
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. John Pombe Magufuli
amesema njia pekee itakayosaidia kuinua sekta ya kilimo Nchini ni ma afisa
ugani kutumia matokeo ya utafiti pamoja na kuimarisha vituo vya utafiti vya
kilimo Nchini ili kuongeza fursa ya uzalishaji.
Rais Magufuli ametoa kauli hiyo leo Jijini Dar es salaam wakati
akizindua mpango wa maendeleo ya kilimo awamu ya pili ambapo amesema iwapo
maafisa ugani watatumia matokeo ya utafiti katika sekta ya kilimo yatasaidia
kuinua sekta ya kilimo hapa Nchini.
Amesema chuo kikuu cha sokoine kina wajibu mkubwa wa kusaidia
sekta ya kilimo kwa kufanya tafiti nyingi ikiwemo kubuni teknolojia mpya ambayo
ni rahisi kwa wakulima kama kuhifadhi mazao, kubuni dawa na mbinu za kupambana
na magonjwa ya mimea pamoja na kuanzisha mashamba darasa katika maeneo
mbalimbali Nchini.
Aidha Rais Magufuli ameeleza kuto kuridhishwa na utendaji kazi wa
Bank ya maendeleo ya kilimo Nchini (TADB) na kubainisha kuwa kwa sasa Nchi ina
jumla ya hekta milioni 44, na hekta milioni 29.4 zinafaa kwa kilimo cha
umwagiliaji na katika mifugo Tanzania ikishika nafasi ya pili kwa kuwa na idadi
kubwa ya mifugo barani afrika ikifuatiwa na Ethiopia.
Nae waziri wa kilimo, mifugo na uvuvi Dr. Charles Tizeba amesema
sekta ya kilimo ina uhusiano wa moja kwa moja na sekta ya viwanda kutokana na
baadhi ya malighafi ambazo huzalishwa katika kilimo hutumika pia katika
kuzalisha bidhaa viwandani na kwamba kwa mwaka 2016/17 jumla ya viwanda
vitumiavyo malighafi kutoka sekta ya kilimo vimeongezeka kutoka viwanda 49243
hadi viwanda 52546 mwaka mwaka 2016/17.
Na Pius Jauynga DODOMA FM
Comments
Post a Comment