Serikali imeahidi kutoa ushirikiano
kwa waganga wa tiba asili katika jitihada za kuwabaini watu
wanaojihusisha na mauaji ya vikongwe na watu wenye Ualbino.
Hatua hiyo imekuja kufatia hivi
karibuni waganga wa tiba asili kuomba kupewa ushirikiano na serikali wakati wa
zoezi la kusajili waganga hao ili kubaini waganga wabaya na wazuri jambo ambalo
litasaidia kuwabaini waganga matapeli wanaojihusisha na vitendo hivyo.
Akiongea na umoja wa waganga wa tiba
asili na wakunga (UWAWATA) pamoja na watu wenye ualbino Mwenyekiti wa
bunge la Jamhuri ya muungano wa Tanzania Mussa Zungu amesema kuwa
waganga wabaya wataendelea kuwepo iwapo wateja wabaya watakuwepo hivyo waganga
wote watoe ushirikiano kwa vyombo vya dola ili hatua zichukuliwe dhidi ya wale
watakaobainika.
Naye kamanda wa polisi mkoa wa
Dodoma Gilles Muroto amewataka kuanza kuibainisha mikoa iliyo na
matukio mengi ya aina hiyo pamoja na kutoa elimu katika mikoa mbalimbali hapa
inchini ikiwemo mkoa wa kagera kwani ndio unaotajwa kuwa na vitendo vingi vya
mauaji.
Hata hivyo ili kuendelea kuboresha
mahusiano baina ya waganga wa tiba asili na watu wenye ualbino nchini
mwenyekiti wa waganga hao Bwana Bujukano Mahungu John kwa niaba ya umoja wa
waganga hao akamtangaza mkurugenzi wa Taasisi ya Hope Derivery Foundation inayoshughulika
na masula ya kupinga ukatili kwa watu wenye ualbino Bwana Michael Salali kuwa
mratibu wa umoja huo hapa nchini.
NA ALFRED BULAHYA DODOMA FM
We are providing online services to customer for SEO and search engine marketing (SEM). They produce more effect result within one month. I am advising you please do not wash your money and time. they are generating organic results and different types of full package on monthly basis.Thank You
ReplyDelete