
Serikali kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,
Wazee na Watoto leo imekutana na wadau wa maendeleo kujadili hatua zilizofikiwa
katika utekelezaji wa Mpango mkakati wa kutokomeza vitendo vya ukatili dhidi ya
wanawake na watoto hususani eneo la sita la mkakati huo linalohusiana na eneo
la huduma kwa waathirika wa ukatili na unyanyasaji wa watoto nchini.
Wizara kupitia idara ya Ustawi wa Jamii ina jukumu la kusimamia
Mpango Mkakati wa kutokomeza ukatili dhidi ya Wanawake na watoto eneo la sita
la kukabili vitendo vya ukatili na unyanyasaji dhidi ya wanawake na watoto
hivyo leo imeitisha kikao na wadau wa maendeleo kama hatua ya utekelezaji wa
eneo hilo la mkakati.
Akizungumza katika kikao hicho Kaimu Kamishna wa ustawi wa Jamii
Bi. Amina Mafita amewambia wajumbe wa kikao hicho kuwa wanakutana kujulishana
na kupeana taarifa kuhusu hatua za utekelezaji wa mpango mkakati huo katika
juhudi za kutokomeza vitendo vya unyanyasaji na ukatili dhidi ya watoto
kama ilivyo kwenye eneo la sita la mkakati huo.
Aidha Bi. Amina ameongeza kuwa baadhi ya Mashirika
yanayotekeleza eneo la sita la Mkakati wa Kutomeza ukatili dhidi ya Wanawake na
Watoto yatatakiwa kuonesha na kuwataarifu mashirika mengine ya wadau wa
maendeleo kuhusu maeneo yanayayofanyia kazi katika ngazi ya Mkoa, Wilaya mpaka
Kijiji.
Ameyataja maeneo muhimu yakufanyia kazi kwa baadae kuwa ni
kupunguza idadi ya watoto wa mitaani, ajira kwa watoto katika mkakati
hutakaohusisha familia lakini pia kuandaa mwongozo wa uanzishaji wa makazi
salama ya watoto ambao ni wahanga wa ukatili.
Mpango Mkakati wa Kutokomeza Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto
una maeneo nane ya utekelezaji mojawapo ni eneo la sita linalohusiana na
kukabiliana na vitendo vya unyanyasaji na ukatili dhidi ya wanawake na watoto
na utekelezaji wa mapango huu ni wa kipindi cha miaka mitano 2017/2018-2022
MARIAM MATUNDU DODOMA FM
Comments
Post a Comment