA PANGA UZAZI YAZUA TAHARUKI WILAYANI BAHI DODOMA

                                                  Mganga Mkuu wa Wilaya ya Bahi Jijini Dodoma Dk.Philipina Philipo amewatoa hofu wakazi   wa Wilaya hiyo juu ya taarifa za kuwepo kwa madhara katika miti ya kivuli maarufu kama PANGA UZAZI ambayo imezua hofu kwa wananchi hao. Hoja hiyo imeibuliwa katika kikao cha Baraza la Madiwani wa halmashauri hiyo ambapo baadhi ya madiwani wameomba kupatiwa ufafanuzi kuhusu kuwepo kwa fununu kuwa mti huo una madhara na kuongeza kuwa baadhi ya wananchi wameanza kuikata wakihofia kupatwa na madhara hayo. Akitoa ufafanuzi kuhusu miti hiyo Mganga Mkuu wa Wilaya Dk.Philipina Philipo amesema hadi hivi sasa hakuna utafiti wowote uliofanyika na kubainisha kuwa mti huo hauna madhara hivyo wananchi hawana haja ya kuhofia chochote. Kutokana na Majibu hayo ya DK PHILIPINA yamepelekea kuibua kwa hoja nyingine kwa madi...