
Waziri mkuu wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kasimu Majaliwa amewataka watumishi wa umma
kuwa na imani na Serikali ya awamu ya tano katika utekelezaji wa ahadi yake ya
kulipa stahiki za watumishi.
Mh. Kasimu Majaliwa
ameysasema hayo leo Bungeni katika kipindi cha maswali ya papo kwa hapo kwa
Waziri mkuu wakati akijibu swali la Mbunge Suzan Limo aliehoji ni lini Serikali
itawapatia watumishi wa umma stahiki zao kitendo ambacho kinashusha mwamko wa
watumishi hao katika kutimiza majukumu yao.
Waziri mkuu amesema mpango
uliowekwa na Serikali wa kuondoa watumishi wasio kuwa na sifa stahiki umesaidia
kutambua idadi ya watumishi walio na sifa na hatua zilizokwisha anza
kuchukuliwa hadi sasa na Serikali ni kuanza kulipa stahiki za watumishi hao
kupitia fedha zaidi ya bilioni 200 zilizotengwa na Rais Dr. John Pombe
Magufuli.
Akizungumzia juu ya
nyongeza ya mishahara ya watumishi hasa katika nyakati za mei mosi Waziri mkuu
amesema kitendo cha kutangaza nyongeza hizo katika mikutano ya hadhara
huambatana na madhara yake katika jamii ikiwemo swala la kupanda kwa bei ya
bidhaa mbalimbali, kitendo ambacho huleta athari kubwa kwa wananchi hasa
wasiokuwa na mishahara.
Baada ya kukamilika
kwa kipindi cha maswali ya papo kwa hapo kwa Waziri mkuu, Bunge limeendelea na
kipidi cha maswali ya kawaida ambapo Waziri wa maji na umwagiliaji Mhandisi
Isack Kamwele amesema Serikali inapeleka maji katika maeneo ya Sikonge, Urambo,
pamoja na Kariua na utekelezaji wake utaanza katika mwaka wa fedha 2018/19.
Na
Pius Jayunga DODOMA FM
Comments
Post a Comment