Kuelekea maadhimisho ya siku ya mazingira
duniani jamii mkoani Dodoma imetakiwa kuhakikisha inatumia vyombo maalumu
vilivyoko katika maeneo yao kuweka uchafu ili kuunga mkono juhudi za serikali
za kuimarisha usafi nchini.
Wito huo umetolewa leo na kaimu afisa mazingira
wa jiji la Dodoma bw, Ally Mfinanga, wakati akiongea na DODOMA FM ikiwa ni
siku moja tu imesalia ili kufikia kilele cha maadhimisho ya siku ya mazingira
duniani.
Amesema kuwa jamii inapaswa kuvitumia vyombo
hivyo kwani vimewekwa kwa ajili ya kazi hiyo ili kuepusha suala la utupaji wa
taka hovyo hivyo kila mmoja Anatakiwa kuzingatia jambo hilo ili kuliweka jiji
la Dodoma katika hali safi.
Akizungumzia hali ya usafi katika jiji la Dodoma
amesema kuwa hali inaendelea kuimarika licha ya elimu ya usafi kuwa ndogo
katika jamii huku akisisitiza wananchi kufanya mabadiliko ya kuhakikisha usafi
unaimarika katika meneo yao ili kuepusha usumbufu wa kuchuliwa hatua ikiwemo
kutozwa faini.
Baadhi ya wananchi wa jiji la Dodoma wameimbaia
Taswira ya habari kuwa kwa sasa hali ya usafi inaendelea kuimarika mkoani hapa
na kwamba serikali inapaswa kuendelea na jitihada za kuhamamsisha suala la
usafi kwani wapo baadhi ya wananchi bado hawana elimu sahihi juu ya utunzaji wa
mazingira.
Maadhimisho ya siku ya mazingira duniani
huadhimishwa kila mwaka ifikapo june 5
na kwa mwaka huu mkoa wa Dodoma yatafanyika katika viwanja vya Nyerere Square huku kitaifa kilele cha maadhimisho
hayo kitafanyika Jijini Dar es salaam kikiwa na kauli mbiu isemayo mkaa
ni gharama tumia nishati mbadala, na kimataifa kauli mbiu inasema Tuongeze
nguvu katika kupambana na taka zitokanazo na plastiki.
NA ALFRED BULAHYA DODOMA FM
Comments
Post a Comment