
Katika kuhakikisha tatizo la ukosefu wa ajira
kwa vijana nchini linatatuliwa Serikali imesema inaendelea kutekeleza mikakati
mbalimbali ili kukabiliana na tatizo.
Naibu Waziri ofisi ya Waziri mkuu sera,
bunge, kazi, ajira na watu wenye ulemavu Mh. Athony Mavunde ameyasema hayo leo
Bungeni jijini Dodoma wakati akijibu swali la Mbunge wa viti maalumu Mh. Asha
Abdul Juma alietaka kujua ni lini Serikali itafanya juhudi za dhati
kulishughulikia swala hilo ili kuongeza fursa ya ajira.
Naibu waziri Mavunde amesema Serikali imetoa
kipaumbele kwa vijana waliohitimu elimu ya vyuo vya ufundi kwa kupewa
kipaumbele hasa katika mradi wa ujenzi wa reli ya kisasa, ujenzi wa bomba la
mafuta, mradi wa usambazaji umeme vijijini pamoja na mradi wa kufua umeme na
katika mradi wa bomba la mafuta zaidi ya nafasi elfu 11 za ajira mbalimbali
zitapatikana.
Aidha Mh. Mavunde amesema Serikali imeainisha
aina ya ujuzi unaohitajika katika ujenzi
wa miradi husika na tayari imetenga fedha za kugharamia pengo la ujuzi lililopo
kati ya wahitimu pamoja na soko la ajira na kwamba kupitia mfuko wa maendeleo
ya vijana Serikali imeendelea kutoa mikopo yenye mashariti nafuu.
Amevitaja
vituo vya vijana vilivyopo chini ya
ofisi ya Waziri mkuu kuwa ni pamoja na kituo cha vijana Sasanda Mbozi,
kituo cha vijana Ironga kilosa pamoja na kilimanjaro vituo ambavyo vipo kwa
ajili ya kuwalea vijana pamoja na kuwaandaa kuwa na sifa za kuajirika.
Na
Pius Jayunga Dodoma FM
Comments
Post a Comment