
Waziri
wa elimu sayansi na teknolojia Prof. Joyce Ndalichako amewataka Watanzania hususani
wazazi na walezi kuto kuwaficha watoto walio na ulemavu kwa kuwapatia haki ya
kupata elimu.
Prof.
Ndalichako ameyasema hayo leo wakati akihutubia mamia ya wananchi waliojitokeza
kuaga miili ya Marehemu Maria pamoja na Consolata waliofariki Dunia mwishoni
mwa wiki iliyopita wakati wakipatiwa matibabu katika hospitali ya Mkoa wa Iringa.
Amesema
Serikali ya awamu ya tano imetoa kipaumbele kwa kundi la watu wenye ulemavu kwa
kuwapatia elimu na kwamba jamii inapaswa kuunga mkono juhudi hizo kwa
kuwapeleka shule watoto walio na ulemavu ili kupatiwa haki hiyo stahiki.
Naibu
Waziri ofisi ya Waziri mkuu anaeshughulikia maswala ya watu wenye ulemavu Mh. Stella
Ikupa amesema baadhi ya watu wenye ulemavu wamekuwa wakishindwa kujiamini
kutokana na malezi yatolewayo katika familia zao kwa kukatishwa tamaa jambo
ambalo jamii inapswa kulipinga na kuwatetea watu walio na ulemavu.
Akitoa
salamu za rambirambi kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Iringa, mkuu wa Wilaya ya Makete
Bi. Veronica Kesi amesema Maria na Consolata wameacha somo kwa jamii juu ya
umuhimu wa kuwapatia nafasi watu walio na ulemavu ili kuonesha uwezo wao hasa
katika upande wa elimu.
Mapacha walioungana Maria na Consolata walifariki Dunia siku ya jumamosi
june 2, 2018 wakati wakipatiwa matibabu katika hospitali ya Mkoa wa Iringa na
enzi za uhai wao mapacha hao walifanikiwa kuanza masomo ya juu katika chuo kikuu cha
katoliki cha Ruaha cha mjini Iringa baada ya kufaulu katika mitihani yao ya kidato
cha sita.
Na Pius Jayunga DODOMA
FM
Comments
Post a Comment