Serikali imesema itaendelea kuboresha viwanda vya kuchakata
samaki vilivyopo nchini ili kuhakikisha
bidhaa zinazozalishwa zinakua na ubora na zinaendelea kuwa na soko
kimataifa.
Naibu waziri wa mifugo na uvuvi Abdalla Ulega amesema
wanahakikisha viwanda vinakuwa na uhakika
wa upatikanaji wa mali ghafi pamoja na
kurekebisha sheria zinazosimamia ili kuwezesha serikali kupata mapato
kikamilifu.
Amesema viwanda vya kuchakata samaki vimekuwa na mchango kwa
maendeleo ya nchi kwani mbali na kuingezea serikali mapato pia vimekuwa
vikizalisha ajira miongoni mwa watanzania.
Sekta ya uvuvi imetajwa kuchangia kiasi kidogo cha pato la
taifa ambapo kwa mwaka wa fedha 2017/2018 sekta ya uvuvi ilipangiwa kuchangia
takribani bilioni 19 katika pato la taifa.
Mariam Matundu
DODOMA FM
Comments
Post a Comment